Moto wawaka jengo la PPF Tower - Dar

Moto wawaka jengo la PPF Tower - Dar

Status
Not open for further replies.
Jengo la ppf lawaka moto ni saa la pili sasa tangu moto uanze....dar-es-salaam...
 
Hasikia faya wanachota mchanga pale feri kwa ajili ya kuja kuuzima moto
 
Iliungua WTC unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au kule hakuna umeme

Hapo kwenye red hapo kuna tatizo. Enzi ya utawala wa Mzee Mkapa ikulu paliwaka moto!
 
Kikosi cha zimamoto kilisema hakina hela kikaanzisha utaratibu wa kila gari kulipia elfu 20 kama kibali cha fire extuingisher.tena mzigo unapitia TRA automatically sasa hzo hela wanapeleka wp wanashindwa kununua vifaa?au mradi wa mtu kujipatia hela?tujiulize sie janga la moto lishakua lakitaifa
 
Hii ni changamoto kwa FIRE kuwa na vifaa vya kisasa zaidi kuweza kuzima hata maghorofa kuanzia 20 kwenda juu!!!.

Inasikitisha sana maana hapo jengo lilipo kama moto ukisambaa basi itakuwa kitisho.
 
Iliungua WTC unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au kule hakuna umeme

kuongozi ikulu imeshawahi kuunguua kipindi cha mkapa
 
duuuh isije kuwa watu walipiga deal lao sa wamehisi linataka kuingiliwa wameamua unguzu documents makusudi kwa style hiyo


,.....jst conspiracy
 
Ukienda ujerumani miji yao mingi haina maghorofa marefu ukiuliza wanakwambia ni kwa sababu ya kukabiliana kwa urahisi na majanga ya moto kama haya.
Viongozi wetu hapa Bongo sijui bado wana fikra za kikoloni za kujenga ofisi zote katikati ya mji, wakoloni walitumia mbinu hii ili waweze kutuchunga kama mbuzi waliokusanywa zizini. Leo hii kuna ulazima gani wa kujenga majengo marefu ambayo hatuwezi kumudu pale ambapo moto na majanga mengine yakitokea? majengo mengine hata maegesho ya magari ni vigumu kupata?majengo mengine hata mahali kwa kupeleka maji taka ni tatizo!

Hii nchi ni moja na huru na ni yetu, kwa nini majengo mengine yasijengwe nje ya miji kama walivyofanya idara ya hali ya hewa kujenga Ukonga!! Sasa hivi kila kitu City Centre na ndio maana asubuhi watu mjini jioni watu nje ya mji, hii ni hatari. Iko siku gari moja litawaka kwenye foleni na mengine yashike moto sijui itakuwaje!! Tuchukue hatua na maamuzi magumu kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
Terrible ordeal...na hizi equipment za kuunga-unga.Taabu tupu.
 
Twahitaji Watu Wenye Ujuzi, Vifaa, Sera nzuri zenye kuzingatia maslahi ya watu wanaofany kazi za hatari, na Uzalendo!!

FFE2.jpg
 
uwiiiiiiii pole kwao wote!! hii nchi hii!! MUNGU atusaidie sana!
 
moto kama huo hua unazimwa kwa hericopta au ndege kwanza ninyi mnapeleka zimamoto itafika ghorofa ya 11??kama serikali haina ndege wala hericopta ndio pa kujipanga kununua ili kudhibiti hali kama hiyo
 
Kama nchi haiwezi kuzima moto iwapo utatokea kwenye jengo lililopo kuanzia mita fulani juu ya ardhi, serikali inatakiwa kupiga marufuku jenzi wowote utakaokiuka hilo

Japan na maendeleo yake yote hadi mwaka 1964, ilikuwa na marufuku ya majengo kuzidi urefu wa mita 30 juu ya ardhi kutokana na hofu ya ajali zitakazotokana na matetemeko ya ardhi.

Wizara ya ujenzi inapaswa kuwa makini inapotoa vibali vya ujenzi kwa sababu kazi yake moja ni ku-verify kuwa jengo ni salama wakati wa ujenzi na utumiaji.

Kama zimamoto haina vifaa vya kufikia majengo marefu, yakataliwe vibali
 
Acheni porojo embu mlioko eneo la tukio mtujuze umezimaa?
 
Majanga kama haya yalishatokea na uchunguzui ukafanyika lakini taarifa huwa hazitolewi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=81771&stc=1&d=1359876655
 

Attachments

  • Screenshot_2013-02-03-10-30-50.png
    Screenshot_2013-02-03-10-30-50.png
    219.2 KB · Views: 5,056
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom