Mpango uliovuruga mbwembwe za EX-Girlfriend

Nilikuwa nihadhirike ndugu zangu katika ukumbi wa harusi maeneo ya Mbezi Beach.
Hii ilikuwa harusi ya classmate wangu, ambapo miongoni mwa watu waliohudhuria alikuwa EX girlfriend wangu ambaye baada ya kuachana naye alitengeneza uadui wa hali ya juu.
Siku ya tukio nikiwa miongoni mwa wanakamati mara baada ya kutoka kanisani, macho yangu yanatua moja kwa moja kwa ex- girlfriend akiwa na jamaa yake. Hizo mbwembwe sasa yaani akaja mpaka eneo nililokuwa nimesimama akiwa na jamaa yake wameshikana mikono,akafika na kunisalimia huku akinitambulisha kwa jamaa yake kuwa mimi ni jirani yake huko mtaani kwao. Dah kwa dakika kadhaa nikaona kabisa hapa nishapoteza mechi uwanja wa nyumbani.
Ila kwa kuwa nina uzoefu wa haya mambo, nikapiga hesabu za haraka haraka ili walau nijitutumue tukifika ukumbini.
Wakati huo sikuwa na girfriend, hivyo uwepo wa ex-girlfriend na zile nyodo tena akiwa na jamaa yake ilifanya nione harusi itakuwa ndefu sana.
Nikamkumbuka jirani yangu mmoja, mtoto wa Kinyamwezi mwenye chembechembe za jangwani(uarabuni)huyu alikuwa rafiki tu, ila niliona leo nimtumie ili kusawazisha matokeo kwa EX-girlfriend. Ratiba ya ukumbini ilikuwa saa 12.30 jioni na hapo ni saa 10.30 nikaona haya masaa mawili acha nimpange mtoto wa kinyamwezi.
Baada ya mazungumzo ya dakika 7 ndani ya choo cha kanisa, mtoto wa kinyamwezi akakubali kuja kwa masharti ya kumpelekea usafiri, nikamcheki jamaa yangu dereva babaji pale mwenge amfuate.
Saa 1 kamili usiku, nikiwa ndani ya ukumbi huku ex- girlfriend akiwa na furaha tele na jamaa yake, huku wakionyesha mapenzi na mahaba ya kufunguliana vinywaji, wakiinuka na kucheza kwa kweli hali yangu ilikuwa mbaya.
Mara napata ujumbe ‘’nimefika nipo hapa nje, huyu dereva anataka kuondoka’’, nilitoka na kulipa bajaji huku nikimkata awepo hapo majira ya saa tano kwa ajili ya kumrudisha mrembo. Binti wa kinyamwezi alikuwa amependeza ajabu, kwa ile rangi yake na aina ya gauni aliyovaa, kifua kilichojaa vyema , kiuno kilichokaa mahali pake, sura ya kitoto, macho ya duara , nywele zilizotengezwa vyema kwa hakika mtoto alikuwa amependeza sana.
Sasa nikaone nikabadili matokeo ndani ya ukumbi, nikampanga kabisa binti kwamba ukumbini kuna EX- girlfriend na kwa kweli ameshanitesa sana na jamaa yake. Tukaingia nikiwa nimeshika kiuno cha mtoto wa kinyamwezi na kupita karibu kabisa na alipokaa EX-girlfriend, kwa mwendo wa taratibu kabisa. Nikavuta kiti, binti akapita na kukaa, muda wote huu namwangalia namna EX-girlfriend anavyoniangalia kwa kuibiaibia, tulikaa kwa bashasha huku Mc akikaribisha bibi na bwana harusi kuingia.
Baada ya bibi na bwan harusi kuingia, MC akatangaza anaomba couple tatu zilizopendeza kuja mbele kwa ajili ya kuwasindikiza bibi na bwana harusi kwenye sehemu yao. Sikupoteza muda kwani tuliinuka na binti wa kinyamwezi huku nimemshika kiuno kwa mwendo wa kunesanesa mpaka mbele.
Nikiwa nimekaa text ikaingia kutoka kwa EX-girlfriend ‘’ siku hizi una misifa, huyo chotara sijui umemuokota wapi?’’, nikamjibu kwa kifupi ‘’ nimemuokota ubungo’’, akaendelea ‘’embu kuwa serious huko’’ nikaona huyu tayari sindano imeshamuingia.
Harusi ikasha kila mtu akaenda njia yake.
Asubuhi, napokea meseji nyingine kutoka kwa EX-girlfriend ‘’ naona bado umelala na huyo mwarabu koko wako?’’ nikamjibu kama ‘’wewe ulivyolala na jamaa yako’’ akajibu ‘’ yule sio jamaa yangu ni workmate tu’’
Kilichoendelea kati yangu na x-girlfriend kitakuja siku nyingine.
Huyu dada aliumia sana wakati mimi na binti wa kinyamwezi tulikuwa tunaigiza tu.

Sio kila unachokiona ndivyo kilivyo. Wakati mwingine X anaweza kutaka kukuumiza tu. Relax na ufanye mambo yako.
huyo binti wa kinyamwezi kama.namjua hivi
 
Tatizo ni utapindua meza mara ngapi? Yani dunia hii kuumizwa kupo tu. Utajihusisha na huyo chotara, atakuacha kisha utataka kumwonyeshea tena nk. Hakuna sababu ya kuonyesheana na mtu. Demu alikuwa anajionyesha na workmate wake, na ww ukaamua kumwonyeshea. Alikuingiza mkenge, na ww ukazama. Ukaingia gharama nk. Furaha uliyoipata ni ya muda mfupi. Pambana upate amani ya ukweli. Kama ni $$$, basi pambana uwe nazo. Kama ni familia, pambana uwe nayo. Hayo ya kupindua meza wala hayana mantiki. Hapo hata huyo mwanamke atakuheshima heshima unayistahili. Na sio heshima ya ku-show off.
 
Tatizo ni utapindua meza mara ngapi? Yani dunia hii kuumizwa kupo tu. Utajihusisha na huyo chotara, atakuacha kisha utataka kumwonyeshea tena nk. Hakuna sababu ya kuonyesheana na mtu. Demu alikuwa anajionyesha na workmate wake, na ww ukaamua kumwonyeshea. Ukaingia gharama nk. Furaha uliyoipata ni ya muda mfupi. Pambana upate amani ya ukweli. Kama ni $$$, basi pambana uwe nazo. Kama ni familia, pambana uwe nayo. Hayo ya kupindua meza wala hayana mantiki.
kwake yana mantiki as long he was happy with that
 
Tatizo ni utapindua meza mara ngapi? Yani dunia hii kuumizwa kupo tu. Utajihusisha na huyo chotara, atakuacha kisha utataka kumwonyeshea tena nk. Hakuna sababu ya kuonyesheana na mtu. Demu alikuwa anajionyesha na workmate wake, na ww ukaamua kumwonyeshea. Alikuijgiza mkenge, na ww ukazama. Ukaingia gharama nk. Furaha uliyoipata ni ya muda mfupi. Pambana upate amani ya ukweli. Kama ni $$$, basi pambana uwe nazo. Kama ni familia, pambana uwe nayo. Hayo ya kupindua meza wala hayana mantiki. Hapo hata huyo mwanamke atakuheshima heshima unayistahili. Na sio heshima ya ku-show off.
Umesoma vizuri alichoandika jamaa?

Mwishoni ameandika kuwa mambo mengi ni maigizo kwa wapenzi, jambo la muhimu ni kila mtu kuendelea na maisha yake.

Labda nikuuulize hela ni mbadala wa mapenzi?

Wenye hela huwa hawapitii hizi changamoto za kimapenzi?

Huu muda unaopoteza hapa si ungekuwa unatafuta hela kama hizo hela ndio kila kitu.

Maana hapa mtu akiposti kitu basi watu mnakuja na habari ya hela
 
kwake yana mantiki as long he was happy with that
Watu wengi wanafanya makosa ya kupata furaha feki. Hio ni furaha feki. Demu sio wake. Na sio wa kudumu. Watu wanapenda sana instant gratifications badala ya delayed gratifications. Ili mtu ufanikiwe kimaisha, ni vizuri to focus kwenye delayed gratification.

Kama ni mimi yeye, ningefurahi sana kuona msichana huyo Ex wangu ana mpenzi wake. Ningewapongeza sana sana. Na hata kukaa nao na kuwa rafiki. Nisingeonyesha inaniuma hata kama inauma sababu maumivu ya mapenzi yanaishaga tu.
 
Umesoma vizuri alichoandika jamaa?

Mwishoni ameandika kuwa mambo mengi ni maigizo kwa wapenzi, jambo la muhimu ni kila mtu kuendelea na maisha yake.

Labda nikuuulize hela ni mbadala wa mapenzi?

Wenye hela huwa hawapitii hizi changamoto za kimapenzi?

Huu muda unaopoteza hapa si ungekuwa unatafuta hela kama hizo hela ndio kila kitu.

Maana hapa mtu akiposti kitu basi watu mnakuja na habari ya hela
Suala la hela ni mfano tu. Kuna watu hela inawapa furaha, ndio nikasema waitafute hio. Kuna watu familia inawapa furaha, nikasema watafute familia. Mimi nina hela zangu ndg. Niko sawa kabisa kiuchumi. Napenda JF sababu najifunza mengi. Kuwa na hela haimaanishi kujitenga na watu.
 
Umesoma vizuri alichoandika jamaa?

Mwishoni ameandika kuwa mambo mengi ni maigizo kwa wapenzi, jambo la muhimu ni kila mtu kuendelea na maisha yake.

Labda nikuuulize hela ni mbadala wa mapenzi?

Wenye hela huwa hawapitii hizi changamoto za kimapenzi?

Huu muda unaopoteza hapa si ungekuwa unatafuta hela kama hizo hela ndio kila kitu.

Maana hapa mtu akiposti kitu basi watu mnakuja na habari ya hela
Ww post yangu yote ulichoona ni hela tu? Una matatizo ww.
 
Watu wengi wanafanya makosa ya kupata furaha feki. Hio ni furaha feki. Demu sio wake. Na sio wa kudumu. Watu wanapenda sana instant gratifications badala ya delayed gratifications. Ili mtu ufanikiwe kimaisha, ni vizuri to focus kwenye delayed gratification.

Kama ni mimi yeye, ningefurahi sana kuona msichana huyo Ex wangu ana mpenzi wake. Ningewapongeza sana sana. Na hata kukaa nao na kuwa rafiki. Nisingeonyesha inaniuma hata kama inauma sababu maumivu ya mapenzi yanaishaga tu.
Furaha muda mwingine lazima ufake huwezi kua mnyonge kila saa.
 
bora hata hiyo furaha feki wewe huoni mtoa maada alivyojiona kidume tena mpaka huyo x wake kaumia huo ni ushindi tosha kwake
 
Tatizo ni utapindua meza mara ngapi? Yani dunia hii kuumizwa kupo tu. Utajihusisha na huyo chotara, atakuacha kisha utataka kumwonyeshea tena nk. Hakuna sababu ya kuonyesheana na mtu. Demu alikuwa anajionyesha na workmate wake, na ww ukaamua kumwonyeshea. Alikuingiza mkenge, na ww ukazama. Ukaingia gharama nk. Furaha uliyoipata ni ya muda mfupi. Pambana upate amani ya ukweli. Kama ni $$$, basi pambana uwe nazo. Kama ni familia, pambana uwe nayo. Hayo ya kupindua meza wala hayana mantiki. Hapo hata huyo mwanamke atakuheshima heshima unayistahili. Na sio heshima ya ku-show off.
Paragraph ya mwisho
"... Sio kila unachokiona ndivyo kilivyo. Wakati mwingine X anaweza kutaka kukuumiza tu. Relax na ufanye mambo yako...."
 
Furaha muda mwingine lazima ufake huwezi kua mnyonge kila saa.
Mimi nilikuwa maskini sana, nikaenda abroad nikashika milioni 140 kwa mwaka. Nikaja tz ku-show off. Nikachezea muda na hela sana kupata furaha feki na watu ambao mambo yalipoharibika baadae walinitupa wote.

Mungu akasaidia nikarekebisha mambo na kupata $$ ya kutosha. Naishi maisha yangu ya furaha wala sihitaji ku-show off. Nyumba zipo magari yapo, ila mara moja moja napanda daladala au hata toyo. Heshima yangu iko palepale hata nipande toyo sababu watu wanajua nilivyojijenga kiuchumi.

Ni vizuri kupata heshima halisia na sio sababu ya ku-show off
 
Back
Top Bottom