Moja ya Kauli za Kukatisha Tamaa za JK

Hivi hapa Tanzania ni asilimia ngapi ya watanzania wanatumia umeme? Lazima tujue kuwa tunapolifanya tatizo la umeme kuwa ni janga la Taifa tunawakosea wengine wenye matatizo makubwa zaidi ktk maswala ya Afya, Elimu na Usafiri.

Umeme bado kwa asilimia kubwa bado unategemea vyanzo vya maji hivyo jibu lake kwa short run solution yupo sawa maana wengi wanalaamu kwa wakati huu ila kwa long-run walisha sema ifikapo 2015 tatizo litakuwa historia. Tatizo lipo wapi hapo.
 
Mh. Ngambo Ngali, nielekeze huko unapoishi wanapo uza unga sh. 400 manake huku kwetu unga ni sh.700
 
Sioni cha kushangaza apo ndo uwezo wake wa kufikilia huo na pia kumbuka alishawai sema hajui why watz ni maskini
 
Huyu bwana aliwahi kusema asilaumiwe kwa swala la njaa AKASEMA" hata mimi naomba Mungu mvua inyeshe".
 
kwa long-run walisha sema ifikapo 2015 tatizo litakuwa historia. Tatizo lipo wapi hapo.
Hizi story za "mgawo kuwa historia" si ngeni! Mara ya kwanza tuliambiwa ni mpaka 2013, sasa hivi tunaambiwa ni mpaka 2015, baadaye tutaambiwa ni mpaka 2020! Kaaaaazi kweli kweli!
 
Na eti.....kuna wale wanaotarajia mtu kama huyu ajiuzulu kwa kukiri kushindwa! Kujiuzulu, kama mtu kujiua, kunataka ujasiri na akili!
 
Na eti.....kuna wale wanaotarajia mtu kama huyu ajiuzulu kwa kukiri kushindwa! Kujiuzulu, kama mtu kujiua, kunataka ujasiri na akili!
Tatizo la JK liko hivi: "HAJUI KWAMBA HAJUI!" Only that! Mengine yoote yanatokana na ukweli huo!
 
Kauli nyengine yenye utata aliyotoa akiwa saba saba ni pale aliposema 'hivi gari si huwa linaenda mbele na nyuma eh?"
 
Balali yupo mkuu, walizika sanamu lake. Bado mgao anapata wa Rada, meremeta, EPA, na wa Madini yetu, anaishi ulya km vile yuko peponi wakati cc tunaishi kwenye giza. naamini siku viboko vitakapo lipuka, wahuni wote watakoma wanao jiita magamba
mkuu pamoja sana good thinking.
 
Ni Raisi wa kwanza mwenye vituko asiyeguswa kabisa na maumivu na kilio cha wananchi tofauti kabisa na waliomtangulia japo walikuwa na mapungufu yao lakini waliwajali wananchi wao hata wakizungumza ungeona wanaumia ndani ya mioyo yao, lakini huyu ana roho ya chuma.

Alivyo na roho ya visasi usikute anatukomesha eti kwa sababu tumempunguzia umaarufu na tunaandamana kila siku
 
Wewe ulitegemea kauli gani kutoka kwa huyu mlugaluga? Kama hana uwezo wa kutatua matatizo yanayoikabili nchi kwanini asiachie ngazi waje wale ambao wana ubunifu wa kumaliza matatizo yetu? Yeye alipokuwa anagombea urais alifikiri ikulu anakwenda kucheza ngoma? Hao ndo CCM bwana chama cha magamba.
we kweli msema hovyo! Rais ni mlugaluga. Hii kali, mi nadhani nchi imemshinda
 
Jamani tumtendee haki JK, huo ndiyo upeo wake wa kufikiri. Ukweli ni kuwa kumtaka JK atoe jibu la matatizo ya nchi hii ni sawa na kumtaka ng'ombe dume atoe maziwa. Huyu mtu ni kilaza wa kutupa,msameheni bure.
 
Angekuwa siriaz angemaliza tatizo hili kwenyde awamu yake ya kwanza maana anauzoefu na wizara hii kwani alishawahi kuwa waziri wa nishati na madini na diye aliyeileta IPTL,Sasa hakuna sababu ya kumshangaa hana jipya!
 
hana maana hata kidogohuyu m.kwere........litegemea jibu kama hilo......maana hajui kwa tz ni maskini
 
.....Pamoja na kujiandaa kwa miaka 10 (1995-2005) kuwa Rais, bado binafsi simwoni JK kutosha kwenye kiti cha U-Rais! Masihara na majibu yake hayafanani kabisa na Kiongozi wa ngazi yake.
 
JK ni sawa na Maria Antoinnete wa France, nae alikuwa anawakatisha tamaa wananchi wake kwa kauli chafu na ufisadi hali iliyopelekea France revolution.

TZ revolution is coming soon we ngoja...
 
Buchanan, Habari ya siku? Ulikuwa Sabatical nini umekuwa kimya muda mrefu?

Tukirudi kwenye mada, jana nimeangalia taarifa ya habari saa mbili usiku,hakuna kipya na cha maana alichosema lakini watu wazima na akili zao wanakimbilia kutaka kugonga naye wakati wakirudi nyumbani Umeme hakuna na yeye kishasema hawezi kuwa wingu, nyama kilo 5000, kilo ya mchele 1600, unga 400, nauli 400 one trip. Hakuna hata mmoja kati ya wale waliokuwa wanakenua aliyeuliza mzigo huu mgongoni kwetu watanzania utaisha lini. Hakuna aliyeuliza maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi.

Hakuna aliyeuliza kasi zaidi ilikuwa ya kwenda wapi, nguvu zaidi zilikuwa za kufanyia nini na ari zaidi ilikuwa ya kufikia wapi? Na jee mpaka sasa tumekaribia huko tulikokuwa tunaenda kwa kasi na kwa nguvu?
Unga wa shs 400 unapatikana wapi mkuu nije kununua.. sie tunauziwa 6,00
 
KWA KAULI KAMA HII, HIVI VIONGOZI WA SERIKALI YA TANZANIA WAKO SERIOUS KUTATUA TATIZO LA UMEME KWELI????????

JK amkingia kifua Ngeleja
na Mwandishi wetu
RAIS Jakaya Kikwete, amemkingia kifua Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja, kuwa si chanzo cha mgawo wa umeme uliopo nchini hivi sasa.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja huku kukiwa na shinikizo kubwa la watu mbalimbali hapa nchini kumtaka Waziri Ngeleja kujiuzulu kwa kushindwa kulinusuru taifa na mgawo wa umeme unaotokea mara kwa mara.
Rais Kikweta alitoa kauli hiyo jana katika viwanja vya Maonyesho ya Sabasaba vilivyopo katika Barabara ya Kilwa, mara baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali za kupunguza mgawo wa umeme.
Akijibu swali hilo, Rais Kikwete alisema ni kweli tatizo la umeme linachangia kudorora kwa uzalishaji mali lakini ukosefu wa maji katika mabwawa yaliyopo kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme ndiyo sababu ya kuwapo kwa mgawo wa umeme.
Alisema kiini kikubwa cha tatizo la umeme ni ukame na si makusudi ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja au Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), William Mhando.
“Mtera maji hakuna. Hicho ndicho kiini cha tatizo. Tunachofanya tunatafuta nini badala ya umeme wa kutokana na maji. Ubungo kuna megawati za umeme 100, Tegeta megawati 45 na ifikapo Desemba, tutakuwa tumepata nyingine 100.
“Sina namna ya kugeuka kuwa wingu la mvua nikaenda kugeuza wingu kubwa la mvua pale Mtera,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa, pamoja na serikali kuwa na mkakati wa nishati mbadala ya umeme, jambo hilo si suala la kuzungumza asubuhi na kuupata jioni, lakini ifikapo mwisho wa mwaka huu, kutakuwa na megawati 300 za umeme.
Alibainisha kuwa katika kipindi hiki serikali imeagiza umeme wa kukodi kutoka Kampuni ya Aggreko na kwamba TANESCO imeshafanya mazungumzo na kampuni hiyo.
Aliongeza kuwa anaamini miaka mitatu ijayo tatizo la umeme litakuwa limekwisha na kutakuwa na megawati 3000 mpya.
Amesema kuwa, serikali inajitahidi kutafuta njia mbadala za kutatua tatizo la umeme, badala ya kutegemea ule wa nishati ya maji, na kwamba ifikapo 2015 kuwe na megawati 3000.
Upande mwingine alishauri wajasiriamali wanaopata nafasi ya kuonyesha na kuzitangaza biashara zao kwenye maonyesho hayo, ni vema wakatengewa maeneo maalum ili wawe wanafanya biashara zao kwa mwaka mzima.
 
Wewe ulitegemea kauli gani kutoka kwa huyu mlugaluga? Kama hana uwezo wa kutatua matatizo yanayoikabili nchi kwanini asiachie ngazi waje wale ambao wana ubunifu wa kumaliza matatizo yetu? Yeye alipokuwa anagombea urais alifikiri ikulu anakwenda kucheza ngoma?

Hiyo kauli haikutarajiwa kutoka kwa mkuu wa nchi. Wote tunajua kwamba yeye sio wingu la mvua, ni binadamu kama sisi. Lakini hii sio mara ya kwanza Bwawa la Mtera kupungukiwa na maji. Swali ni je yeye kama mkuu wa nchi ni kipi amekifanya kuhakikisha kwamba endapo Mtera itakauka turudi kwa plan B lakini huduma ya umeme iendelee kutolewa?. Haya masuala ya kutegemea nature ndio tuweze kuishi ilishapitwa na wakati ila kwa Tanzania bado tunakimbilia kulaumu "hali ya hewa".

Tiba
 
Back
Top Bottom