The Boss wakati mwingine wanaume huwa wanawanyima wake zao kufanya kazi
Mie nna mfano hai....nnae rafiki kipenzi kabla hajaolewa alikuwa anafanya kazi.....baada ya kuolewa mume kamkataza kufanya kazi.....huezi amini huyu dada aliolewa toka mkoa mwingine akaletwa mkoa niliopo.....hajui hata sokoni panafananaje manake mume anamletea kila kitu.....akitaka kwenda popote mume anamchukua kwa gari......hajui hata maduka gani yapo upande gani.....yaani yupo yupo tu......amejaribu kulalamika kwa ndugu jamaa na marafiki ila mume ameweka msimamo kuwa sitaki mke wangu afanye kazi manake mie kipato changu kinatosheleza familia! Kabla hajamuoa alimwahidi kuwa atamfungulia mradi baada ya ndoa, ila nao umekuwa historia......aliolewa mwaka juzi mwezi wa 4.....mpaka dakika hii wala hakuna dalili ya mradi......mume hamnyimi chochote ila sasa ndiyo yaleeee siku yakimkumba ya kumkumba wala hatajua aanzie wapi! Hii mbaya sana asee!