Moja ya Kauli za Kukatisha Tamaa za JK

Hivi hapa Tanzania ni asilimia ngapi ya watanzania wanatumia umeme? Lazima tujue kuwa tunapolifanya tatizo la umeme kuwa ni janga la Taifa tunawakosea wengine wenye matatizo makubwa zaidi ktk maswala ya Afya, Elimu na Usafiri.

Umeme bado kwa asilimia kubwa bado unategemea vyanzo vya maji hivyo jibu lake kwa short run solution yupo sawa maana wengi wanalaamu kwa wakati huu ila kwa long-run walisha sema ifikapo 2015 tatizo litakuwa historia. Tatizo lipo wapi hapo.

Kama huoni tatizo liko wapi, basi wewe mwenyewe ni tatizo!!!!!

Tiba
 
..miaka 6 madarakani bado analeta visingizio vya uhaba wa maji/mvua!!!

..CCM wangekuwa na uchungu na nchi hii wangeshamfukuza uongozi, wasingempa second term.
 
Nadhani wanaokuwa frustrated na JK ni wale ambao bado wana matumaini kuwa ipo siku, kwa miujiza fulani huyu baba atageuka na kuwa rais wa nchi.

Ukishakubali tumekula hasara ya miaka 10, ukisha kubali JK atasema chochote, ukishakubali serikali hii imeshindwa basi utamchukulia poa tu huyu mzee. Tuendelee na maisha jamani huyu mtu habadiliki na haondoki mpaka 2015.
 
Hivi hapa Tanzania ni asilimia ngapi ya watanzania wanatumia umeme? Lazima tujue kuwa tunapolifanya tatizo la umeme kuwa ni janga la Taifa tunawakosea wengine wenye matatizo makubwa zaidi ktk maswala ya Afya, Elimu na Usafiri.

Umeme bado kwa asilimia kubwa bado unategemea vyanzo vya maji hivyo jibu lake kwa short run solution yupo sawa maana wengi wanalaamu kwa wakati huu ila kwa long-run walisha sema ifikapo 2015 tatizo litakuwa historia. Tatizo lipo wapi hapo.
Tukilitazama tatizo la umeme kwa mtazamo wako ni 10 perc tu ya watanzania wanatumia umeme kuwasha japo taa. Lakini kama umepevuka unaweza kutambua kuwa umeme ndiyo unaotumika viwandani kusaga unga,kuzalisha sukari kukoboa mpunga n.k.

Kwa mtazamo huu kama umeme haupo basi nadhani unaweza kuona madhara yake. Na kwa mtazamo huu mpana je ni watanzania wangapi wanatumia unga? Sukari? Mchele? Chumvi? Ngano?Nadhani umeelewa kuwa tatizo la umeme siyo kama unavyofikiri kwa mtazamo mfupi kama huo. Unaposema serikali imetoa long term plan hadi 2015, ninani asiyejua mipango mizuri ya kila kitu tuliyonayo watanzania lakini miaka inapita na hakunakinachotekelezwa?

Hatujashuhudia watu wakizindua mipango mizuri kwa mbwembwe na hudiriki hata kufanya sherehe lakini baada ya hapo yote kapuni? Unataka kutuaminisha nini na serikali hii ya magamba kama ndo mtazamo wao kuwa hakuna suluhisho la tatizo hili isipokuwa mvua zinyeshe?

Tanzania tunaweza kutatua tatizo la umeme pasipo kutegemea mvua tukiamua. Lakini hatuta tatua tatizo hili kama tutaendelea kulitumia tatizo la umeme kwa manufaa ya mafisadi kujitajirishia kupitia miradi ya dharula.Tuwapeni nchi hii watu wenye nia njema na watanzania hatutaona matatizo haya tena lakini hatutakaa tutoke kwenye hili lindi la umasikini kwa kuendelea kucheka na CCM.

Ukicheka na nyani utavuna mabua!
 
Wewe jigeuze wingu uende ukanyeeshe Mtera au kokote kwenye ukame, unangoja nini?
 
Unajua pamoja na matatizo yote haya uchaguzi ukiitishwa leo CCM watashinda sababu watz hatuna uthubutu hatutaki mabdiliko na ndo mtaji wa CCM, Kikwete hata mumsemeje anajua hatarudi tena, so anafanya ajuavyo yeye!

Najuta kuwa Rais kama huyu yupo yupo tu kama amekosa maono ktk kipindi hki kigumu hamna umeme, ajira, miundo mbinu mibovu, uvivu maofisini
 
Wewe jigeuze wingu uende ukanyeeshe Mtera au kokote kwenye ukame, unangoja nini?

Majibu kama haya yanaonesha ni jinsi gani, some members kama FF wanataka kuigeuza JF kuwa kama Bunge la Jamhuri ya Muungano (Sehemu ya mipasho, badala ya kujadili mambo kwa tija na mustakabali wa Taifa). JF ingekuwa na watu wenye majibu kama haya from 2006, ni dhahiri vichwa vyenye kufikiri beyong kulinda ulaji visingeweza kujiunga.

Topic ina-invite healthy discussion ya mambo yanayolitafuna taifa kutokana na kutokuwa na watu makini waliopewa mamlaka, leo anajitokeza mpambe na kuja na majibu rahisi, mtu makini angeanza na kutafuta uhalali wa kilichowekwa na mtoa mada, je kimetokea kweli? Then katika mazingira gani? Na kwa nini?. Je majibu haya yanapotolewa na CEO wa nchi mwenye mamlaka ya kuhakikisha kuwa consumer confindence is higher what will happen to the market?.

Tutetee yanayoonekana ila tukianza kutetea mpaka kinyesi kwa kulazimisha kuwa si kinyesi ni chakula basi hapo tutakuwa tumepoteza maana ya kuwa hapa, labla wewe uwe ni muathirika wa moja kwa moja na unatetea uozo wako under cover.
 
Umasikini wetu ni wa akili tu!Poverty of philosophy.Pamoja na madudu yoooooooooote ya JK bado US inamlinda usipime,jiulize amewahidi nini???
 
Wewe jigeuze wingu uende ukanyeeshe Mtera au kokote kwenye ukame, unangoja nini?

Hivi hata bwana wako unampenda kama unavyoipenda ccm? Hapa hoja siyo kikwete kugeuka wingu ni uwezo wake wakushughulikia hili tatizo ukizingatia jamaa yako alishawahi kuwa waziri kwenye hii wizara! Kwa mfano kwanin asitumie vyanzo vingine kama makaa ya mawe na upepo ambavyo vipo? Yeye anang'ang'ania mvua tu!
 
Amwachie Dr Slaa, hao mafisadi anaowafuga watakimbia nchi na "kufariki" kama Dr Ballali!
mkuu kwenye red hapo ni kwmba dr.balali yupo hai ila kafichwa kisiwa flani cha maraha,alifanyiwa facial surgery,ana siri nzito huyu bwana...
 
Kauli kama hiyo aliitoa Dodoma kwenye sherehe za Magamba alisema " natamani ningekuwa mvua, ningeenda mtera ningenyesha weeeee kutoka hapo ningeenda Mto wa mbu, ningenyesha weeee lakini mimi sio mvua, tatizo hili hatuna wa kumlaumu
 
Wallahi, Rais wetu Mzuka 100%, nashangaa pale anapomalizia kuwa "anaamini kuwa miaka mitatu ijayo tatizo la umeme litakuwa limekwisha na kutakuwa na megawati 3,000"
 
Wewe jigeuze wingu uende ukanyeeshe Mtera au kokote kwenye ukame, unangoja nini?
Hapo utakuwa umekosea,binadamu tuna uwezo wa kutengeneza na kuivuna mvua.
Too bad Rais wetu anafikiria tofauti.1992 Energy policy haizungumzii mkakati wowote wa kulinda our water sources,mabonde yetu yanahujumiwa.
Hatuzungumzii rain harvesting,hatuna irrigation schemes za nguvu na environmental conservation kwetu ni hadithi.Mafuta hayawezi hata siku moja kumaliza tatizo la umeme,ila ni biashara nzuri tu.
Kumbukeni.....kumchinja kobe,timing!
 
"Sina namna ya kugeuka kuwa wingu la mvua nikaenda kugeuka wingu kubwa la mvua pale Mtera." Alisema Rais Kikwete alipoulizwa maswali na Waandishi wa Habari wakati anatembelea maonesho ya Sabasaba majuzi!

Source: Tanzania Daima.

My take:
Kwa kauli hii Kikwete ataondoka madarakani akiwa hajatatua tatizo la umeme! Kauli nyingine aliyowahi kutoa ni pale alipodai kwamba hajui kwa nini Tanzania ni maskini!
Kwa kauli hii anajionyesha uwezo wake wa kufikiri na uwezo wa washauri wake. Anaanza zile za malikia wa milki ya ufaransa aliyesema walio na njaa kwa kukosa mkate wale Keki. Ni nani anayetegemea au hata kufikiria kwamba anaweza kuwa wingu????analeta hadithi za hekaya za abunuwasi wakati nchi nzima imesimama na hatujui nani atatupa uongozi kutoka tulipo..Du Mheshimiwa anatusikitisha saaaana
 
Jk anadhani anawaongoza watu bangi na majibu yake pia yanaonesha ni mzito wa kufikiri hao washauri wake wanamshauri kitu gan huyu? alwayz i use 2 say 2naongozwa na majuha
 
Hapo mwenyewe unaona umejibu? Kama vibaraka wa CCM ndio wa dizaini hii basi kwishnei...isubiri mazishi rasmi
Wewe umeona kuwa ni jibu lile? Kasome tena ukiikuta alama ya kuuliza uje kuniambia ina maana gani?
 
Back
Top Bottom