.Mkuu Fuso, imenigusa. Kwani hadi leo hii tuusomapo ujumbe wako huu unawadai kodi ya miezi mingapi?
Kodi ni Haki yako na Lazima Uipate, lakini kuna wakati mwingine unajiwa na mitihani ambayo hujui hata inatokea wapi!
Kuna wakati huko nyuma katika maisha haya ya Upambanaji nilijikuta nikilazimika kupitisha miezi miTano kwenye Nyumba ya MTU bila kulipa Kofi!
Ilipofika miezi miwili nilimfuata baba Mwenye Nyumba na kumuambia kuwa anivumilie tu kwa sababu Kofi in Haki take na angeipaya tu ila nilikuwa nimesimamishwa kibarua nilipokuwa ninatumika...lakini Kodi take nisingeondoka Nyumba ile bila kumpa Kodi yake, hats kwa kukuacha vyombo vyote ninavyomiliki!
Ninamshukuru sana Mzee wangu yule alinielewa na akauchuna kuhusu suala la Kodi.
Nadhani alikuwa anaona pia hats suala la Diet lilivyokuwa hafifu kwa Mimi, make wangu na watoto wawili.
Ndio maana hats alipoenda mahali kama ferry kuchukuwa kitoweo cha jumla cha familia take, hakukosa kuniita na kunitupia samaki wawili watatu nasi tupate japo samaki Wa kukaanga...hata kama hatuna Unga.
Yakapita. Siku ya Siku mitihani ikaisha na nikaweza sio tu Kumlipa Mzee wangu yule Kodi ya Miezi Mitano niliyopitisha Bali nikaweza hata kulipa Kodi ya Mwaka Mzima.
Haishangazi sana miaka michache baadaye nikiwa ndani ya kakibanda kangu Siku niliyoletewa taarifa ya Mzee yule kufariki dunia ilikuwa Siku ya Huzuni sana Ndani ya Nyumba yangu...
Ndugu yangu Fuso, in Haki yako kupata Kodi ya Nyumba yako lakini pia iangalie hip familia ya Wapangaji wako.
Unawadai Kofi ya miezi mingapi?
Haki yako ya maisha ikoje!
Lishe yao ikoje?
Mwanaume mwenzako amepatwa na dharuba gani ya maisha?
Fahamu tu huko chumbani atakuwa anapata dharuba Kali zaidi kuliko ya unavyomdai yeye...ile ya kutoka kwa Make ya kwa Mimi hajajenga!!!
Tafakari, na chukua hatua njema Mkuu!!