moyo wangu unavuja damu

kutosamehe?mh sina hakika lakini kimsingi kusamehe ni ngumu sana kwa mwanadamu!kuna jamaa yangu mmoja hivi aliwahi kunimbia bwana wewe kusamehe sio kitu rahisi i see Mungu mwenyewe alikuwa anawapa maadhabu kibao wamisri !alisema kama utani lakini ilinipa tafakari sana kiukweli!

bottom line
kusamehe kama haitoki moyoni
sio lazima
 
Baba, umeshasahau scandal ya Marie Stopes hospital ya mwenge? Mjamzito alitaka kubakwa na mpiga ultra sound? Baada ya ile scandal rafiki yangu wa karibu sana alinisimulia kuwa na yeye aliwahi kupigwa ultra sound hapo na kulikuwa na 'excessive touching'. Zipo sana, huwa staki kuwaza wanachotufanya wakati wa operesheni aisee!
Nahisi kama umewadhalilisha Madaktari wetu kwa kiwango cha juu sana......
Hivi kweli madaktari wetu, hawa hawa ninaowajua, hivi kweli jamani........................!
 
operation jitahidi mwenza aingie.

Hospital zetu ziko too 'corrupted'

hata asipobaka mtoto unaweza pewa wa kichina.

Baba, umeshasahau scandal ya Marie Stopes hospital ya mwenge? Mjamzito alitaka kubakwa na mpiga ultra sound? Baada ya ile scandal rafiki yangu wa karibu sana alinisimulia kuwa na yeye aliwahi kupigwa ultra sound hapo na kulikuwa na 'excessive touching'. Zipo sana, huwa staki kuwaza wanachotufanya wakati wa operesheni aisee!
 
hii ni ishu nyingine asipopona.
Basi daktari atakuwa kala kwako na wewe umeliwa bure.

Sasa hiyo uitamke kabla ya kumvulia pichu daktari, sio saa ya kuachwa! Una guarantee hata hiyo operesheni atapona? Daktari ndio Mungu? Akhuuu!
 
Baba, umeshasahau scandal ya Marie Stopes hospital ya mwenge? Mjamzito alitaka kubakwa na mpiga ultra sound? Baada ya ile scandal rafiki yangu wa karibu sana alinisimulia kuwa na yeye aliwahi kupigwa ultra sound hapo na kulikuwa na 'excessive touching'. Zipo sana, huwa staki kuwaza wanachotufanya wakati wa operesheni aisee!
Hayo mambo ya ultra sound nilishampiga maroufouk mama yenu na kama ni matibabu nampeleka hospitai ya Wairan pale Mikocheni maana pale mwanamke anatibiwa na daktari mwanamke na mwanaume anatibiwa na daktari mwanaume.... Chezea Mtambuzi weye.. madaktari wa bongo watamsikia mama Ngina hapa hapa JF..... ujinga uwatoke
 
Hahhahaha! Unajua wivu wa hivi ni dalili ya uzee? Mie dr lazma kwanza awe handsome afu kijana, mzee mzee simtaki anatetemeka mikono. Lol!
Hayo mambo ya ultra sound nilishampiga maroufouk mama yenu na kama ni matibabu nampeleka hospitai ya Wairan pale Mikocheni maana pale mwanamke anatibiwa na daktari mwanamke na mwanaume anatibiwa na daktari mwanaume.... Chezea Mtambuzi weye.. madaktari wa bongo watamsikia mama Ngina hapa hapa JF..... ujinga uwatoke
 
haya tunayasema sasa kwa sababu hatuna tatizo na hatuko kwenye hamaki.

Nampatia picha huyo mwenye mume hana kitu na dokta anampa altimatamu, weeee.

Sisemi sana, lakini . . . .

Hiyo operesheni una uhakika atapona hadi ujiuze? Short cut is the longest route!
 
