BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Huku Mbezi Louis maeneo ya Mtaa wa Mshikamano Jijini Dar es Salaam hakuna maji ni mwezi sasa (Hadi muda naandika andiko hili Februari 10, 2024).
Mara chache yanayoka usiku mwingi, Watu wanasumbuka kuamka mida hiyo na kukuta maji yanayotoka ni machafu balaa.
Imagine kukaa mwezi mzima maji yanasumbua na hakuna taarifa yoyote kutoka kwa mamlaka.
Serikali ya mtaa haitoi taarifa yoyote na DAWASA nao wamekaa kimya. Hii inamaanisha nini kwa wakazi wa huku? Hili joto linaloendelea hapa wanategemea watu wanaishi vipi?
Sasa tunashangaa hatutangaziwi uhaba wa maji wakati mvua zimenyesha kwa muda mrefu sana. Kwani kuna shida gani kutuambia kuwa ratiba ya maji itakuwa ni kila baada ya wiki na yatatoka usiku wa manane tu?
Kwakweli Mbunge wa Ubungo na viongozi wa Halmashauri ya Ubungo wanatuangusha sana jamani.
Tunaomba serikali ifanye kutatua hii changamoto. Kama kuna matengenezo ya mabomba tuambiwe. Kama kuna uhaba wa maji tuambiwe.
Uongozi unaokalia taarifa kwa mtindo huu unatia mashaka sana. Viongozi wa serikali za mtaa hadi Halmashauri wanapaswa kuwajibika kwa hili. Kukalia taarifa si jambo zuri. Ni aidha watuambie hatutapata maji kabisa au watuambie ni lini yatapatikana.
Mtu unataka kujisaidia ila hata ukienda baa nako hakuna maji. Hii si sawa kabisa. Tunataka maji yatoke leo, vinginevyo tujulishwe lini yatatoka lini.
==== =====
Jamii Forums imezungumza na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Baraka Mwaijande kuhusu changamoto hiyo amesema “Kweli changamto hiyo ipo, uwepo wa changamoto ya umeme umesababisha hali hiyo ya maji.
“Nawasiliana na DAWASA ambao wanafanya kazi kwa bidi kule Ruvu ili huduma ipatikane, kumbuka kuwa mitambo yao inatumia umeme na hivyo kama hakuna umeme wa uhakika basi hata ufanyaji kazi pia unakuwa hauna ubora.
“Madai kuwa kuna maji machafu yanayotoka usiku hilo sijawahi kuliona wala kupata malalamiko hayo.”