moyo wangu unavuja damu

utafute mamito ni mzuri sana,si unajua bahati na ile saut yake sasa ndo ukute anashusha hiyo mistari kwa kweli it is too touching!lakini inaweza pia kuwa imeshamtokea mtu au yeye mwenyewe au rafiki yake ,kiukweli nimejaribu kuvaa viatu vya huyo mwanamke vimenibana jamani!

Alipokuwa anahojiwa aliulizwa je ni kisa cha kweli ? Akasema ni cha kweli ila hakijatokea kwangu.....kimemtokea rafiki angu so snowhite hivi vitu vipo ila ndio kama hivyo ukijaribu kuvifikiria sana unahisi kuchanganyikiwa.....yaani viatu lazima vikubane lol

Ujue kama ni mwanamke mwingine pia asingejihangaisha , angeweza kumwacha huyo mume afilie mbali .....watu tuna mioyo tofauti sana!
 
Last edited by a moderator:
oh pole ukaanza kunionea huruma!lakini hata kama sio mimi kuna watu wanakutwa na haya mambo rafki yangu!thanks for caring mkuu!
yeah! nilianza kukuonea huruma huku nusu ya nafsi yangu ikikupongeza kwa upendo na kumjali mumeo. Ni kweli haya mambo yanatokea au hata kama siyo jambo hilo exactly basi linalofanana na hilo. Mungu ni mwema tumuombe tu awape mawazo sahihi wale wote wanaokutwa na matatizo ya aina hiyo wapate utatuzi mzuri ambao baadae hautaleta mfarakano ktk ndoa/familia zao maana muda mwingine watu hufanya yale wasiyopanga kufanya ili kuleta matokeo chanya kutokana na kuzidiwa na matatizo na kukosa ufumbuzi wa haraka.
 
Yaani mimi muislam lakini hizi nyimbo za kikiristo zinanigusaga sana! Yaani kama huyu bahati nina album zake zote!

Safi sana mama D .....tunachoangalia ni ujumbe uliopo.......haijalishi kama wewe ni mkristo au la!
 
Last edited by a moderator:
wala usiumize kichwa.....cheza karibu na redio safina utaupata.....nimeupenda sana huu wimbo......
Dada yangu kwetu porini hii Redio safina inapatikana wapi? na hii single ni audio tu hakuna Video yake maana nina maswali mengi kwa BAHATI BUKUKU
 
nimejifunza mwanamke hutakiwi kuwa golikipa
yaani hata shilingi ya soda umtegemee mumeo?
yaah hili pia ni funzo,manake hapo kama mtu una akiba fulani si unasolve tu hii habari ,lakini kuna watu hawataki wake zao wafanye kazi i see kisa wana uwezo wa kuwaprovide kila kitu!mke hafanyi biashara/kazi wala hasomi yupo tu kisa mume ana uwezo na kila kitu anchotka ni fridge open!basi ndoa mambo ya kumegwa bila mpangilio yanapokufika ndo kama hv!mi niliwaza katika uhalisia viatu vilinibana mkuu!nimehisi kama ningebaki na mihasira yangu hata kama ningekuwa na hela,ah!ngumu sana i see!
 
Ah unafkiri wanaume wanaelewa hilo? Hata kama umenusuru maisha yake basi ataona wema uliotenda ni ubaya..tenda wema wende zako

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
 
nimejifunza mwanamke hutakiwi kuwa golikipa
yaani hata shilingi ya soda umtegemee mumeo?
The Boss wakati mwingine wanaume huwa wanawanyima wake zao kufanya kazi