ni asubuhi njema tu,ghafla napokea simu kutoka kwenye namba nisiyoijua
mazungumzo yalikuwa kama yafuatayo
Mpiga simu!:nenda muhimbili kachukue mzoga wa mume wako
Mimi:mbona sikuelewi
Mpiga simu:nimekwambia nenda muhimbili ukachukue mwili wa mumeo
kisha akakata simu
nikawasha gari mpaka muhimbili nafika mapokezi naambiwa kama nimepewa maelezo hayo niende motuary
nafika motuary na haya ndo majibu niliyopewa
''kama ni mwanaume unayemzungumzia ni yule aliyefumaniwa na kupgwa na kuvunjwa mguu tumemuhamishia ICU manake hajafa bado"
bado sielewi linaloendelea mara najisikia nikiuliza ICU ndio wapi naelekezwa na kujikuta tu naenda huko nafika na kuonyeshwa kitanda alicholala kipenzi cha moyo wangu,baba wa watotto wangu,mwanaume niliyekabidhi maisha yangu ,nafsi na akili yangu yote akiwa amelala hajitambui.
nikajikuta namuuliza mume wangu hapa ndio mbeya kwenye semina,hizi bandeji ndio zawadi ulisema utaniletea sipati majibu maana hanisikii wala kutambua kama niko pale!
anakuja daktari na kuniambia bora umefika mama maana mgonjwa anatakiwa kupelekwa thieta sasa hvi vinginevyo tunampoteza!tunahitaji damu ya kumuongeza na pesa ili tufanye hiyo operation!
nikajishangaa kuwa nilitoka pale na kurudi nyumbani ili nichukue pesa mume wangu apone,kwenye droo tunaloweka pesa hakuna,kwenye mabegi yake pesa hakuna,nikona ngoja nichukue kadi za benki,nafika kwenye ATM pesa hakuna!nikijiona nachanganyikiwa!
narudi hospitali kumuomba daktari amtibu mume wangu kisha akipona atalipa hizo pesa ananiambia haiwezekani vinginevyo nimuache afe maana hakuna mjinsi
naanza kuwapigia simu ndugu na marafiki zake nao hawanipi msaada wowte
wifi yangu ananijibu nina sherehe ya mwanangu jumapili ijayo na nimealika rafiki zangu
kaka yake ananijibu ana safari ya kwenda ulaya mwezi ujao hivo pesa ni za safari
ukoo wangu ni mimi ndo nilikuwa nawasaidia toka nimeolewa hvo wala hakuna anayeweza kunisaidia
mimi mwenyewe sina akiba yoyote nilishazoea nikiomba tu pesa kwa mume wangu ninapewa na kwa saababu nilimini zipo kila siku sikuwa na akiba wala akaunti ya benki!
narudi kwa daktari huku nalia na ni siku ya pili hali ya mume wangu inazidi kuwa mbaya,
daktari anasema hana jinsi ya kunisaidia labda kama nitampa ushirikiano wa kutosha !simwelewi anamaanisha nini!ananisogelea na kunza kunifungua vifungo vya shati langu,nikiwa bado sielewi nini kinaendelea anafungua na sidiria yangu,kisha na kumalizia na vitenge nilivyojifunga,akili zikanikaa sawa hapo kuwa nini natakiwa kufanya,najikuta napanda kitandani na kuruhusu yule daktari afanye analokusudia,baada ya kumaliza anashuka na kuanza kuchukua vifaa vya operation kuelekea wodini kwa mume wangu,na anatoa maelekezo aandaliwe kwa ajii ya operation.nimekaa nje ya wodi na mume wangu anarudishwa baada ya saa 2 za operation.baada ya mwezi amepata nafuu na anrudishwa nyumbani,baada ya mwezi huo pia ninajihisi mjamzito!mume wangu hakuwepo nyumbani kama miezi mi2 hivi maana ni mtu wa kusafiri sana kutokana na mazingira ya kazi yake,hivyo ni wazi ujauzito huu sio wa mume wangu!mume wangu amelihisi hilo na amenihoji nimeshindwa la kujibu zaidi ya kulia.ameita kikao cha familia akinishutumu kuwa mimi ni malaya na hanitaki tena !nirudi kwetu!

well it is a story nimeibadilisha kidogo kutoka kwenye wimbo wa BAHATI BUKUKU,lakini wadau
1.tushuriane hapa iwapo mume au mke anajikuta kwenye mazingira haya !anafanyaje!
2.umejifunza kitu gani hapa!

Afadhali umesema umedesa!

Huo wimbo nimeusikia, ila ni story ya kusikitisha,

Lakini mimi nauona unajenga taswira mbaya kwa madaktari kana kwamba wao hawana utu, wanachojali ni kitu kidogo na pengine hata rushwa ya ngono

Na kitu cha kushangaza taswira nyingine ninayoipata ni kuwa madaktari ni mahodari wa kuhimiza matumizi ya kondomu wakati wao hawatumii, kama katia mtu mimba is more likely kuambukiza au kuambukizwa UKIMWI.
 
apart from alichosema The Boss, another lesson I get from here ni kwamba,desperate moments call for desperate measures...
 
haya tunayasema sasa kwa sababu hatuna tatizo na hatuko kwenye hamaki.

Nampatia picha huyo mwenye mume hana kitu na dokta anampa altimatamu, weeee.

Sisemi sana, lakini . . . .

Mie nimeshajijengea attitude ya emergency preparedness and response plan yangu. So ikitokea at least dhamira yangu itaniambia 'you are better than tjis king'asti. This too shall pass, think like you always do baby, THINKI!!!!!'. Hapo hapo akili ya bhange itastuka. Usijiandae kufeli aisee, ni dhambi kwanza. Mwili wako hauwezi kuwa dirisha la kukimbia jaribu.
Ngoja kwanza naskiliza kinyau nyau kikia cha pweza.
 
ila kweli, ujue mwili ndio hekalu pekee unaloweza miliki mwenyewe?

Mie namwonea huruma tu.

Mie nimeshajijengea attitude ya emergency preparedness and response plan yangu. So ikitokea at least dhamira yangu itaniambia 'you are better than tjis king'asti. This too shall pass, think like you always do baby, THINKI!!!!!'. Hapo hapo akili ya bhange itastuka. Usijiandae kufeli aisee, ni dhambi kwanza. Mwili wako hauwezi kuwa dirisha la kukimbia jaribu.
Ngoja kwanza naskiliza kinyau nyau kikia cha pweza.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom