Moja ya Kauli za Kukatisha Tamaa za JK

"Sina namna ya kugeuka kuwa wingu la mvua nikaenda kugeuka wingu kubwa la mvua pale Mtera." Alisema Rais Kikwete alipoulizwa maswali na Waandishi wa Habari wakati anatembelea maonesho ya Sabasaba majuzi! Source: Tanzania Daima. My take: Kwa kauli hii Kikwete ataondoka madarakani akiwa hajatatua tatizo la umeme! Kauli nyingine aliyowahi kutoa ni pale alipodai kwamba hajui kwa nini Tanzania ni maskini!
Najivunia zuzumagic wangu, the most handsome, a.k.a the traveller
 
Ni jambo ambalo halielezeki kirahisi kwa rais wa nchi kutoa kauli hii. Hii ni kauli ya kukata na kukatisha tamaa. Ina maana kuwa hakuna ufumbuzi. I think it might be a joke of the year!
 
HATA WAZEE WALIWA PLEASE
WATOTO WAO WAKATI wa NJAA KALI KWA KUWAPA MATUMAINI YA KULA "watoto chocheeni moto hicho chungu chakula kiive kumbe ndani ni mawe au vipande vya miti" rais hapaswi kuwa na majibu ya kujoki wakati watu wanateseka
 
sio kazi ndogo mkuu! zile kauli zake za ARI MPYA, NGUVU MPYA NA KASI MPYA na baadae ikawa ARI ZAIDI, KASI ZAIDI, NGUVU ZAIDI ndo sasa inaonekana kuwa na maana zaidi kimtizamo hasi.

Zumbe sasa hii ZAIDI ndio itatuua !
 
TUNA MASWALI HATUNA MAJIBU! TUNA MATATIZO HATUNA UFUMBUZI!
Akili zetu zilidumazwa! Waliotudumaza wangali nasi wakitutazama kama mdato umetuisha watuongezee mwingine!!
Hatujitambui wala bado hatujifahamu...
Ndio maana bado hatutofautishi nyigu na nge! Tunawafananisha kabisa bila kujua wote ni wadungaji! Sijui tumerogwa?
 
ila ukimuuliza jamaica kuna bembea ngapi za kubembea atakutajia zote na hadi mitaa zilipo lakini si mambo ya nchini kwake huyu mtalii.
 
****** hana jipya.mipasho na majungu na kukenua meno wakati hali ni tete kwa mtanzania wa kawaida.
 
Umeelezea vizuri sana, lakini mpaka leo hii Tanzania hatuna heavy Industries zinazofanya production 24/7. Na sio kama umeme hakuna kabisa bali unapatikana kwa mgao, sasa tatizo hakuna maji ya kutosha tunafanyaje Kwasasa kama bado tupo ktk long run plan zakutafuta vyanzo mbadala?
Mkuu sijui kama umemsikiliza makamu mwenyekiti wa CTI bwana shah alivyokuwa akitoa athari za matatizo ya umeme huu. Amesema udhalishaji umeshuka kwa 30 perc. Hii ina maana gani basi kwa mtu wakawaida? Nilazima bei ya vitu ipande maana market huenda kwa supply/demand system. Bidhaa zikipungua sokoni bei inapanda. Pia TRA wamepoteza mapato kwa sababu uzalishaji umeshuka hivyo serikali imepungua uwezo wa kuhudumia wananchi. Kuna madhara makubwa ya kukosekana kwa umeme, haya ni yale ya indirect lakini yapo ya direct kwa mwana nchi wa kawaida kama kukwama kwa biashara ndogondogo,kuharibika kwa vyakula vya akiba kwenye storage zetu hivyo kuharibika kwa budget za watu.Mkuu kumbuka tatizo la umeme usioaminika kimekuwa ni kikwazo kikubwa cha uwekezaji wa viwanda na makampuni makubwa nchini. Nimesikia JK anawashawishi wamarekani waje kuwekeza lakini wanamwambia nenda kahakikishe kwanza umeme wa uhakika na nafuu. Hivyo umeme unaturudisha nyuma ki uchumi.umeme ni moja ya miundo mbinu mihimu katika kujenga uchumi kama ili barabara,reli,viwanja vya ndega nk.
 
