Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,106
Kwako ndugu Waziri mwenye dhamana ya mambo ya maji.
Iko hivi:
Bili ambazo watu wa DAWASA wanawatumia wananchi siyo bili za kweli, haziakisi matumizi halisi ya maji ya wateja. Ni bili za kupikwa.
Haiwezekani bili yako kwa miezi ya nyuma iwe ni shilingi X halafu ghafla bin vuup bili inaamza kuja mara tatu ya ulivyokuwa ukitumia.
Ndugu Waziri, DAWASA na wizara ya maji isituone sisi wananchi ni Wapumbavu. Tunajua kuwa Unit Moja ya maji ni Lita 1000. Na Tunajua kuwa bei ya Maji kwa Unit Moja ni around shilingi 1670 hivi. Unapomletea mtu bili ya Maji ya Shilingi laki moja kwa mwezi maana yake ni kuwa katumia Unit 59.9 kwa mwezi ambayo ni sawa na Lita 59900! Hii inawezekanaje wakati Matumizi ni ya kawaida, kupikia, kuoga, kufua na maji hayatumiki kibiashara wala kwa kilimo na WALA HAKUNA LEAKAGE YOYOTE?
Ndugu Waziri nataka nikueleze ukweli, Familia nyingi zinatumia Chini ya Unit moja au maximum Unit moja kwa siku, lakini cha ajabu bili zinakuja zikiwa inflated sana.
Ndugu waziri,
Ninafahamu, kuwa kuna uhuni katika usomaji wa mita, wakati mwingine wale vijana hawazunguuki kusoma hizo mita wanakadiria!
Wakati mwingine kuna uhuni unafanyika kwenye kutuma meseji ya kiwango ambacho mtu anadaiwa, Sometime Message ya malipo haitaji Units ambazo mtu kazikuta mwanzo wa mwezi na mwisho wa mwezi anatajiwa Pesa tu. Yote hii ni kuficha traces ili wananchi wawe gizani kama billing imefanyika kwa haki au la
Ndugu Waziri,
Kisingizio kikuu ambacho DAWAS hutoa ni kwamba kuna leakage, lakini keakage wananchi tunaijua, kama kuna leakage basi Mita lazima itakuwa inazunguuka hata kama mtu hatumii maji!- Hapa kuna magumashi hapa
Ndugu Waziri,
Athari za kubambikiza watu kodi ya Maji ni watu kumchukia rais.
Kwa kuwa nchi hii hii power na mamlaka in reality ziko kwa rais( achilia mbali wananchi), basi madhila na maumivu yao lawama na manung'uniko haya ya bili za kubambika za maji wanamtupia rais. Na kwa kuwa maji yanagusa watu wote ndani ya familia, basi kitendo cha mlipa bili kumnung'unikia rais mbele ya familia nzima kunaifanya familia nzima isimuelewe rais.
Rai yangu:
1. Timiza wajibu wako kwa kuchunguza hizi bili feki za DAWASA
2. Vijana wavivu wasiokwenda site kusoma bili ila wanakaa kwenye computer kuzitengeneza fukuza kazi.
3. Toeni tamko la kuelezea kinagaubaga juu ya hili jambo linaloikwaza jamii
4. Shirikisheni wananchi kwenye kusoma mita. Mkisoma mita acheni kipande cha fomu kuwa mlikuja saa ngapi kusoma hiyo mita, mmekuta unit ngapi na mumtake mteja akahakiki. Siyo mnakuja kimyakimya kama wachawi. Hatuwaamini sisi!