Mie nna mfano hai....nnae rafiki kipenzi kabla hajaolewa alikuwa anafanya kazi.....baada ya kuolewa mume kamkataza kufanya kazi.....huezi amini huyu dada aliolewa toka mkoa mwingine akaletwa mkoa niliopo.....hajui hata sokoni panafananaje manake mume anamletea kila kitu.....akitaka kwenda popote mume anamchukua kwa gari......hajui hata maduka gani yapo upande gani.....yaani yupo yupo tu......amejaribu kulalamika kwa ndugu jamaa na marafiki ila mume ameweka msimamo kuwa sitaki mke wangu afanye kazi manake mie kipato changu kinatosheleza familia! Kabla hajamuoa alimwahidi kuwa atamfungulia mradi baada ya ndoa, ila nao umekuwa historia......aliolewa mwaka juzi mwezi wa 4.....mpaka dakika hii wala hakuna dalili ya mradi......mume hamnyimi chochote ila sasa ndiyo yaleeee siku yakimkumba ya kumkumba wala hatajua aanzie wapi! Hii mbaya sana asee!
 
Last edited by a moderator:
Dada yangu kwetu porini hii Redio safina inapatikana wapi? na hii single ni audio tu hakuna Video yake maana nina maswali mengi kwa BAHATI BUKUKU
sidhani kama video ameshatoa,nafikiri ni audio tu mpka sasa hivi!
 
The Boss wakati mwingine wanaume huwa wanawanyima wake zao kufanya kazi

Mie nna mfano hai....nnae rafiki kipenzi kabla hajaolewa alikuwa anafanya kazi.....baada ya kuolewa mume kamkataza kufanya kazi.....huezi amini huyu dada aliolewa toka mkoa mwingine akaletwa mkoa niliopo.....hajui hata sokoni panafananaje manake mume anamletea kila kitu.....akitaka kwenda popote mume anamchukua kwa gari......hajui hata maduka gani yapo upande gani.....yaani yupo yupo tu......amejaribu kulalamika kwa ndugu jamaa na marafiki ila mume ameweka msimamo kuwa sitaki mke wangu afanye kazi manake mie kipato changu kinatosheleza familia! Kabla hajamuoa alimwahidi kuwa atamfungulia mradi baada ya ndoa, ila nao umekuwa historia......aliolewa mwaka juzi mwezi wa 4.....mpaka dakika hii wala hakuna dalili ya mradi......mume hamnyimi chochote ila sasa ndiyo yaleeee siku yakimkumba ya kumkumba wala hatajua aanzie wapi! Hii mbaya sana asee!
hili lakumpa mke kila kitu so asijishighulishe kwa kweli ni mbya,na inatengeneza kunyanyasika sana kwa mwanamke!
 
Ah unafkiri wanaume wanaelewa hilo? Hata kama umenusuru maisha yake basi ataona wema uliotenda ni ubaya..tenda wema wende zako

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums

kha!hata katika hili na ukweli anaujua!
 
hili lakumpa mke kila kitu so asijishighulishe kwa kweli ni mbya,na inatengeneza kunyanyasika sana kwa mwanamke!

Mnoo mpendwa.....unabaki kunyenyekea mume kila siku vile tu unahisi usipofanya hivyo anaweza kukuacha na wewe umemfanya ndio kila kitu kwako.....yaani huyu rafiki huwa analalamika sana lakini mumewe wala hamsikilizi!
 
kabla sijamaliza nikasema snowhite amepatwa na nini tena..

ana nyimbo nzuri Bahati ila huu sijapata kuusikia. naomba unitajie title ya wimbo.
 
Mnoo mpendwa.....unabaki kunyenyekea mume kila siku vile tu unahisi usipofanya hivyo anaweza kukuacha na wewe umemfanya ndio kila kitu kwako.....yaani huyu rafiki huwa analalamika sana lakini mumewe wala hamsikilizi!
wakati mwingine hata akikosea unashindwa kureact kisa utamudu vipi maisha,na yeye anakuwa na kiburi since anajua huwezi kufanya lolote!mimi kwa kweli tupendane tu lakini maswala ya kuachishana kazi au biashara eti unapesa nikae nikulelee watoto hata siyataki,yani hata kununua kijiblouse kwa muda niutakao pia ni shida,mume wangu anihudumie sawa but nataka kuwana pesa yangu kutokana na jasho langu mwenyewe!ndo humu kunakuwaga na maswali "ile niliyokupa jana imeisha"ah
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom