Moja ya Kauli za Kukatisha Tamaa za JK

Kuna kitu jeshini wanaita maintenance of Morale...yaani hata mkipigwa kamanda wenu anasema hawa tumeshawashinda na sasa hizo wanazopiga ni za mwisho wameishiwa kabisa...kumbe anatafuta plan B...sasa huyu Rais wetu nasikia alikua jeshini lakini sidhani kama huyu jamaa anaweza kuongoza nchi ikashinda vita yeyote achilia mbali hii ya umeme,njaa,umasikini,wizi,,uporaji wa mali za umama!!! ikija vita kabisa hapa ya mtutu atakimbia kabisa..
Somoche umenigusa kwa mananeno yako hasa ikizingatiwa kwamba Mheshimiwa alikua Luteni Kanali. Kwa kauli yake kaweka silaha chini katika hili la umeme. Hivi hapa wananchi tunatakiwa tufanyaje??Hali hii haikubaliki
 
Kama tatizo lenu ni JMK, basi hamna ujanja, inabidi mngoje mpaka 2015. Mjaribu bahati yenu labda safri hii atakuwa mumtakae, ama kutoka cdm ama kutoka ccm.

Halafu nasikia Prof Safari ndio anaegombea urais 2015 kutokea Chadema.
 
"Sina namna ya kugeuka kuwa wingu la mvua nikaenda kugeuka wingu kubwa la mvua pale Mtera." Alisema Rais Kikwete alipoulizwa maswali na Waandishi wa Habari wakati anatembelea maonesho ya Sabasaba majuzi! Source: Tanzania Daima. My take: Kwa kauli hii Kikwete ataondoka madarakani akiwa hajatatua tatizo la umeme! Kauli nyingine aliyowahi kutoa ni pale alipodai kwamba hajui kwa nini Tanzania ni maskini!
Ageuke kuwa mbayuwayu nadhani itafaa zaidi ili awe anaruka ruka na kula wadudu.Kweli magogoni hamna mtu.
 
Nadhani wanaokuwa frustrated na JK ni wale ambao bado wana matumaini kuwa ipo siku, kwa miujiza fulani huyu baba atageuka na kuwa rais wa nchi.

Ukishakubali tumekula hasara ya miaka 10, ukisha kubali JK atasema chochote, ukishakubali serikali hii imeshindwa basi utamchukulia poa tu huyu mzee. Tuendelee na maisha jamani huyu mtu habadiliki na haondoki mpaka 2015.

Sawa tumsubiri aondoke kwa amani huyu Kihiyo type!

Lakini mbaya zaidi mkuu wataiba kura hawa watuwekee mtu ambaye hatukumchagua!!!

Sijui Wa-TZ tujipange namna gani wandugu ili kudhibiti huo wizi utakaofanyika 2015?

Kwa kweli hasara tuliyokula hatutaisahau mpaka kizazi hiki kifutike!!

Ikulu haina Kiongozi!
 
Hivi hapa Tanzania ni asilimia ngapi ya watanzania wanatumia umeme? Lazima tujue kuwa tunapolifanya tatizo la umeme kuwa ni janga la Taifa tunawakosea wengine wenye matatizo makubwa zaidi ktk maswala ya Afya, Elimu na Usafiri. Umeme bado kwa asilimia kubwa bado unategemea vyanzo vya maji hivyo jibu lake kwa short run solution yupo sawa maana wengi wanalaamu kwa wakati huu ila kwa long-run walisha sema ifikapo 2015 tatizo litakuwa historia. Tatizo lipo wapi hapo.
Inaonyesha wewe si mtanzani,halafu ni tegemezi hujui nini maana ya maisha.
 
Wewe umeona kuwa ni jibu lile? Kasome tena ukiikuta alama ya kuuliza uje kuniambia ina maana gani?
FF majibu yako yanaongeza chuki dhidi ya magamba badala ya kupungua! Mmewapuuza sana wananchi wachache waliowapa ridhaa na kura nyinginezo mlizochakachua ili kuhakikisha kwamba mnabaki madarakani kwa gharama yoyote! Kwa hiyo mnaona kuwapuuza wananchi walalahoi na kuwajibu mtakavyo ni sawa tu ili mradi "mliwanunua" kwa chumvi, t-shirt, khanga, sukari, nk wakati wa uchaguzi? Ipo siku mtaikimbia nchi kama akina Hosni Mubarak, marehemu Mobutu Sessesseko, nk! Remember you can fool people for sometime but not always!
 
