moyo wangu unavuja damu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

moyo wangu unavuja damu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by snowhite, Sep 16, 2012.

 1. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ni asubuhi njema tu,ghafla napokea simu kutoka kwenye namba nisiyoijua
  mazungumzo yalikuwa kama yafuatayo
  Mpiga simu!:nenda muhimbili kachukue mzoga wa mume wako
  Mimi:mbona sikuelewi
  Mpiga simu:nimekwambia nenda muhimbili ukachukue mwili wa mumeo
  kisha akakata simu
  nikawasha gari mpaka muhimbili nafika mapokezi naambiwa kama nimepewa maelezo hayo niende motuary
  nafika motuary na haya ndo majibu niliyopewa
  ''kama ni mwanaume unayemzungumzia ni yule aliyefumaniwa na kupgwa na kuvunjwa mguu tumemuhamishia ICU manake hajafa bado"
  bado sielewi linaloendelea mara najisikia nikiuliza ICU ndio wapi naelekezwa na kujikuta tu naenda huko nafika na kuonyeshwa kitanda alicholala kipenzi cha moyo wangu,baba wa watotto wangu,mwanaume niliyekabidhi maisha yangu ,nafsi na akili yangu yote akiwa amelala hajitambui.
  nikajikuta namuuliza mume wangu hapa ndio mbeya kwenye semina,hizi bandeji ndio zawadi ulisema utaniletea sipati majibu maana hanisikii wala kutambua kama niko pale!
  anakuja daktari na kuniambia bora umefika mama maana mgonjwa anatakiwa kupelekwa thieta sasa hvi vinginevyo tunampoteza!tunahitaji damu ya kumuongeza na pesa ili tufanye hiyo operation!
  nikajishangaa kuwa nilitoka pale na kurudi nyumbani ili nichukue pesa mume wangu apone,kwenye droo tunaloweka pesa hakuna,kwenye mabegi yake pesa hakuna,nikona ngoja nichukue kadi za benki,nafika kwenye ATM pesa hakuna!nikijiona nachanganyikiwa!
  narudi hospitali kumuomba daktari amtibu mume wangu kisha akipona atalipa hizo pesa ananiambia haiwezekani vinginevyo nimuache afe maana hakuna mjinsi
  naanza kuwapigia simu ndugu na marafiki zake nao hawanipi msaada wowte
  wifi yangu ananijibu nina sherehe ya mwanangu jumapili ijayo na nimealika rafiki zangu
  kaka yake ananijibu ana safari ya kwenda ulaya mwezi ujao hivo pesa ni za safari
  ukoo wangu ni mimi ndo nilikuwa nawasaidia toka nimeolewa hvo wala hakuna anayeweza kunisaidia
  mimi mwenyewe sina akiba yoyote nilishazoea nikiomba tu pesa kwa mume wangu ninapewa na kwa saababu nilimini zipo kila siku sikuwa na akiba wala akaunti ya benki!
  narudi kwa daktari huku nalia na ni siku ya pili hali ya mume wangu inazidi kuwa mbaya,
  daktari anasema hana jinsi ya kunisaidia labda kama nitampa ushirikiano wa kutosha !simwelewi anamaanisha nini!ananisogelea na kunza kunifungua vifungo vya shati langu,nikiwa bado sielewi nini kinaendelea anafungua na sidiria yangu,kisha na kumalizia na vitenge nilivyojifunga,akili zikanikaa sawa hapo kuwa nini natakiwa kufanya,najikuta napanda kitandani na kuruhusu yule daktari afanye analokusudia,baada ya kumaliza anashuka na kuanza kuchukua vifaa vya operation kuelekea wodini kwa mume wangu,na anatoa maelekezo aandaliwe kwa ajii ya operation.nimekaa nje ya wodi na mume wangu anarudishwa baada ya saa 2 za operation.baada ya mwezi amepata nafuu na anrudishwa nyumbani,baada ya mwezi huo pia ninajihisi mjamzito!mume wangu hakuwepo nyumbani kama miezi mi2 hivi maana ni mtu wa kusafiri sana kutokana na mazingira ya kazi yake,hivyo ni wazi ujauzito huu sio wa mume wangu!mume wangu amelihisi hilo na amenihoji nimeshindwa la kujibu zaidi ya kulia.ameita kikao cha familia akinishutumu kuwa mimi ni malaya na hanitaki tena !nirudi kwetu!  well it is a story nimeibadilisha kidogo kutoka kwenye wimbo wa BAHATI BUKUKU,lakini wadau
  1.tushuriane hapa iwapo mume au mke anajikuta kwenye mazingira haya !anafanyaje!
  2.umejifunza kitu gani hapa!
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,216
  Trophy Points: 280
  Huu wimbo mzuri mno
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Haaaaaa naupenda sana huo wimbo,ebu attach mp3 yake tuishushe hapa!
   
