Mwanaume, tambua sababu 5 za mwanamke kufanya mapenzi na X wake wakati mpo kwenye mahusiano

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Sababu hizi sio kwa ajili ya kuwalaumu wanawake bali ni kwa ajili yako mwanaume, sababu wewe ndo kiongozi na ni jukumu lako kutambua hali na kuchukua hatua. Vingine vinaumiza lakini ndivyo ilivyo. Ila kama mwanamke uliyenaye ana rekodi nzuri ya kudanga, na hajabadilika basi ukae tayari kusalitiwa.

Hana muda mrefu tangu aachane na bwana wake. Muda wa siku moja hadi takribani miezi miwili mwanamke ni rahisi kurudi kufanya mapenzi na ex wake kwa kuwa bado wanajuana au bado wanataka kutatua tatizo na warudiane hivyo usijiingize haraka kwenye mahusiano na mwanamke wa hivyo, utaishia kuumia kama hauna uzoefu mzuri na wanawake.

Ukimpa nafasi kubwa mwanamke/ ukilega kuwa mwanaume jasiri. Ikitokea mwanaume akamuachia uongozi mwanamke, akaanza kumnyenyekea mwanamke ili apendwe zaidi, anamfanyia kila kitu ili amfurahishe, anaendeshwa hovyo na matendo/ maneno ya mwanamke na anateseka lakini anajipa moyo anaogopa kumpoteza huyo mwanamke, mwanaume wa hivyo atahisi anamfurahisha mwanamke lakini ukweli ni kwamba anamuudhi zaidi na kujishushia heshima, mwanamke hatomthamini.

Kama ex wake ni mwanaume jasiri kuliko yeye, mwanamke atataka arudi ili ajisikie raha ya kuongozwa na mwanaume jasiri.

Hivyo ni muhimu ujue jinsi ya kumuongoza mwanamke vizuri ili asahau kuhusu wanaume wengine na akuwaze wewe tu, hayo yote utajifunza katika kundi la infinite kiumeni (whatsapp) na kuishi kwa amani bila wasiwasi mwanamke wako atarudi kwa ex wake.

Ex wake kufanikiwa zaidi ya alipomuacha. Wanawake hawapendi kupitwa na vitu vizuri hata kidogo, atajiona amepoteza dhahabu na kujikuta katika njia panda, je, arudi aone nini kinaendelea au akubali kupitwa na wanawake wenzake.

Mara nyingi huchagua arudi aone nini kinaendelea. Kwaiyo tambua hilo, utaanza kusikia anakuambia vitu kama, umemuona Ibra (ex wake) ana gari mpya, apo lisikuyumbishe ilo jambo, we mpeleke kitandani ukamuendeshe na gari lako.

Ex wake anajua kushawishi/ kuhudumia mwanamke kuliko wewe. Unakuta ex wake ana wanawake wengi, na anajua kuwaridhisha vizuri kitandani, akikutana naye ni wanawake wachache huweza kujizuia. Ili aweze kujizuia lazima umfanye awe anakuwaza wewe zaidi, na ajue akikusaliti atapoteza dhahabu kubwa zaidi ya huyo ex wake.

Hili jambo linaweza kukuumiza hivyo lazima ujikaze na ujifunze jinsi ya kumhudumia mwanamke vizuri kitandani na nje ya kitanda.

Ukianza kumsaliti, kumpotezea au kutomtunza mwanamke. Kama umepata mwanamke mwenye utu na heshima zake kwenye jamii alafu unafanya vitu vya hovyo na hajakusamehe, atakulipizia tu au atafanya usaliti ili naye apate raha uliyomkosesha kwa muda mrefu.

Na sehemu rahisi kukusaliti si pengine bali kwa ex wake. Hivyo kuwa makini usije ukapoteza mwanamke mwenye utu ukaishia kujilaumu.

Ni muhimu kwanza ujue mwanamke uliyenaye ni aina gani, alafu ujue jinsi kumfanya akupende zaidi, yote hayo ni safari hivyo katika kundi la infinite kiumeni tutakua pamoja na utajifunza na wanaume wengine wenye kutaka kufanikiwa katika mapenzi yao, jinsi ya kuvutia na kumtunza mwanawake unayetaka kujenga naye maisha.
 
Sio kwasababu hujawahi kuona, kuamini au kusikia kitu basi hakipo.
Nilikuwa nakuzingua tu bana hata sijasoma bandiko lako lote ila najua nature ya maandiko yako mengi kusuhu mapenzi ni vitu kutoka vitabuni tena kwa wazungu huko na siyo huku kwetu....ambako kila kitu utaambiwa "tafuta pesa"

Usichoke. Endelea kuwaelimisha madogo 👏👏👏
 
Usihangaike na
FB_IMG_16736332356720586.jpg
 
Mleta mada nasikitika kwamba unayoongea kwa asilimia kubwa hayatokei alafu yanayotokea hujahusia hata moja.

Pole sana
 
Back
Top Bottom