Kama tatizo lenu ni JMK, basi hamna ujanja, inabidi mngoje mpaka 2015. Mjaribu bahati yenu labda safri hii atakuwa mumtakae, ama kutoka cdm ama kutoka ccm. Halafu nasikia Prof Safari ndio anaegombea urais 2015 kutokea Chadema.
"unasikia" tena kutokea ccm,vp kuhusu Mkama atagombea uraisi ccm?
 
FF majibu yako yanaongeza chuki dhidi ya magamba badala ya kupungua! Mmewapuuza sana wananchi wachache waliowapa ridhaa na kura nyinginezo mlizochakachua ili kuhakikisha kwamba mnabaki madarakani kwa gharama yoyote! Kwa hiyo mnaona kuwapuuza wananchi walalahoi na kuwajibu mtakavyo ni sawa tu ili mradi "mliwanunua" kwa chumvi, t-shirt, khanga, sukari, nk wakati wa uchaguzi? Ipo siku mtaikimbia nchi kama akina Hosni Mubarak, marehemu Mobutu Sessesseko, nk! Remember you can fool people for sometime but not always!

Tatizo lenu si CCM tatizo lenu ni Rais aliyeko madarakani, semeni kweli, kwani hao viongozi wenu wote, si walitokea CCM? walifanya nini walipokuwa huko? ambacho wakiwa nje ya CCM watakifanya zaidi? sikioni ila tu, wana uchu wa madaraka na wana agenda za siri zinazoambatana na mfumo wa itikadi fulani, kwani si tumeona nyumba za ibada fulani huko sumbawanga zikiwapiga marufuku maumini wao eti kwa sababu tu wamempigia kura Kikwete na hivi juzi tumeona chama cha kisiasa kinachofata dini fulani mpaka kwenye jina lake kikiwatembelea chadema, na tunaona viongozi wangapi wadini fulani wakiiongoza chadema kwa sasa? na wabunge wangapi wa kutokea hukohuko?

Tusidanganyane, ukweli uko wapi na "all roads leads to Rome".
 
Umeelezea vizuri sana, lakini mpaka leo hii Tanzania hatuna heavy Industries zinazofanya production 24/7. Na sio kama umeme hakuna kabisa bali unapatikana kwa mgao, sasa tatizo hakuna maji ya kutosha tunafanyaje Kwasasa kama bado tupo ktk long run plan zakutafuta vyanzo mbadala?
Tukilitazama tatizo la umeme kwa mtazamo wako ni 10 perc tu ya watanzania wanatumia umeme kuwasha japo taa. Lakini kama umepevuka unaweza kutambua kuwa umeme ndiyo unaotumika viwandani kusaga unga,kuzalisha sukari kukoboa mpunga n.k. Kwa mtazamo huu kama umeme haupo basi nadhani unaweza kuona madhara yake. Na kwa mtazamo huu mpana je ni watanzania wangapi wanatumia unga? Sukari? Mchele? Chumvi? Ngano?Nadhani umeelewa kuwa tatizo la umeme siyo kama unavyofikiri kwa mtazamo mfupi kama huo. Unaposema serikali imetoa long term plan hadi 2015, ninani asiyejua mipango mizuri ya kila kitu tuliyonayo watanzania lakini miaka inapita na hakunakinachotekelezwa? Hatujashuhudia watu wakizindua mipango mizuri kwa mbwembwe na hudiriki hata kufanya sherehe lakini baada ya hapo yote kapuni? Unataka kutuaminisha nini na serikali hii ya magamba kama ndo mtazamo wao kuwa hakuna suluhisho la tatizo hili isipokuwa mvua zinyeshe? Tanzania tunaweza kutatua tatizo la umeme pasipo kutegemea mvua tukiamua. Lakini hatuta tatua tatizo hili kama tutaendelea kulitumia tatizo la umeme kwa manufaa ya mafisadi kujitajirishia kupitia miradi ya dharula.Tuwapeni nchi hii watu wenye nia njema na watanzania hatutaona matatizo haya tena lakini hatutakaa tutoke kwenye hili lindi la umasikini kwa kuendelea kucheka na CCM. Ukicheka na nyani utavuna mabua!
 
Ngeleja mwenyewe kishoka tu,waziri gani unasoma bajeti kama unatangaza mpira?!! The guy is always not serious
 
Ngeleja mwenyewe kishoka tu,waziri gani unasoma bajeti kama unatangaza mpira?!! The guy is always not serious
How cud he be serious if the head of state is hopeless? Nobody is serious in ths country! I want to revolt.....
 
huwezi kuwa na jipya au ubunifu kama una serikali ya watu ambao hawajui kwa nini taifa ni maskini hata siku moja.
 
Tatizo lenu si CCM tatizo lenu ni Rais aliyeko madarakani, semeni kweli, kwani hao viongozi wenu wote, si walitokea CCM? walifanya nini walipokuwa huko? ambacho wakiwa nje ya CCM watakifanya zaidi? sikioni ila tu, wana uchu wa madaraka na wana agenda za siri zinazoambatana na mfumo wa itikadi fulani, kwani si tumeona nyumba za ibada fulani huko sumbawanga zikiwapiga marufuku maumini wao eti kwa sababu tu wamempigia kura Kikwete na hivi juzi tumeona chama cha kisiasa kinachofata dini fulani mpaka kwenye jina lake kikiwatembelea chadema, na tunaona viongozi wangapi wadini fulani wakiiongoza chadema kwa sasa? na wabunge wangapi wa kutokea hukohuko?Tusidanganyane, ukweli uko wapi na "all roads leads to Rome".
Nadhani umelaaniwa sana ndugu
 
FF tatizo sio ****** ila mfumo mbovu ndio unaotuumiza, hilo la udini ni mtazamo wa wachache ndani ya ccm na hata ndani ya upinzani, ili tujikwamue hapa lazima kubadili mfumo na kama mfumo ungekuwa mzuri ****** angefanya mengi tu mazuri mathalani ni dhahiri ccm kinaendeshwa na cc ambayo inamwelekeza hata m/kiti wake hatua gani za kuchukua kwenye masuala muhimu ya nchi. Chukulia uzoefu wa bunge letu linapojadili mambo mazito ya kuikosoa na kuielekeza serikali kama chama kikiona kuna kuadhirika kwa baadhi ya watendaji wake wakuu kunafanyika kikao cha wabunge wa chama (ccm) ili kuweka msimamo wa pamoja ambao mara zote ni kuinusuru serikali na chama, ili tuweze kupiga hatua kwanza bunge linapaswa kuwa huru kabisa na chama kisiingilie wabunge katika utendaji wao wa kila siku na hili linapaswa kuwa kikatiba kwani laweza kutokea hata kwa chama kingine chochote na matokeo ni wananchi kuumia na nchi kudidimia kiuchumi, kwahiyo nikuhakikishie tu kwamba wananchi wanafedheheshwa na mfumo uliopo flani anadhihirika ni fisadi lakini kwakuwa kumgusa yeye kutaathiri wengine ndani ya mfumo inabidi aachwe
 
Tatizo lenu si CCM tatizo lenu ni Rais aliyeko madarakani, semeni kweli, kwani hao viongozi wenu wote, si walitokea CCM? walifanya nini walipokuwa huko? ambacho wakiwa nje ya CCM watakifanya zaidi? sikioni ila tu, wana uchu wa madaraka na wana agenda za siri zinazoambatana na mfumo wa itikadi fulani, kwani si tumeona nyumba za ibada fulani huko sumbawanga zikiwapiga marufuku maumini wao eti kwa sababu tu wamempigia kura Kikwete na hivi juzi tumeona chama cha kisiasa kinachofata dini fulani mpaka kwenye jina lake kikiwatembelea chadema, na tunaona viongozi wangapi wadini fulani wakiiongoza chadema kwa sasa? na wabunge wangapi wa kutokea hukohuko?Tusidanganyane, ukweli uko wapi na "all roads leads to Rome".
Baada ya JK kushindwa kabisa kuleta "maisha bora kwa kila Mtanzania" kama alivyoahidi amekimbilia hoja ya udini ili kujinusuru! Tunakumbuka JK alipoitwa kuwa ni "chaguo la Mungu" mwaka 2005 hakulalamikia kabisa "udini!" Amesahau kwamba hata Mkapa ilitolewa hoja kwamba kinga iondolewe ili ashtakiwe kwa ufisadi wake lakini hakukimbilia blanketi la "udini" ili kujifunika nalo! Vile vile akina Lowasa, Chenge, Anna Makinda, etc wameshambuliwa mno haijasikika kwamba wanalalamika kwamba eti dini zao zimewaponza! Ni Rais Kikwete pekee anayelialia Ikulu eti "anaonewa" kwa sababu ya dini yake! Anapoegemea kwenye dini yake JK akumbuke kwamba, pamoja na uchakachuaji wa kura alioufanya, hata Wakristo na watu wa dini nyingine walimchagua, asifikiri ni Waislamu tu! Yeye alitaka tumsifie kwa lipi huyu "Mtalii?" Anazurura tu kwenye nchi za watu na kusahau kutimiza ahadi zake tamu tamu! Hizi kauli zake za ajabu ajabu nazo zinatupa mashaka zaidi, hatuoni mwanga mbele, maana yake hana nia ya kuwatumikia Watanzania!
 
Back
Top Bottom