 4. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  yani mi sikuwahi kusikia nilipousikia leo mchana,nimejikuta nalia kwa kweli!
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mzuri sana na unafundisha mnoo!


  Ila kama ni mimi huyo mdada itabidi nimwambie mume ukweli wote na nini kilisababisha nikajikuta naanguka dhambini ......asingemaliza hela zote yote hayo yasingetokea manake angeweza kupata matibabu bila tatizo.....wakati mwingine sio vizuri kuanza kumhukumu mtu kabla hujajua chanzo cha tatizo!......mama alifanya kumwokoa mumewe.....mume halijui hilo na tayari keshamuita malaya......hajui kuwa yeye ndio chanzo!
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mie pia bado kuusikia......ila niliwahi kumsikia Bahati akihojiwa kuhusu wimbo wake.....ntautafuta niusikilize.....mie wakati nasoma hapa nikajua yamemkuta labda rafiki.....sio siri wakati naendelea kusoma moyo nao unazidi kujaa huzuni.....kidogo na mimi nilie ila nilivyofika mwisho ndio nkasema Aaaah!
   
 7. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  huyo mume hata baada ya kujua mkewe amefanya hilo kwa ajili yake bado aliendelea kumtuhumu lakini mwisho alimsamehe na maisha yakaendelea!ila ni wimbo una mafunzo mengi sana kuhusu suala la msamaha!
   
 8. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  utafute mamito ni mzuri sana,si unajua bahati na ile saut yake sasa ndo ukute anashusha hiyo mistari kwa kweli it is too touching!lakini inaweza pia kuwa imeshamtokea mtu au yeye mwenyewe au rafiki yake ,kiukweli nimejaribu kuvaa viatu vya huyo mwanamke vimenibana jamani!
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Tulizanaaaaaaaa!!
   
 10. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  sina mp3 yake ,BAK anaweza kuwa nayo!
   
 11. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  kimya tu!
   
 12. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ... Inafaa kutengenezea movie! itakuwa na mvuto sana!
   
 13. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  yaah sijui kama BAHATI BUKUKU analijua hili,yani itauza sana!
   
 14. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  wala usiumize kichwa.....cheza karibu na redio safina utaupata.....nimeupenda sana huu wimbo......
   
 15. m

  mossad Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Daaaah!! snowhite yaani nilikuwa nasoma kwa makini mno huu ujumbe wako, nilihisi Daktari kakula mzigo kumbe ni nukuu za wimbo. Ila kama Dk kala mzigo poa tu umeokoa uhai wa mumeo na inabidi umwambie mumeo hata akikuacha haina noma Mungu atakulipa kwa wema wako wa kuokoa uhai wake na pia atakuhukumu kwa usaliti ulioufanya kwa mumeo.
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  siujui kabisa.
   
 17. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  oh pole ukaanza kunionea huruma!lakini hata kama sio mimi kuna watu wanakutwa na haya mambo rafki yangu!thanks for caring mkuu!
   
 18. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  vipi hiyo story haijakufanya uutufute?utafute mkuu.pengine ukiusikilzza mwenyewe utajifunza kitu cha tofauti kuhusu haya maisha na tafsiri yake,maana dah!
   
 19. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Thanks dear.......ntafuata maagizo yako!
   
 20. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Yaani mimi muislam lakini hizi nyimbo za kikiristo zinanigusaga sana! Yaani kama huyu bahati nina album zake zote!
   
Loading...