Mpangaji wangu kashindwa kunilipa kodi

Mpangaji wangu kashindwa kunilipa kodi

Kama vipi we mtafune huyo mke wa huyo jamaa ujipoze, yaani anakuandikia hadi SMS hujiongezi tu mkuu!! unafeli sana ningekuwa katika position yako nishakula kitumbua zaman!!
 
kaka umesema maneno magumu mno, ila kumbuka nimewavumila mno mwaka wa pili sasa jamani...kweli? yaani hela ya kodi miaka miwili
Kama umeweza kuvumilia miaka miwili sina shaka na moyo wako kwa kuwa najua ni mzuri,hivyo kwa uvumilivu huo huo nakuomba usichoke kutenda wema huo zaidi kwa kuwa hajagoma lakini ni hali tu ngumu kwake.
 
Mkuu hicho ndicho kimesababisha nilete hii mada hapa, yule binti pamoja na mitihani huwa anani sms kuniomba nisiwatimue wazazi wake... huwa nampa moyo kwamba binti endelea na mitihani yako tu usijali siwezi kufanya hivyo - yaani haya maisha jamani laaah
Kama binti anasoma shule ambayo wanaruhusu mtoto kuwa na simu ya kuchati na baba mwenye nyumba, hiyo familia ni ya kutimulia mbali.
 
Ni majaribu makubwa. Mi yalinikuta nilikuwa na Mpangaji driver wa malori ya mafuta. Kuna la mchezo walikuwa wanachezaga ngoma ikasanuka akafungwa miaka 3 huko Zambia. Mke wake na kichanga vikawa mzigo kwangu. Ikabidi niingize kwenye list ya familia yangu kwa maana kula , matibabu na Huduma zingine. Deni nilisamehe (ingawa si kiasi kikubwa kama chako). Jamaa alitoka jela na baada ya miezi 6 kalipa deni lote na ziada juu.
Sasa hivi ni zaidi ya ndugu kwangu ingawa hawapo tena kwangu kwani wamejenga huko Kisemvule.

Sema na moyo wako ingawa uwezekano wa kulipwa siuoni kwa issue yako.
ubarikiwe mkuu watu kama wewe ni wachache sana🙏🙏🙏
 
Huyu mpangaji wangu nimemvumilia sana, ni mwaka wa pili sasa anasema mambo yake hayako vizuri, nikienda kumdai kodi yeye na mkewe wanalia sana kwamba nizidi kuwavumilia.

Kuna binti yao yupo form four huyo naye anajiunga nao kunililia anasema baba tusaidie tu babaa tutakulipa huku kanipigia magoti kushika viatu vyangu na suruali.

Imefikia hatua mke wa jamaa ananiandikia sms kuniomba niendelee niwavumilia, hata binti naye anaandikia sms kunipa shikamoo na kuniambia baba naomba tuvumilie tu maana baba yangu hana hela kabisa hata mimi nasoma kwa shida sana babangu.

Anapofanyia kazi huyo jamaa napajua na anapofanyia kazi huyo mkewe napajua ila siwezi kuwaambia sababu ya kulinda maudhui ya hapa JF.

Nipeni ushauri ila mimi naona ni kuwatimua tu tarehe 30th November hii, kifupi kila mtu atabeba sanduku lake mwenyewe na hapa mjini kila mtu kaja kivyake.
Unawadai kodi kiasi gani mhenga?
 
kama huwa haupatagi shida za kuomba Msaada watimue tu...
Ila kama na wewe unapataga shida mpaka unahitaji ndugu jamaa wakusaidie, Wavumilie tu...
Shida ni Rafiki tunaeishi nae kwenye dhiki...
 
Timua haiwezekani mtu umefulia alafu bado anakomaa kupanga nyumba ya kodi ya laki 3 kwa mwezi kuna watu wanapokea milioni kwa mwezi lakini wanaishi nyumba ya chini ya 200000

Hao bado hawajakubaliana na hali tena unaweza kukuta wanamiliki na chombo cha usafiri na kufanya outings kama.kawaida. pia utakuta kwenye vikao vya harusi wao ni wanakamati na wanatoa madau makubwa.

Mimi nimepatwa na majanga kibao yaani hao wapangaji wanakuchukulia poa sana Tena wameajiriwa mke na mme. Ata shetani ana majaribu mkuu usizani upole ndio tiketi ya kwenda peponi ama ukali ni tiketi ya kwenda motoni nazani pepo la umasikini linakuandama wafuatilie kwa akili zaidi kuliko hisia huenda ata apajamii forum wapo.....haikuwa vema kutaja taarifa zao sahii kama kidato cha mtoto ungesema ata yupo form two .....kama hawajakuloga kuwa makini kwenye kudai chako unaweza kupoteza vingi kimchezo mchezo bila kujua mwanzo wala mwisho.
Sitaki kusema huo mkasa kwani sio lazima na wewe mwisho wako uwe vile inaweza isitokee ukafanikiwa zaidi amaukabaki kama ulivo ama kisibadilike chochote uwe umepata tu story ya kusimulia mbeleni ama wewe ndio uje kuwa story ya kusimuliwa huko mbeleni
 
UNAAMUA KUWAHURUMIA NA KUA NA UTU, unawavumilia mwisho wa siku wanakuja kutoroka na kwenda kupanga kwingine na kodi wanalipa. Binadamu sisi tuna hatari sana.

MAONI YANGU: Naomba uwahurumie na kuwasaidia kwa changamoto wanayoipitia pia kama itakupendeza dai nusu ya kodi unayodai
 
Unawadai Pesa Ndefu Sana,kama Vp Jimilikishe Huyo Binti Ili Ijulikane Unakaa Na Ndugu Zako!!
 
FUSO,

Serikali inadaiwa trilioni 43 na haijauzwa, na wewe unadai visenti unabwatuka, kuwa na utu kama serikali
 
kaka Maisha ni SIASA na ndiyo maana kila nikiwadai wananijibu siasa tupu - ndo nimekuja hapa mnipe ushauri ila sitaki ushauri wa kisiasa.
Waambie walipe mwezi mmoja mmoja kila mtu ana matatizo yake
 
Nyumba yako,umejenga kwa pesa zako bado ushauri kwetu,be serious mkuu NB: zingatia utu pia
 
kaka pango ni Sh 300,000 kwa mwezi, kwa mwaka ni Tsh 3,600,000 kwa miaka miwili ni 7.2m. ni hela nyingi sana wakuu.
Mkuu wape notisi miezi mitatu tu nyumba ya laki 3 mtu mwenye shida hapamfai hapo waambie wasogee nje ya mji kuna vyumba hadi vya 25k wahamie huko.
Kama umewabeba 2yrs mkuu its enough.
 
Huyu mpangaji wangu nimemvumilia sana, ni mwaka wa pili sasa anasema mambo yake hayako vizuri, nikienda kumdai kodi yeye na mkewe wanalia sana kwamba nizidi kuwavumilia.

Kuna binti yao yupo form four huyo naye anajiunga nao kunililia anasema baba tusaidie tu babaa tutakulipa huku kanipigia magoti kushika viatu vyangu na suruali.

Imefikia hatua mke wa jamaa ananiandikia sms kuniomba niendelee niwavumilia, hata binti naye anaandikia sms kunipa shikamoo na kuniambia baba naomba tuvumilie tu maana baba yangu hana hela kabisa hata mimi nasoma kwa shida sana babangu.

Anapofanyia kazi huyo jamaa napajua na anapofanyia kazi huyo mkewe napajua ila siwezi kuwaambia sababu ya kulinda maudhui ya hapa JF.

Nipeni ushauri ila mimi naona ni kuwatimua tu tarehe 30th November hii, kifupi kila mtu atabeba sanduku lake mwenyewe na hapa mjini kila mtu kaja kivyake.
Huenda hata nyumba huna unalala kwa shemeji yako
 
kaka siwezi, hiyo ni nyumba yangu ya kwanza ya ujana - nimejenga kwa kujinyima sana, sikukaa bar kula bia na nyama choma kama vijana wengine, nilipanda daladala kwenda na kurudi jo, sikutaka kununua gari kama vijana wengine walivyokuwa wanatesa wakati huo, sikwenda club bali ni kukaa kwenye chumba changu kimoja huku kila senti niipatayo ikiingia kwenye ujenzi.... nikajenga nikamaliza....Nyumba yangu ya ujana inaniuma sana, watalipa tu ngoja nisubiri huyo binti yao amalize paper ili nilianzishe timbwili.
Ohoooo kumbe huwezi kusamehe mkuu?
 
Yani maisha magumu sn.Me mwenyewe hapa nadaiwa balaa pango ila mwenye nyumba kaelewa Na ameniacha tu maana pamoja na kuwa ana ukwasi ila anakumbuka alikotoka kulikuwa kugumu sana.Nawaza hapa nianze punguza deni kwa kasi mpaka liishe.Mungu atanisaidia.
 
Wameamua na wamefanikiwa kuishi bure. Nilifikiri hawana kazi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom