Mpangaji wangu kashindwa kunilipa kodi

Mpangaji wangu kashindwa kunilipa kodi

Observation:
Nimeona umem-mention huyo binti yao wa form 4 mara mbili bila reason yeyote ya maana.


My take:
Kwa kuwa umeweza kuwavumilia miaka miwili mi naamini unaweza kuwavumilia kwa lifetime na kuwamilikisha kabisa hapo wanapokaa pawe mali yao
Umeshindwa kung'amua tu, huyo binti ni mwanafunzi kidato cha nne, Mr Fuso anajali elimu ya mtoto na maisha yake huko mbelen..angewatimua siku za nyuma , angemvuruga sana huyo mtoto upande wa elimu yake, ameamua kukaa kama mzazi....
 
kaka pango ni Sh 300,000 kwa mwezi, kwa mwaka ni Tsh 3,600,000 kwa miaka miwili ni 7.2m. ni hela nyingi sana wakuu.
Duh hela nyingi kweliii. Ushauri wangu wasamehe hiyo kodi ila waambie wakuachie nyumba yako wakapange sehemu ingine yakodi ndogo
 
Duh hela nyingi kweliii. Ushauri wangu wasamehe hiyo kodi ila waambie wakuachie nyumba yako wakapange sehemu ingine yakodi ndogo
kaka siwezi, hiyo ni nyumba yangu ya kwanza ya ujana - nimejenga kwa kujinyima sana, sikukaa bar kula bia na nyama choma kama vijana wengine, nilipanda daladala kwenda na kurudi jo, sikutaka kununua gari kama vijana wengine walivyokuwa wanatesa wakati huo, sikwenda club bali ni kukaa kwenye chumba changu kimoja huku kila senti niipatayo ikiingia kwenye ujenzi.... nikajenga nikamaliza....Nyumba yangu ya ujana inaniuma sana, watalipa tu ngoja nisubiri huyo binti yao amalize paper ili nilianzishe timbwili.
 
ili usiendelee kupata hasara zaidi kwenye nyumba yako..Fanya hivi

~waombe watafute nyumba ya uwezo wao
~walipie kodi ya miezi 6
~pia ingia nao mkataba namna watakavorejesha pesa yako.!

*usiangalie faida sana

**ONYO...kamwe usiwafukuze kwenye nyumba yako;na imeshindikana kabisa wape chumba kimoja waendelelee kuishi hapo.
 
Daaah miaka miwili?..mimi uvumilivu huishia mwezi tu. Hongera kwa roho safi. Ingawa inaonyesha unasubiria kulipwa fadhila pindi binti atakapomaliza.
 
Si akulipe tu huyo mke wake au angalia yupi akulipe kati ya mke na binti,lakini mimi naona wakulipe wote wawili,mke na binti,hata wenyewe wameonyesha nia ya kukulipa
 
Kweli wewe ni FUSO! umewabeba wapangaji wako ukaja kuwamwaga jukwaa la siasa!!
Hakuona pa' kuwamwagia😂😂😂 ila kama mtu hana pesa ya kulipa kodi si amuache tu, akimfukuza atakwenda wapi na familia yake.
 
Dah mzee wana bahati sana ,mimi nilipanga sehemu kipindi cha nyuma ,nikawa nalipa miezi 6 na hapo hapo mwenye nyumba akiwa na shida kodi yangu bado haijaisha nampa tena kodi ...

Ajabu siku nilipokuja kwama nikamwambia saiv siwezi lipa miezi 6 nina miezi mitatu ,alikataa na sababu mbali mbali ,oooh namtoto anasomesha shule ya ghali ,basi nikamwambia kodi yangu ikiisha ntahama ,kweli nikajikusanya nikamaliza kwangu hivyo hivyo nikahamia ,nikamwachia nyumba yake ampate mteja wakumpa miezi 6 , basi kwa miezi 3 alikuwa anatafta mpangaji mpaka kahisi labda nyumba nimeichawia kumbe wapi ,wakati mwingine masononeko na kumnyanyasa mtu ,mungu hukupiga kofi
 
Kama kweli una mpango wa kuwadai hiyo pesa ya rent ya miaka miwili basi hakikisha nyaraka za mikataba ya pango unayo. Maana utaihitaji wakati wa madai hayo.
 
Umeshindwa kung'amua tu, huyo binti ni mwanafunzi kidato cha nne, Mr Fuso anajali elimu ya mtoto na maisha yake huko mbelen..angewatimua siku za nyuma , angemvuruga sana huyo mtoto upande wa elimu yake, ameamua kukaa kama mzazi....

Hii ni aina gani ya huruma? SIJUI kama mtume Petro alifundisha maana alituasa tuwe na KIASI. Angalia jamaa asiwe anatenda dhambi kwa huruma zake
 
kaka pango ni Sh 300,000 kwa mwezi, kwa mwaka ni Tsh 3,600,000 kwa miaka miwili ni 7.2m. ni hela nyingi sana wakuu.
Timua hao!

Haiwezekani mtu aje mjini kuteleza kwenye maganda ya ndizi!
 
Mkuu kama unasali ama kuswali basi Mwnyezi Mungu huja kwetu kwa namna mbali mbali ila ni wachache sana waliojaaliwa hekimu hutambua hili, yumkini Mwenyezi Mungu kaamua kutumia mpangaji wako huyu kukupima imani na ikiwa utashinda hili basi heri ya Bwana ii nawe... fuata ushauri wa ndugu Samson Ngomboli na utauona ukuu wa Bwana! Hii ni mitihani tu ya maisha na haidumu!
 
kaka wale wameajiliwa.....sasa sijui kuna nini kimetokea kwenye hii familia kwa kweli sijui kabisa....Binti anamaliza shule ndiyo nasubiri akimaliza tu niwashe moto maana huwa anani text kuniomba nisiwatimue wazazi wake na wadogo zake...yaani ni kama binti anajivika majukumu ya kifamilia akiwa bado mdogo....inatia huruma sana... ila wataondoka tu.
Kama amejivika majukumu ya familia nawe mvike majukumu ya ki mother mother. U balance.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom