Mpango uliovuruga mbwembwe za EX-Girlfriend

Mpango uliovuruga mbwembwe za EX-Girlfriend

Hakuna asiye na matatizo. Matatizo yangu sana sana ni ku-deal na wafanyakazi. Sometimes wanavuruga kazi. Sometime si waaminifu nk. Ila matatizo ya $$$ kweli sina. Namshukuru sana Mungu.
Naona na wewe unaigiza kuwa huna matatizo nyuma ya keyboard
 
Mimi nilikuwa maskini sana, nikaenda abroad nikashika milioni 140 kwa mwaka. Nikaja tz ku-show off. Nikachezea muda na hela sana kupata furaha feki na watu ambao mambo yalipoharibika baadae walinitupa wote.

Mungu akasaidia nikarekebisha mambo na kupata $$ ya kutosha. Naishi maisha yangu ya furaha wala sihitaji ku-show off. Nyumba zipo magari yapo, ila mara moja moja napanda daladala au hata toyo. Heshima yangu iko palepale hata nipande toyo sababu watu wanajua nilivyojijenga kiuchumi.

Ni vizuri kupata heshima halisia na sio sababu ya ku-show off
Unaona na wewe unaleta maigizo vilevile katika maisha
 
Wewe unaongelea mfano sahihi na upo sawa kabisa ila katika case study tofauti.

Imagine jamaa angekua mnyonge hapo mpaka sasa angekua anasononeka kwa maigizo ya huyo bibie...
 
Kwa nini uruhusu mtu akupe stress? Kila kitu ni uamuzi. Na ni vizuri kuwa na stress-coping mechanisms ambazo hauhitaji kuita mtu aigize na ww. Ni vizuri kujifunza namna ya ku-handle stress ww mwenyewe au kwa ndg ambao hawahitaji kulipiwa bajaji nk..

Hapna jamaa yupo sahihi kabsa kwa mfano wake...ktk maisha kujiamini ni ktu kizur...jamaa angejiamini angekuwa really asinge fake naamini hyo mwanamke angejiona mjinga ,kwanza jamaa angejiongezea heshima na ule uanaume.
 
Kwa nini uruhusu mtu akupe stress? Kila kitu ni uamuzi. Na ni vizuri kuwa na stress-coping mechanisms ambazo hauhitaji kuita mtu aigize na ww. Ni vizuri kujifunza namna ya ku-handle stress ww mwenyewe au kwa ndg ambao hawahitaji kulipiwa bajaji nk..
Usiwaze sana, hii ni social forum
Watu wapo tofauti, soma kilichoandikwa na endelea na majukumu yako, watu hawafanani, kila mmoja ana mtazamo wake.

Halafu mwisho hizi ni stori tu jamaa ameamua ku-share. Inawezekana ikawa kweli ama ni fiction tu.
 
Nilikuwa nihadhirike ndugu zangu katika ukumbi wa harusi maeneo ya Mbezi Beach.
Hii ilikuwa harusi ya classmate wangu, ambapo miongoni mwa watu waliohudhuria alikuwa EX girlfriend wangu ambaye baada ya kuachana naye alitengeneza uadui wa hali ya juu.
Siku ya tukio nikiwa miongoni mwa wanakamati mara baada ya kutoka kanisani, macho yangu yanatua moja kwa moja kwa ex- girlfriend akiwa na jamaa yake. Hizo mbwembwe sasa yaani akaja mpaka eneo nililokuwa nimesimama akiwa na jamaa yake wameshikana mikono,akafika na kunisalimia huku akinitambulisha kwa jamaa yake kuwa mimi ni jirani yake huko mtaani kwao. Dah kwa dakika kadhaa nikaona kabisa hapa nishapoteza mechi uwanja wa nyumbani.
Ila kwa kuwa nina uzoefu wa haya mambo, nikapiga hesabu za haraka haraka ili walau nijitutumue tukifika ukumbini.
Wakati huo sikuwa na girfriend, hivyo uwepo wa ex-girlfriend na zile nyodo tena akiwa na jamaa yake ilifanya nione harusi itakuwa ndefu sana.
Nikamkumbuka jirani yangu mmoja, mtoto wa Kinyamwezi mwenye chembechembe za jangwani(uarabuni)huyu alikuwa rafiki tu, ila niliona leo nimtumie ili kusawazisha matokeo kwa EX-girlfriend. Ratiba ya ukumbini ilikuwa saa 12.30 jioni na hapo ni saa 10.30 nikaona haya masaa mawili acha nimpange mtoto wa kinyamwezi.
Baada ya mazungumzo ya dakika 7 ndani ya choo cha kanisa, mtoto wa kinyamwezi akakubali kuja kwa masharti ya kumpelekea usafiri, nikamcheki jamaa yangu dereva babaji pale mwenge amfuate.
Saa 1 kamili usiku, nikiwa ndani ya ukumbi huku ex- girlfriend akiwa na furaha tele na jamaa yake, huku wakionyesha mapenzi na mahaba ya kufunguliana vinywaji, wakiinuka na kucheza kwa kweli hali yangu ilikuwa mbaya.
Mara napata ujumbe ‘’nimefika nipo hapa nje, huyu dereva anataka kuondoka’’, nilitoka na kulipa bajaji huku nikimkata awepo hapo majira ya saa tano kwa ajili ya kumrudisha mrembo. Binti wa kinyamwezi alikuwa amependeza ajabu, kwa ile rangi yake na aina ya gauni aliyovaa, kifua kilichojaa vyema , kiuno kilichokaa mahali pake, sura ya kitoto, macho ya duara , nywele zilizotengezwa vyema kwa hakika mtoto alikuwa amependeza sana.
Sasa nikaone nikabadili matokeo ndani ya ukumbi, nikampanga kabisa binti kwamba ukumbini kuna EX- girlfriend na kwa kweli ameshanitesa sana na jamaa yake. Tukaingia nikiwa nimeshika kiuno cha mtoto wa kinyamwezi na kupita karibu kabisa na alipokaa EX-girlfriend, kwa mwendo wa taratibu kabisa. Nikavuta kiti, binti akapita na kukaa, muda wote huu namwangalia namna EX-girlfriend anavyoniangalia kwa kuibiaibia, tulikaa kwa bashasha huku Mc akikaribisha bibi na bwana harusi kuingia.
Baada ya bibi na bwan harusi kuingia, MC akatangaza anaomba couple tatu zilizopendeza kuja mbele kwa ajili ya kuwasindikiza bibi na bwana harusi kwenye sehemu yao. Sikupoteza muda kwani tuliinuka na binti wa kinyamwezi huku nimemshika kiuno kwa mwendo wa kunesanesa mpaka mbele.
Nikiwa nimekaa text ikaingia kutoka kwa EX-girlfriend ‘’ siku hizi una misifa, huyo chotara sijui umemuokota wapi?’’, nikamjibu kwa kifupi ‘’ nimemuokota ubungo’’, akaendelea ‘’embu kuwa serious huko’’ nikaona huyu tayari sindano imeshamuingia.
Harusi ikasha kila mtu akaenda njia yake.
Asubuhi, napokea meseji nyingine kutoka kwa EX-girlfriend ‘’ naona bado umelala na huyo mwarabu koko wako?’’ nikamjibu kama ‘’wewe ulivyolala na jamaa yako’’ akajibu ‘’ yule sio jamaa yangu ni workmate tu’’
Kilichoendelea kati yangu na x-girlfriend kitakuja siku nyingine.
Huyu dada aliumia sana wakati mimi na binti wa kinyamwezi tulikuwa tunaigiza tu.

Sio kila unachokiona ndivyo kilivyo. Wakati mwingine X anaweza kutaka kukuumiza tu. Relax na ufanye mambo yako.
Tar 28 kura zote kwa Magufuli
 
Back
Top Bottom