Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Asante Mungu kwa kutupa Magufuli na kutuonesha maneno ya Mwl Nyerere kwamba Kwa Katiba hii Rais anaweza kuwa Dikteta Mh Jaji Werema amesema kwa utawala wa MAGUFULI tumejua ubovu wa Katiba yetu zaidi ccm walifinywa na wanajua MAGUFULI alivyokuwa akiwananga mpaka wabunge wanaambiwa kazi yao kupiga makofi tuu mwanamume anawatafutia pesa hawana nguvu ya KUZIHOJI MATUMIZI YAKE
Mwl Nyerere alisema tukipata Rais Kichaa......
 
Asante Mungu kwa kutupa Magufuli na kutuonesha maneno ya Mwl Nyerere kwamba Kwa Katiba hii Rais anaweza kuwa Dikteta Mh Jaji Werema amesema kwa utawala wa MAGUFULI tumejua ubovu wa Katiba yetu zaidi ccm walifinywa na wanajua MAGUFULI alivyokuwa akiwananga mpaka wabunge wanaambiwa kazi yao kupiga makofi tuu mwanamume anawatafutia pesa hawana nguvu ya KUZIHOJI MATUMIZI YAKE

We mpumbavu sana. Ndo uhuru huo wa kuongea. By the way, Mwinyi Hassan na Mkwere na Msuya wako ziarani wanapiga mpunga kwenye miradi yetu pendwa.
 
Asante Mungu kwa kutupa Magufuli na kutuonesha maneno ya Mwl Nyerere kwamba Kwa Katiba hii Rais anaweza kuwa Dikteta Mh Jaji Werema amesema kwa utawala wa MAGUFULI tumejua ubovu wa Katiba yetu zaidi ccm walifinywa na wanajua MAGUFULI alivyokuwa akiwananga mpaka wabunge wanaambiwa kazi yao kupiga makofi tuu mwanamume anawatafutia pesa hawana nguvu ya KUZIHOJI MATUMIZI YAKE
Ni vema sasa tumjengee sanamu
JamiiForums-620675953.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
D4D553FD-6AF9-444B-8130-CA495D373F66.jpeg

Asante Mungu kwa kutupa Magufuli na kutuonesha maneno ya Mwl Nyerere kwamba Kwa Katiba hii Rais anaweza kuwa Dikteta Mh Jaji Werema amesema kwa utawala wa MAGUFULI tumejua ubovu wa Katiba yetu zaidi ccm walifinywa na wanajua MAGUFULI alivyokuwa akiwananga mpaka wabunge wanaambiwa kazi yao kupiga makofi tuu mwanamume anawatafutia pesa hawana nguvu ya KUZIHOJI MATUMIZI YAKE
 
Nina hoja mbili kwa kuanzia:
1) Sisi sote ni waathirika wa mfumo mbaya wa siasa zetu. Sasa basi tusiwaambie wapinzani tu wadai katiba. Ni jukumu letu sote. Nchi zote zilizofanikiwa kupata katiba nzuri za nchi zao haikudaiwa na wapinzani pekee. Mfano wa karibu kabisa ni wenzetu wa Kenya. Walioongoza na wanaoendelea kudai mabadiliko ya katiba Kenya ni Viongozi wa dini, Civil Society Orgnisations, Vijana, Vyuo Vikuu halafu ndo wanakuja vyama vya siasa. Tatizo letu ni pale tunapofikiri kuwa tatizo fulani si tatizo mpaka pale litakaponiathiri mimi. Lazima tubadilike. Kwa kawaida wanasiasa wa kiafrika hawaoni mbali zaidi ya madaraka. Tukiwaachia wapinzani kudai katiba peke yao hawatadai zaidi ya tume huru ya uchaguzi. Naamini tatizo la katiba ni kubwa kuliko tume huru ya uchaguzi. Vyama vya upinzani na wadu tu katika mchakato wa maendeleo ikiwemo siasa na katiba. Sote tunawajibika.

1) hakuna kipya ambacho hakijulikani tunachokitaka katika katiba. Tuongelee kuinishikiza serikali kupeleka mswada bungeni wa ku-adopt mapendekezo yaliyokwishatolewa huko nyuma. Tuna mapendekezo kutoka tume ya Nyalali, Shivji na Jaji Kisanga. Ripoti zote hizi zilianisha kwa kina matatizo ya katiba yetu na mapendekezo ya kufanyika. Huwezi kuniambia leo Mrema atakuja na mapendekezo tofauti na yale yaliyopo kwenye hizo tume zilizoongozwa na watu wenye vichwa vyao.

Narudia tena, matatizo ya kisiasa ikiwemo katiba katika nchi yetu hayawezi kuwa ya wapinzani peke yao. Ni ya kwetu wote nasi sote tunawajibika kuyatatua. Kuwataka kina JJ peke yao walete hoja ni kukwepa wajibu. Sam tupe maoni yako pia.
Haya msikilize huyu Kitila Mkumbo anayoyaongea siku hizi. Watu wakipata madaraka wanabadilika
 
Wanabodi ninakerwa na jambo hili naomba tujadili. Hivi serikali ni nani? Nilidhani ni wananchi ambao wanawakilishwa na Bunge?

Kutokana na majadiliano yanayoendelea bungeni kuhusu mikataba ambayo serikali haitaki ijadiliwe sisi kama wananchi ambao tumewachagua wabunge hawa tunapenda kuonyesha msimamo wetu kwa kufanya maandamano ya amani na mkutano mkubwa kutoa msimamo wetu. Mikataba yote ipelekwe bungeni. Sisi wananchi ndio tunasema.

Tanzania kweli ni nchi ajabu sana duniani. Ni kama nchi isio na watu wenye uchungu nchi yao. Jamani mawaziri mnasafiri sana nchi za watu na kuona maendeleo yao. Hivi kweli mna vision kuwa kuna siku Tanzania itaendelea? Ni lazima mfike mahali pa kuona wivu wa maendelo ya nchi siyo yenu binafsi tu. Tafadhali mheshimiwa Mbowe tunaomba uandae mkutano huo na kutoa tamko. Aliye karibu na mheshimiwa tafadhali mpelekee salamu. Msisubiri mpaka wakati wa uchaguzi tu.

" KWA MTAJI HUU NDOTO YA KUWALETEA WATANZANIA WOTE MAISHA BORA NA MEMA HAIWEZEKANI KABISA - IT IS NOT POSSIBLE FULLSTOP"

Sauti za wabunge hawa zisipuuzwe

KAMA kweli wabunge ndio wawakilishi wa wananchi, serikali sasa itaondoa pamba masikioni, itawasikiliza na kutekeleza wanachopendekeza.

Kwa siku nyingi sasa, kilio cha wabunge kuhusu mikataba ya madini na mikataba mingine mikubwa, kimezidi kiwango.

Kilio chao kimevuka mipaka ya kawaida. Kimewagusa hata wale ambao hawakuwa na shauku ya kukisikia.

Wabunge wanataka mikataba ipitiwe. Wanataka kujua kilichomo kwenye mikataba hiyo. Serikali haiwakilishi wananchi. Bunge ndicho chombo cha wananchi.

Wabunge wanapojadili jambo lenye manufaa kwa nchi, wanafanya hivyo kwa niaba ya wananchi wao.

Haiwezekani wabunge wapige kelele za kutaka kupitiwa mikataba, lakini serikali iendelee kuwa jeuri.

Awamu ya Tatu ya uongozi wa taifa hili ilitamba kwa kaulimbiu hewa ya uwazi na ukweli. Hapakuwa na uwazi wala ukweli.

Mikataba ilisainiwa. Wageni wakamilikishwa mali za taifa. Mikataba mingi ya kipuuzi kabisa ikasainiwa. Mzigo wa mikataba hiyo sasa unabebwa na walipa kodi wa nchi hii.

Serikali haikuwa wazi. Ilipuuza maoni ya wananchi, na hata ikafikia hatua ya kuwatisha wabunge waliosimama kidete kuhoji uoza fulani fulani.

Inasikitisha, na kwa kweli inakasirisha, kumsikia leo Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, akiunga mkono kupitiwa upya kwa mikataba ya madini!

Yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kuponda wote waliohoji mikataba hiyo, hata akafikia hatua ya kuwaita waliohoji kuwa ni wavivu wa kufikiri.

Waandishi wa habari walioandika au kuhoji mikataba hiyo, walionekana si wazalendo, na ni watu wasiokuwa na maarifa yoyote.

Serikali ya Awamu ya Tatu ilijaa ujuaji na ubabe. Net Group Solution walipingwa mno. Watanzania wengi walisimama kuipinga kampuni hiyo na hata wakurugenzi wake ambao wengi walikuwa vihiyo.

Lakini kilichofanywa na serikali ni kuwaita FFU wenye bunduki na gesi za kutoa machozi, kuwasindikiza Wazungu hao hadi ofisini.

Kimsingi yamefanyika mambo mengi ya ajabu katika nchi hii. Ndiyo maana tunasema kilio hiki cha wabunge sasa, lazima serikali ikifanyie kazi.

Miktaba ya kipuuzi, kwa mfano ya kuukodisha Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwa dola 1,000 kwa mwaka, ni laana isiyosameheka mbele ya Mola.

Hivi kweli Tanzania kwa utajiri wake ina sababu ya kuomba misaada mingi kama ilivyo sasa? Je, kwa ukwasi uliopo, kuna sababu ya watu kufa kwa magonjwa kama malaria?

Laana ya Tanzania ni nini? Je, si kweli kwamba laana ya Tanzania ni viongozi jeuri na wasioambilika? Kama kweli sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, basi sauti hii ya wabunge lazima iheshimiwe. Serikali ipeleke mikataba bungeni.

Katiba yenyewe hii hapa:

KATIBA YA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA na mabadiliko ya 2005

Angalia attachments hizi mbili (English and Swahili)​
Wewe siyo "Watanzania" wewe ni Mtanzania mmoja tu. Anza na Mbunge wako apeleke hoja Bungeni kama akiona ina mantiki.
 
Back
Top Bottom