'Wanafunzi wanaopata mimba ni kwa ajili ya viherehere vyao'.Sijui tunaelekea wapi watanzania na hawa viongozi wetu
 
Aalijua kuwa atakuja kucheza kiduku. Atakacho jivunia ni kututoa hapa na kutupeleka pale. Yaani kutoka gizani kwenda gizani zaidi.period
"sina namna ya kugeuka kuwa wingu la mvua nikaenda kugeuka wingu kubwa la mvua pale mtera." alisema rais kikwete alipoulizwa maswali na waandishi wa habari wakati anatembelea maonesho ya sabasaba majuzi!

source: tanzania daima.

my take:
kwa kauli hii kikwete ataondoka madarakani akiwa hajatatua tatizo la umeme! Kauli nyingine aliyowahi kutoa ni pale alipodai kwamba hajui kwa nini tanzania ni maskini!
 
kuna kitu jeshini wanaita maintenance of morale...yaani hata mkipigwa kamanda wenu anasema hawa tumeshawashinda na sasa hizo wanazopiga ni za mwisho wameishiwa kabisa...kumbe anatafuta plan b...sasa huyu rais wetu nasikia alikua jeshini lakini sidhani kama huyu jamaa anaweza kuongoza nchi ikashinda vita yeyote achilia mbali hii ya umeme,njaa,umasikini,wizi,,uporaji wa mali za umama!!! Ikija

vita kabisa hapa ya mtutu atakimbia kabisa..

jeshini alikuwa ni mtu wa fitina na kuendekeza politics ndo maana alikimbia monduli. Nadhani wajua kwa nini alikimbia monduli ilyokuwa chini ya sayore.
 
Dah hii kauli inasikitisha sana Sasa watu na mifugo wakifa njaa sababu ya ukame majibu si yatakuwa hayo hayo. Jamani Ukame si unatabirika. Kwani imekuwa ajali ya ghafla kama tetemeko la ardhi au mafuriko.

may be kisukari napressure vilipanda wakati anajibu swali hilo.
 
wakati baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini wamesahau kauli chofu za JK ambazo zinahoji uwezo wa kuliongoza hili taifa.................mimi nina kumbkumbu zifuatazo ya kauli zilizomshushia heshima JK mbele ya jamii ya watanzania nazo ni pamoja na:-

1) Ahadi ya Dr. Slaa ya kujenga Bullet train itakayo safari masaa matatu toka Dar hadi Mwanza...............................JK alipokuwa anafunga kampeni zake za Uraisi Dar alizibeza kwa kusema kuwa............................hayo mawazo ya Dr. Slaa................"are absolutely ridiculous".........

Kwa maoni yangu kiongozi who can not dare to dream is unfit to govern.................................the World has ALWAYS belong to a dreamer irrespective of the final outcome........................................................

Katika karne ya 21 kama huoni Tanzania inamiliki Bullet train then you must pack your bags and go home.....................because that is where you belong...................


2) Alipokuwa kwao Bagamoyo, JK alidiriki kuwakandia waathirika wa ukimwi kuwa....................ni kiherehere chao ndicho kimewafikisha hapo walipo.........................................................sayansi inapingana na kauli hii chofu kwenye maeneo mengi......................waathirika wengi wamesogezewa gonjwa hili na wala siyo kuutafuta............hivyo kuwahukumu bila ya kujua sababu za kuupata ugonjwa huo ni kukosa utashi wa zana pembuzi.....................

3) JK ni gwiji wa kulaumu wale wote ambao wanafanya makosa bila ya kujua ya kuwa kama yeye alikuwa ni bora zaidi yao angeliwashauri kabla ya uzembe kujitokeza lakini siyo baada ya matatizo kujitokeza..........................kama mwingereza asemavyo......................are we not wiser afterwards?

kauli tata za JK zipo nyingi anayezikumbuka nyinginezo azibandike hapa.....................................
 
Sasa wewe umekuja kumponda Rais hapa kwa kukusanya vikumbukumbu vyako visivyokuwa na kichwa wala miguu. Yaani umeishiwa hoja unaanza kuleta chochote kile.
 
Back
Top Bottom