Mpango uliovuruga mbwembwe za EX-Girlfriend

Watu wengi wanafanya makosa ya kupata furaha feki. Hio ni furaha feki. Demu sio wake. Na sio wa kudumu. Watu wanapenda sana instant gratifications badala ya delayed gratifications. Ili mtu ufanikiwe kimaisha, ni vizuri to focus kwenye delayed gratification.

Kama ni mimi yeye, ningefurahi sana kuona msichana huyo Ex wangu ana mpenzi wake. Ningewapongeza sana sana. Na hata kukaa nao na kuwa rafiki. Nisingeonyesha inaniuma hata kama inauma sababu maumivu ya mapenzi yanaishaga tu.
Kwa maana nyingine ufeki kutokuumia hata kama unaumia? Mbona kama unapropose kitu kilekile ulichokikataza..
 
Watu wengi wanafanya makosa ya kupata furaha feki. Hio ni furaha feki. Demu sio wake. Na sio wa kudumu. Watu wanapenda sana instant gratifications badala ya delayed gratifications. Ili mtu ufanikiwe kimaisha, ni vizuri to focus kwenye delayed gratification.

Kama ni mimi yeye, ningefurahi sana kuona msichana huyo Ex wangu ana mpenzi wake. Ningewapongeza sana sana. Na hata kukaa nao na kuwa rafiki. Nisingeonyesha inaniuma hata kama inauma sababu maumivu ya mapenzi yanaishaga tu.
Hiyo ni sawa Liverpool alivyokubali kupigwa za kutosha na astonvilla

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa nihadhirike ndugu zangu katika ukumbi wa harusi maeneo ya Mbezi Beach. Hii ilikuwa harusi ya classmate wangu, ambapo miongoni mwa watu waliohudhuria alikuwa EX girlfriend wangu ambaye baada ya kuachana naye alitengeneza uadui wa hali ya juu.

Siku ya tukio nikiwa miongoni mwa wanakamati mara baada ya kutoka kanisani, macho yangu yanatua moja kwa moja kwa ex- girlfriend akiwa na jamaa yake. Hizo mbwembwe sasa yaani akaja mpaka eneo nililokuwa nimesimama akiwa na jamaa yake wameshikana mikono,akafika na kunisalimia huku akinitambulisha kwa jamaa yake kuwa mimi ni jirani yake huko mtaani kwao. Dah kwa dakika kadhaa nikaona kabisa hapa nishapoteza mechi uwanja wa nyumbani.

Ila kwa kuwa nina uzoefu wa haya mambo, nikapiga hesabu za haraka haraka ili walau nijitutumue tukifika ukumbini. Wakati huo sikuwa na girfriend, hivyo uwepo wa ex-girlfriend na zile nyodo tena akiwa na jamaa yake ilifanya nione harusi itakuwa ndefu sana.

Nikamkumbuka jirani yangu mmoja, mtoto wa Kinyamwezi mwenye chembechembe za jangwani(uarabuni)huyu alikuwa rafiki tu, ila niliona leo nimtumie ili kusawazisha matokeo kwa EX-girlfriend. Ratiba ya ukumbini ilikuwa saa 12.30 jioni na hapo ni saa 10.30 nikaona haya masaa mawili acha nimpange mtoto wa kinyamwezi.

Baada ya mazungumzo ya dakika 7 ndani ya choo cha kanisa, mtoto wa kinyamwezi akakubali kuja kwa masharti ya kumpelekea usafiri, nikamcheki jamaa yangu dereva babaji pale mwenge amfuate.

Saa 1 kamili usiku, nikiwa ndani ya ukumbi huku ex- girlfriend akiwa na furaha tele na jamaa yake, huku wakionyesha mapenzi na mahaba ya kufunguliana vinywaji, wakiinuka na kucheza kwa kweli hali yangu ilikuwa mbaya.

Mara napata ujumbe ‘’nimefika nipo hapa nje, huyu dereva anataka kuondoka’’, nilitoka na kulipa bajaji huku nikimkata awepo hapo majira ya saa tano kwa ajili ya kumrudisha mrembo. Binti wa kinyamwezi alikuwa amependeza ajabu, kwa ile rangi yake na aina ya gauni aliyovaa, kifua kilichojaa vyema , kiuno kilichokaa mahali pake, sura ya kitoto, macho ya duara , nywele zilizotengezwa vyema kwa hakika mtoto alikuwa amependeza sana.

Sasa nikaone nikabadili matokeo ndani ya ukumbi, nikampanga kabisa binti kwamba ukumbini kuna EX- girlfriend na kwa kweli ameshanitesa sana na jamaa yake. Tukaingia nikiwa nimeshika kiuno cha mtoto wa kinyamwezi na kupita karibu kabisa na alipokaa EX-girlfriend, kwa mwendo wa taratibu kabisa. Nikavuta kiti, binti akapita na kukaa, muda wote huu namwangalia namna EX-girlfriend anavyoniangalia kwa kuibiaibia, tulikaa kwa bashasha huku Mc akikaribisha bibi na bwana harusi kuingia.

Baada ya bibi na bwan harusi kuingia, MC akatangaza anaomba couple tatu zilizopendeza kuja mbele kwa ajili ya kuwasindikiza bibi na bwana harusi kwenye sehemu yao. Sikupoteza muda kwani tuliinuka na binti wa kinyamwezi huku nimemshika kiuno kwa mwendo wa kunesanesa mpaka mbele.

Nikiwa nimekaa text ikaingia kutoka kwa EX-girlfriend ‘’ siku hizi una misifa, huyo chotara sijui umemuokota wapi?’’, nikamjibu kwa kifupi ‘’ nimemuokota ubungo’’, akaendelea ‘’embu kuwa serious huko’’ nikaona huyu tayari sindano imeshamuingia. Harusi ikasha kila mtu akaenda njia yake.

Asubuhi, napokea meseji nyingine kutoka kwa EX-girlfriend ‘’ naona bado umelala na huyo mwarabu koko wako?’’ nikamjibu kama ‘’wewe ulivyolala na jamaa yako’’ akajibu ‘’ yule sio jamaa yangu ni workmate tu’’Kilichoendelea kati yangu na x-girlfriend kitakuja siku nyingine. Huyu dada aliumia sana wakati mimi na binti wa kinyamwezi tulikuwa tunaigiza tu.

Sio kila unachokiona ndivyo kilivyo. Wakati mwingine X anaweza kutaka kukuumiza tu. Relax na ufanye mambo yako. Unaweza kujikuta unafanya jambo miaka mingi ijayo utabaki unacheka tu.

Embu share na wewe jinsi ulivyokabililana na tukio la kuletewa majivuno na ex- wako.

Furaha ni muhimu kwa afya.
ahahaha,nadhani na mzigo alikupa ukala
 
Ni wanawake wajinga wajinga wasio na msimamo tu ndo huona wivu na kukubali kuvua eti kisa kakuona na mwanamke mkali kumzidi, mi nikikukatalia hata uje na Lori la mfanano wa malaika nitakukataa tu.
 
Wengine wanakuwa hawana sababu ya msingi kukataa, ndo maana ukitikisa kidogo tu nao hao wanaingia kingi, ila Kama unazo sababu mahsusi za kumkataa mtu na unajielewa pyeeeee atakudolishia wazuri wote na wewe ukibaki na msimamo huo huo.
 
Mimi nilikuwa maskini sana, nikaenda abroad nikashika milioni 140 kwa mwaka. Nikaja tz ku-show off. Nikachezea muda na hela sana kupata furaha feki na watu ambao mambo yalipoharibika baadae walinitupa wote.

Mungu akasaidia nikarekebisha mambo na kupata $$ ya kutosha. Naishi maisha yangu ya furaha wala sihitaji ku-show off. Nyumba zipo magari yapo, ila mara moja moja napanda daladala au hata toyo. Heshima yangu iko palepale hata nipande toyo sababu watu wanajua nilivyojijenga kiuchumi.

Ni vizuri kupata heshima halisia na sio sababu ya ku-show off
Ujumbe murua!
 
Umesoma vizuri alichoandika jamaa?

Mwishoni ameandika kuwa mambo mengi ni maigizo kwa wapenzi, jambo la muhimu ni kila mtu kuendelea na maisha yake.

Labda nikuuulize hela ni mbadala wa mapenzi?

Wenye hela huwa hawapitii hizi changamoto za kimapenzi?

