Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
kesho (jumapili) kama kuna mtu anataka kupiga simu na kuunguruma kuhusu suala hili (pande zote zinakaribishwa) nitawapatia namba ya studio...!
Kulikoni,
Your arguments are usually quite good but this weekend you are not your normal self. The Minister's answer that we will cross that bridge when we get to it is a very bad one. Governments have to have answers to various possible scenarios. For example, the PM should have an answer now to the following hypothetical question: What will we do if it does not rain for the next two years? We should not wait until we get two years without rain before we figure out how to handle an extended drought.
Kulikoni, do not defend Kayombo at any cost. He is making bad mistakes. Let him wallow in the mud by himself; you need not join him there.
Augustine Moshi
Nakusikia Nyani... ndio maana tunafanya mpango wa kuweza kusikika kwenye radio za ardhini huko kijijini..!
Mzee Mwanakijiji,
Umewafafanulia vizuri sana wabunge namna walivyopashwa kumjibu Gaudence Kayombo. Kayombo alidanganya (labda bila kujua) aliposema separation of powers hairuhusu wabunge kuridhia mikataba ya kiserikali kabla haijawa sheria. Ni wazi kabisa toka kwenye ibara za katiba ulizotaja (IBARA 63(2) (E)) kwamba Wabunge wana haki na uwezo wa kuhakiki mikataba kati ya Jamhuri ya Muungano na mtu yeyote.
Inabidi wabunge wawe wanaifahamu vizuri Katiba. Wanaapaje kuilinda kama hata hawaifahamu? Kama wangekuwa wanaifahamu, wangejibu huo uongo wa Gaudence Kayombo hapo hapo, kwa njia ya swali la ziada.
Gaudence Kayombo amejichanganya aliposema wabunge wana uwezo wa kusimamia serikali inavyotekeleza mikataba, na huku anasema hawana uwezo wa kudai kuiona mikataba yenyewe. Kuna level mbili za kuona mkataba. Kuna kuuona kabla haujasainiwa na kuwa wa kisheria, na kuna kuuona wakati umeshasainiwa. Inaelekea kwa sasa wabunge wananyimwa kuona mikataba hata baada ya kusainiwa. Watasimamiaje utekelezaji wake?
Wabunge watumie Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulazimisha serikali isisaini mkataba wowote bila ridhaa ya Bunge.
Wanaong'ang'ania mikataba iwe siri na isiridhiwe na wabunge wana lao!
Augustine Moshi
Mzee Mwanakijiji:
Ingekuwa wachangiaji wetu wote hapa wanachangia objectively kama wewe, wakubwa wetu wengi wangekuwa wanakuja hapa na kujifunza maoni hasa ya wananchi, they're not necessarily correct lakini at least ni views zinazoweza kusikilizwa na wasomi, this is good and I encourage you and others to embrace this line of argument....wakubwa wengi for information tu wapo aware na JF ila honestly sina tena nguvu ya kuwahimiza wapite hapa kwani siku hizi 'upupu' ni mwingi wengi wao wakiingia siku mbili tatu wanalose interest kwa vile hamna hoja.... hivyo ni wito kuwa kama mnataka sauti zenu zisikike basi toeni kwa hoja na uchambuzi yakinifu sio kubwabwaja tu nk...
On the issue:
Separation of powers ni pana zaidi ya alivyoeleza sahihi kabisa mheshimiwa Kayombo, yaani yes ni kweli kama alivyosema mwanakijiji kuwa ipo haki kwa wabunge kujadili mikataba ya serikali ambayo jina la serikali limehusika, sasa wabunge wana haki ya kujadili na kuelezea mapungufu [if any] ya mikataba nk lakini sio kama anavyosema Mzee Moshi kuwa ''kuhakiki'' hii ni kazi ya watendaji wa serikali...
Bunge lilikuwa na haki ya kujadili mkataba wa Richmond in the context of:
- Validity [ ni sababu zipi zilizopelekea mikataba husika ikaingiwa]
-Execution [ umetekelezwa kivipi]
- Deficiencies [kasoro zozote zilizojitokeza nk]
Kama mbunge ana hoja ya msingi katika hayo anaweza kuuliza in terms of swali binafsi na ikiwa wabunge woooote wataridhika basi wanaweza kwa pamoja kutoa kauli iundwe tume huru ya kuchunguza 'kadhia' [ mind the language] ili ukweli ujulikane.... tume ikitoa kauli yake basi hapo inakuwa ndio the beginning of the end for the matter yaani aidha wanaohusika kama wamezembea wataondolewa au kuwa exonerated...
Lakini Bunge kama haliwezi ku-overlap majukumu ya serikali [executive] kwa kuuandika mkataba, kutathmini utekelezaji wake wa day to day nk sasa hoja kuwa mikataba ipitiwe ''kabla'' ni hoja mfu kwa vile there is no legal mandate for the parliament to do that....
Imagine everyday serikali inaingia mikataba mingi sana ya kiutendaji, inatoa tenders, kandarasi na inapokea misaada mingi tu ya kifedha ambayo inainvolve some form of mikataba, kwa hiyo kama mikataba yote hii inabidi ipitiwe na bunge...it will be detrimental to gov't activities....
Ni pale tu ambapo kama bunge lina wasi wasi wa Rushwa ndio linaweza kuipitia au kuhoji uhalali wake.... kama richmond mnahisi ina walakini mwambieni Zitto....
sasa tofauti iko wapi baina ya mikataba iliosainiwa na bw. Kerl Peter na mfalme mSoveru tuliosoma kwenye historia? kumbe bado tuko enzi zile zile!!!!!!!!!!!!
Naona kuna haja ya kufundisha elimu ya uraia maana kama wabunge hawajui kuwa wao ni sehemu ya serikali basi tuna matatizo!!