Moto wawaka jengo la PPF Tower - Dar

Moto wawaka jengo la PPF Tower - Dar

Status
Not open for further replies.
Tatizo kubwa ni vifaa vya majanga ya moto hakuna labda yanavyoungua majengo yao wataliangalia upya ili suala.
Tatizo kubwa ni CCM, wanawapa vifaa vya kutosha askari wa FFU ili wapambane na raia wema wanaodai haki yao lakini wanawaacha askari wanaotakiwa kushughulikia majanga na dharura ili kuokoa maisha ya watu.

Mbona hatukuwahi kuambiwa gari la maji ya kuwasha limeishiwa maji ya kuwasha kwa hiyo tuchangie? Au kwamba FFU wamekosa mafuta kwenye magari yao kwa hiyo tuchangie? Tukivamiwa na majambazi usiku, tukawapigia simu polisi watakwambia gari halina mafuta. Hovyo kabisa CCM! Kuwa na chama kama CCM ni laana kwa nchi!
 
Iliungua WTC unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au kule hakuna umeme
Hata ikulu moto ulishawahi tokea!
 
hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo, tunaweza jenga majengo marefuuu lakini vifaa vya kuzimia moto majengo kama hayo kimeo
 
Kwa akili yake madhara ni kuumia tu!!! Kwani hicho kinachoungua kilinunuliwa kwa kutumia simbi, ebu kama hajui mambo aache kubwabwaja. Angesema madhara ya moto huu hayajulikani hadi hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika. Watangazaji makanjanja ni janga la kitaifa.

As usual Watanganyika we need a new culture and marshal plan with modern fire fighting system . Hii ya kutumia mobile itakuja kutupeleka pabaya. Kwanza hatuna maji na hao watu wa Magufuri pamoja na tambo zao including CRB , mambo ya ndani hawana ujuzi wa fire tenders na ndio maana wanatoa certificate za occupancy bila kuzingatia mambo muhimu kwa mfano ventilation and even spacing between buildings achiilia mabali moto. This is a crazy Gang without any connectivity it's just bora liende!
 
Iliungua WTC unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au kule hakuna umeme

Usiseme hujawahi sikia Ikulu kuungua moto? Mbona kulitokea tatizo la Moto ikulu enzi za mwisho za Mkapa sehemu ya Ikulu iliungua ikiwemo library maalum ya Rais hadi kupelekea kufanyika ukarabati mkubwa? Hukuwa umepitapita ikulu muda mrefu eenh!?
 
haya mambo ya kuungua ofisi weekend watu wwakiwwa hawapo kazini kunaleta utata sana

... Mkuu' inashangaza sana' jinge hili lina ofisi nyeti, tena nyingine za ukaguzi wa mahesabu ya taasisi nyeti hapa nchini.
Isije ikawa kama ile ya benk kuu ya Tanzania.
 
Tatizo nini au watu washatia moto nyaraka za siri kuficha ushhidi wa wizi wao kama ilivyofanyika mika ya 80 enzi zile za wizi wa beni na yule muheshimiwa naniliu......

Sitashangaa kusikia nyaraka zimeungua, maana hata mimi kuna pesa zangu zilipelekwa huko halafu nikicheki account hakuna kitu.
 
:israel:hilo nalo ni janga jingine tz bhana majanga kila kukicha jamani tumuite yule muimbaji wa hip hop roma awaumbue wakandaras au ni mchezo waho walishazoea
 
Nyaraka mhimu zitakuwa zimechomwa kwa manufaa ya makupe machache.
 
Iliungua WTC unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au kule hakuna umeme

Alafu siku pale kuna twin tower. Wasipoongeza umakini ohoo!
 
Ppf tower ya wapi? Mbona huweki mambo yaeleweke!

Kifai wee una lako Jambo! Au mitaa ya Jiji la Dar huifahamu? Mbona Kasema Jengo la PPF lililoko makutani ya Ohio na Garden Avenue katikati ya jiji la DSM. Kwa nyongeza na faida yako jengo liko Posta
 
aiseee hapa watu washafutwa kazi na kupokonywa contract, hakuna kampuni ya simu inayoweza vumilia aibu hii, labda tu huyo contractor aliyesababisha haya awe na mikono mirefu zaidi ya maelezo.
 
Sio lazima mipira ya magari ifike floor ya juu, majengo yote ya kisasa hua yana mabomba yalioanzia ground floor yakupeleke maji ya kuzimia moto kila floor na kila floor inamipira ya kutolea maji ya kuzima moto! Hivyo tatizo linaweza kua ni pump za kusukuma maji hazina nguvu au firefighter wetu waoga wanaogopa kwenda floor inayoungua kupitia ngazi za jengo.

Sio kila moto unazimwa kwa maji. Kuna moto unaozimwa kwa powder maalum nk nk.
 
Waafrika tuna definition mbovu sana ya maendeleo. Ukienda kwenye website ya Michuzi utaona anasifu "vikwangua-anga" vinavyoongezeka katika jiji la Dar. Cha kusikitisha, hatujawahi kujiuliza kama tuna miundo mbinu inayoendana na hayo majengo. Ni jambo la kushangaza tunaweza kununua baiskeli lakini tunashindwa kuona umuhimu wa kununua pampu.
 
Iliungua WTC unashangaa PPF? Acha makandarasi watengeneze deal, TUMESHAWAZOEA. Af utasikia "ooh, shoti ya umeme", pumbaf, mbona ikulu hatujawah sikia, au kule hakuna umeme
Iliwahi kuungua kipindi cha mkapa mkuu....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom