Mpaka sasa kila mmoja amejionea umuhimu wa Bunge kuwa na wabunge wa upinzani

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Kwa huu Utopolo unaoendelea bila shaka Kila mtu amejionea kuwa kule bungeni ni muhimu kuwa na wabunge ambao sio kijani pekee.

Inshu ya Tozo kwamfano! Ni mpaka Wananchi wenyewe mtaani wanajisemea hakuna wa kuwasemea! Bungeni kule ni watu kupongeza tu.

Sasa hivi bei ya nafaka haikamatiki na hakuna mbunge anainua Sauti kusema!

Tukubali tukatae upinzani ni muhimu sana katika nchi yoyote Ili watu wasibweteke na kufanya mambo Kwa faida zao Binafsi.

My take
Mpaka kufika December kilo ya mchele itakuwa elf 4
Na CCM haitaona Tatizo!
 
Kuna nchi inaongozwa na Mapaka👇😁😁😁
MuiAd.jpeg
YAEbhVu.jpeg
AAOqup.jpeg
 
Mzee wa unyiramba anasema CCM imefanya maisha ya wananchi kuwa nafuu. Sheeenzi, sheenzi kabisa
 
Bila wapinzani Bungeni hakuna la maana kule hata siku moja!
Hawa wa ccm kila kitu ni ndiooooooooooooooooooo!
Hata mvuto wa kusoma taarifa za bunge hakuna!
ndio maana miswada ya ajabu kabisa inapita tu na nahisi pia huwa hawasomi !
 
Wabunge wa upinzani wa vyama gani?
Nimeuliza swali ungejibu swali kiufasaha ingekuwa na maana zaidi, Ila ulicho andika kina nipa mashaka juu ya uwezo wako wa akili.
Yaani nishasema kabisa "wabunge Wa UPINZANI" ila wewe unauliza Eti wapinzani wa Chama Gani!

Halafu Eti wewe ndio unahoji uwezo wangu wa akili..
dah
 
Tukubali tukatae upinzani ni muhimu sana katika nchi yoyote Ili watu wasibweteke na kufanya mambo Kwa faida zao Binafsi.
Naunga mkono hoja, ndio maana tumemuomba Mama
P
 
Hivi bado lipo? sikuwahi kuwaskia tena baada ya upinzani kuondolewa na yule mwovu!
Nina imani kama lipo halina la maana zaidi ya umbea tu!
 
Back
Top Bottom