MORUWASA ndiyo mamlaka ya maji ya ovyo sana Tanzania

Algore

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
2,097
3,362
1. Maeneo mengi ya Morogoro mjini hayana maji toka June, 2022 wao wamekaa tu kama hawahusiki.

2. Sehemu zinazopata maji hasa eneo la Bong'ola, maji hayo ni machafu na hayatibiwi.

3. Bili haziakisi kiasi cha maji mteja alichotumia

4. Matatizo ya wateja hayafanyiwi kazi

4. Waziri wa maji tunakuomba uje uongee na wanao. Umeweza dawasa, hawa moruwasa hawakushindi.
 
Waziri usimuombe bali MUAGIZE afanye hili na lile mnalohitaji kumuomba ni makosa , huyu ameapa kuihudumia jamii huru ya watanzania
 
Ni kugombana tu na Wakandarasi. 10% isipotolewa basi mradi utatiwa mzengwe na wananchi wanakiona Cha mtema kuni.

Moruwasa hii bila mabadiliko ni kazi bure
 
Aah bwana Moruwasa imeshindikana. Mji wa Morogoro ni mji wenye miundombinu duni sana. Wapigaji ni wengi sana. Kuna jamaa mmoja alisema kuna "kuna nyuklia" (uchawi) umetegwa pale milimani ukija na kidomodomo chako hutoboi.
 
Aah bwana Moruwasa imeshindikana. Mji wa Morogoro ni mji wenye miundombinu duni sana. Wapigaji ni wengi sana. Kuna jamaa mmoja alisema kuna "kuna nyuklia" (uchawi) umetegwa pale milimani ukija na kidomodomo chako hutoboi.

Hamna mkuu basi tu viongozi wa moro na wananchi wake wana rabia za pwani pwani! We angalia mlima ule kule juu unaona kabisa wamejenga juu ya mlima lakini hakuna anaesema chochote yani wapo kimya!!! Unategema kweli tutapata maji yakutosha....... na bado maji mgao alafu mbaya zaidi iyo bill ikija unaweza kushanga nakuchoka kwa pamoja
 
Back
Top Bottom