Huu muda unaopoteza hapa si ungekuwa unatafuta hela kama hizo hela ndio kila kitu.

Maana hapa mtu akiposti kitu basi watu mnakuja na habari ya hela
ndio jf ilivyo wazoeeni hawa
 
Suala la hela ni mfano tu. Kuna watu hela inawapa furaha, ndio nikasema waitafute hio. Kuna watu familia inawapa furaha, nikasema watafute familia. Mimi nina hela zangu ndg. Niko sawa kabisa kiuchumi. Napenda JF sababu najifunza mengi. Kuwa na hela haimaanishi kujitenga na watu.
furaha ya kweli ipo kwenye ushindi siku zote. Iwe kiuchumi, kisiasa au kiimani! Winning is happiness...
 
Nilikuwa nihadhirike ndugu zangu katika ukumbi wa harusi maeneo ya Mbezi Beach. Hii ilikuwa harusi ya classmate wangu, ambapo miongoni mwa watu waliohudhuria alikuwa EX girlfriend wangu ambaye baada ya kuachana naye alitengeneza uadui wa hali ya juu.

Siku ya tukio nikiwa miongoni mwa wanakamati mara baada ya kutoka kanisani, macho yangu yanatua moja kwa moja kwa ex- girlfriend akiwa na jamaa yake. Hizo mbwembwe sasa yaani akaja mpaka eneo nililokuwa nimesimama akiwa na jamaa yake wameshikana mikono,akafika na kunisalimia huku akinitambulisha kwa jamaa yake kuwa mimi ni jirani yake huko mtaani kwao. Dah kwa dakika kadhaa nikaona kabisa hapa nishapoteza mechi uwanja wa nyumbani.

Ila kwa kuwa nina uzoefu wa haya mambo, nikapiga hesabu za haraka haraka ili walau nijitutumue tukifika ukumbini. Wakati huo sikuwa na girfriend, hivyo uwepo wa ex-girlfriend na zile nyodo tena akiwa na jamaa yake ilifanya nione harusi itakuwa ndefu sana.

Nikamkumbuka jirani yangu mmoja, mtoto wa Kinyamwezi mwenye chembechembe za jangwani(uarabuni)huyu alikuwa rafiki tu, ila niliona leo nimtumie ili kusawazisha matokeo kwa EX-girlfriend. Ratiba ya ukumbini ilikuwa saa 12.30 jioni na hapo ni saa 10.30 nikaona haya masaa mawili acha nimpange mtoto wa kinyamwezi.

Baada ya mazungumzo ya dakika 7 ndani ya choo cha kanisa, mtoto wa kinyamwezi akakubali kuja kwa masharti ya kumpelekea usafiri, nikamcheki jamaa yangu dereva babaji pale mwenge amfuate.

Saa 1 kamili usiku, nikiwa ndani ya ukumbi huku ex- girlfriend akiwa na furaha tele na jamaa yake, huku wakionyesha mapenzi na mahaba ya kufunguliana vinywaji, wakiinuka na kucheza kwa kweli hali yangu ilikuwa mbaya.

Mara napata ujumbe ‘’nimefika nipo hapa nje, huyu dereva anataka kuondoka’’, nilitoka na kulipa bajaji huku nikimkata awepo hapo majira ya saa tano kwa ajili ya kumrudisha mrembo. Binti wa kinyamwezi alikuwa amependeza ajabu, kwa ile rangi yake na aina ya gauni aliyovaa, kifua kilichojaa vyema , kiuno kilichokaa mahali pake, sura ya kitoto, macho ya duara , nywele zilizotengezwa vyema kwa hakika mtoto alikuwa amependeza sana.

Sasa nikaone nikabadili matokeo ndani ya ukumbi, nikampanga kabisa binti kwamba ukumbini kuna EX- girlfriend na kwa kweli ameshanitesa sana na jamaa yake. Tukaingia nikiwa nimeshika kiuno cha mtoto wa kinyamwezi na kupita karibu kabisa na alipokaa EX-girlfriend, kwa mwendo wa taratibu kabisa. Nikavuta kiti, binti akapita na kukaa, muda wote huu namwangalia namna EX-girlfriend anavyoniangalia kwa kuibiaibia, tulikaa kwa bashasha huku Mc akikaribisha bibi na bwana harusi kuingia.

Baada ya bibi na bwan harusi kuingia, MC akatangaza anaomba couple tatu zilizopendeza kuja mbele kwa ajili ya kuwasindikiza bibi na bwana harusi kwenye sehemu yao. Sikupoteza muda kwani tuliinuka na binti wa kinyamwezi huku nimemshika kiuno kwa mwendo wa kunesanesa mpaka mbele.

Nikiwa nimekaa text ikaingia kutoka kwa EX-girlfriend ‘’ siku hizi una misifa, huyo chotara sijui umemuokota wapi?’’, nikamjibu kwa kifupi ‘’ nimemuokota ubungo’’, akaendelea ‘’embu kuwa serious huko’’ nikaona huyu tayari sindano imeshamuingia. Harusi ikasha kila mtu akaenda njia yake.

Asubuhi, napokea meseji nyingine kutoka kwa EX-girlfriend ‘’ naona bado umelala na huyo mwarabu koko wako?’’ nikamjibu kama ‘’wewe ulivyolala na jamaa yako’’ akajibu ‘’ yule sio jamaa yangu ni workmate tu’’Kilichoendelea kati yangu na x-girlfriend kitakuja siku nyingine. Huyu dada aliumia sana wakati mimi na binti wa kinyamwezi tulikuwa tunaigiza tu.

Sio kila unachokiona ndivyo kilivyo. Wakati mwingine X anaweza kutaka kukuumiza tu. Relax na ufanye mambo yako. Unaweza kujikuta unafanya jambo miaka mingi ijayo utabaki unacheka tu.

Embu share na wewe jinsi ulivyokabililana na tukio la kuletewa majivuno na ex- wako.

Furaha ni muhimu kwa afya.
Kachero mbobezi
 
Ni wanawake wajinga wajinga wasio na msimamo tu ndo huona wivu na kukubali kuvua eti kisa kakuona na mwanamke mkali kumzidi, mi nikikukatalia hata uje na Lori la mfanano wa malaika nitakukataa tu.
Kwanini unafikiri wewe ndiyo mwenye akili na hao wengine wajinga?
 
Wengine wanakuwa hawana sababu ya msingi kukataa, ndo maana ukitikisa kidogo tu nao hao wanaingia kingi, ila Kama unazo sababu mahsusi za kumkataa mtu na unajielewa pyeeeee atakudolishia wazuri wote na wewe ukibaki na msimamo huo huo.
Ni sawa unaweza kuwa mzuri sana kwenye eneo hili ila kuna eneo upo dhaifu sana.
Chukua dakika 2 tu kuwaza upuuzi uliowahi kufanya katika mapenzi.
 
Watu wengi wanafanya makosa ya kupata furaha feki. Hio ni furaha feki. Demu sio wake. Na sio wa kudumu. Watu wanapenda sana instant gratifications badala ya delayed gratifications. Ili mtu ufanikiwe kimaisha, ni vizuri to focus kwenye delayed gratification.

Kama ni mimi yeye, ningefurahi sana kuona msichana huyo Ex wangu ana mpenzi wake. Ningewapongeza sana sana. Na hata kukaa nao na kuwa rafiki. Nisingeonyesha inaniuma hata kama inauma sababu maumivu ya mapenzi yanaishaga tu.
tatzo unachukulia sana vitu serious vingine ni vya muda huo huo tu na vinapita
 
Kwani kuchukulia hii issue serious kuna tatizo? Nimechukulia serious na nimeweza kuchangia, kuelimisha wengine, na kuelimika pia. Watu kama ww ambao kila kitu kwenye maisha mnaona ni mzaha hamfanikiwi kabisa. Badilika ndg yangu. Vitu vya kupuuzia ni kama mtu anayekufuatilia maisha yako, watu wakikuongelea nk. Hayo ndio mambo ya kupuuzia sababu ukiya-mind yatakupotezea muda. Ila mambo yanayoathiri maendeleo, watu kama sisi tunayachukulia serious sana sababu napenda kuona community yote inakuwa na maendeleo.
 
Mambo ya kishamba sana...ingelikua mimi ningekausha tu kama unaenda sehemu peke yako unaenda peke yako..mambo sijui kushindana na mwanamke unawaachia wanawake...
 
Back
Top Bottom