Moshi: Watu 20 wapoteza maisha kwa kukanyagana kwenye Ibada ya Mwamposa; Polisi wathibitisha kumshikilia

Brain washed..laa utakua mchepuko wa bulldoza wewe..so niambie wapi kristo alimwaga mafuta kwenye kongamani...
Nilicho gundua watu walio wengi humu Jf mnapenda kuongelea vitu kimihemko sana na porojo za kuchangamsha akili kuliko kuongelea uhalisia ambao una ukweli wa kutosha ambao haupendwi wala kusikilizwa na watu wengi wajinga,
Mara nyingi Mwamposa amekuwa akiandaa makongamano ya kukanyaga mafuta Dsm na watu wengi kuponywa na kokote aliko enda halijawahi tokea tatizo lolote iweje Moshi wakati wa kukanyaga mafuta bahati mbaya wengi wakadondoka na kukanyagana, mtu anatokea aliko toka eti "wajinga ndio waliwao" mnamkosea sana Mungu,
Jifunzeni kufanya research vya kutosha kabla ya kutenda wala kuongea lolote, kuna mtu ame-reply eti mafuta ya upako ni kama hirizi tu, na yametajwa hadi kwenye biblia na matumizi yake, Muogopeni Mungu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio yeye tuu kuna tb joshia nae kanisa liliia kuna kibwetere nae aliwasha moto kabisa
Yaani hizi imani nyingine tabu tupu
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Umaskini ni mbaya sana. Huyo mchungaji akamatwe haraka sana.
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa,sijawahi amini katika huu upuuzi,ivi wakristo nani katuroga......upumbavu sana huu hata hawa walikufa wala binafsi roho hainiumi
 
Hapa Kuna haja ya kujifunza kwa Kagame lazima wachungaji wawe na kiwango fulani Cha Elimu na sio Kila Mtu kuwa mchungaji kwani bado taifa let Lina kiwango kidogo Cha wasomi ambao wanaweza kung'amua lipi Ni sahihi na lipi sio sahihi, Tafsiri ya vitabu vya dini imekuwa ni changamoto
Kwani hao wanaoenda kukanyaga mafuta dogrii hawana? Kikombe Cha Babu walifurika kukinywa Hadi maprofesa.Imani kitu kingine kabisa issue sio elimu
 
Hapa Kuna haja ya kujifunza kwa Kagame lazima wachungaji wawe na kiwango fulani Cha Elimu
Mauaji ya kimbari Rwanda yaliongozwa na mapadri na maaskofu wa kanisa katoliki ambao wote walikuwa na digrii za theolojia.Kagame hajielewi.Yeye mwenyewe huwa anaenda kusali Nigeria kwa TB Joshua ambaye hajawahi somea uchungaji maisha Yale yote
 
Waumini 18 wa Dini ya Kikristo wamefariki dunia usiku huu mjini Moshi, wakati wakikanyagana kugombea kukanyaga mafuta ya upako katika kongamano la kidini la Mtume Boniface Mwamposa, DC wa Moshi Kippi Warioba amethibitisha

Updates: 00:45
Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa kukanyagana imefikia 20 na uenda idadi hiyo ikaongezeka Mkuu wilaya amethibitisha.

UPDATES:
Watu 20 wamefariki dunia leo jioni Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa waumini hao walikumbwa na maafa hayo wakati wakikanyagana kwa ajili ya kugombania kukanyaga mafuta yaliyomwagwa na mhubiri huyo yakidaiwa kuwa na upako.

Inaelezwa kuwa watu zaidi ya 40 walikanyagana katika harakati za kugombania mafuta ya upako na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka kwa kuwa hakuna taarifa ya ujumla ya majeruhi waliopelekwa katika vituo vya afya vya jirani pamoja na Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amelithibitisha leo saa 5:00 usiku kuwa taarifa za awali waumini 20 wamekufa lakini akasisitiza hizo ni taarifa za awali.
“Taarifa za awali tulizonazo ni kuwa ni waumini 20 wamepoteza maisha lakini tunaendelea kufuatilia maeneo mengine ya zahanati, vituo vya afya na hospitali kama kuna watu walipelekwa huko,” amesema Kippi.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Mhubiri huyo alielekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akitaka kuondoka, lakini ndege aliyokuwa amepangwa kuondoka nayo ilichelewa (delayed) na ndipo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro lilipomtia mbaroni uwanjani hapo.
Apostle Boniface Mwamposa a.k.a Bulldozer

Chanzo: Mwananchi

=====


MWAMPOSA ATAKIWA POLISI KWA MAHOJIANO

Jeshi la Polisi limemtaka Boniface Mwamposa kujisalimisha polisi kwa mahojiano ya vifo vya watu 20 vilivyotokea mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro usiku Februari Mosi, 2020

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Elia Mwambapa ndiye aliyeomba kibali cha kongamano hilo la siku tatu lililomalizika jana Jumamosi

Amesema baada ya hilo tukio wamemtafuta sana huyo Boniface Mwamposa maarufu kama Bulldozer bila mafanikio. Na kumtaka ajisalimishe kwa mahojiano

Kamanda Hamduni alifafanua kuwa idadi ya waliokufa ni 20 hadi sasa, ambapo kati yao watoto wadogo ni wanne, watu wazima 16
*Living with Religious OCD (Scrupulosity)*

What’s Going On?

Religious OCD, also known as *Scrupulosity*, is an observed condition that dates back to the 1600s in the Catholic church. It was noticed that some monks were engaging in excessive prayer. Their behavior and constant praying weren’t in keeping with what they believed to be an expression of God’s love. They were actually trying to achieve an unrealistic state of holiness. This is where the term Scrupulosity comes from.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*Living with Religious OCD (Scrupulosity)*

What’s Going On?

Religious OCD, also known as *Scrupulosity*, is an observed condition that dates back to the 1600s in the Catholic church. It was noticed that some monks were engaging in excessive prayer. Their behavior and constant praying weren’t in keeping with what they believed to be an expression of God’s love. They were actually trying to achieve an unrealistic state of holiness. This is where the term Scrupulosity comes from.

Sent using Jamii Forums mobile app
*Common Scrupulosity OCD obsessions:*

Fear of living a life of sin or one that God wouldn’t approve of.
Fear of doing something that doesn’t align with your moral or ethical standards.
Constantly wondering if you’re praying enough or the right way.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom