Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mohamed Said ana siasa za kulialia

Dira...
Hakuna mtafiti anaeweza kuandika historia ya TANU kuanzia African Association, TAA, TANU na uhuru wa Tanganyika au historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere asitaje ukoo wa Sykes.ea

Chuo Cha CCM Kivukoni walidhani kama wanaweza kuandika historia ya TANU kwa kumkwepa Abdul Sykes.

Balaa lake likaja kuwa kubwa sana.
Ndiyo tuko hapa leo tunaisoma historia ya TANU upya.

Nakuwekea link hapo chini ya makala niliyoandika miaka mingi iliyopita baada ya mtu kughadhibishwa na mimi kila ninapoandika historia ya AA, TAA, TANU, uhuru wa Tanganyika na Mwalimu Nyerere lazima ukoo wa Sykes niutaje.

Ikutoshe tu kuwa Kleist Sykes yuko katika Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press, 2011.

Nilialikwa Northwestern University, Chicago kumzungumza Abdul Sykes.
Hiki chuo ndicho kinaongoza ulimwenguni katika African History.

Kitabu cha Abdul Sykes kimebadili historia nzima ya Tanganyika.
Hakika kisa cha akina Sykes ni kisa mimi kimenikamata sana.

Achilia ule udugu lakini siku niliposoma kitabu, ''Modern Tanzanians,'' kitabu alichohariri John Iliffe na kusoma, ''The Townsman: The Life of Kleist Sykes,'' sura iliyoandikwa na mjukuu wa Kleist Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes Buruku historia hii ilikamata fikra zangu (Modern Tanzanians, (ed), East African Publishing House, Nairobi, 1973).

Nakumbuka kama vile jana nilikuwa katika Maktaba ya Taifa, Arusha ndipo nilipokikuta kitabu hiki.

Utafiti wangu wa kutaka kujua mengi ulianza siku ile.
Nikawauliza hawa ndugu zangu juu ya kitabu cha Iliffe.

Wakanifahamisha kuwa babu yao, Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 alikuwa ameandika ''kitabu,'' ambacho alimwachia mwanae Abdul Sykes.

Kwa hakika hakikuwa kitabu bali mswada wa kitabu.

Mwanae Abdu Sykes, Daisy alipoingia Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki mwaka wa 1967 kusoma Elimu na Historia ndipo alipokutana na John Iliffe na huyu mwalimu wake baada ya kufahamu historia ya akina Sykes na yeye kama mimi akakumbwa na hii ''obsession,'' akataka kujua mengi vipi walifika Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini.

Hapo ndipo Daisy akawa anachukua nyaraka zilizokuwa katika familia na kumuonyesha Iliffe pamoja na mswada wa kitabu alichoandika babu yake.

Kutokana na nyaraka hizi Iliffe akaandika paper hii: '‘The Role of the African Association in the formation and Realisation of Territorial Conciousness in
Tanzania.’ Mimeo, Universityof East Africa Social Sciences Conference,'' 1968.
'
Iliffe kapatwa na homa ya ''obsession,'' ya akina Sykes anataka kujua mengi zaidi Daisy akipewa ''assignment,'' anakwenda kwa baba yake anauliza anapewa maelezo na ushahidi wa nyaraka.

Iliffe kila akielezwa hili ndani linazuka jingine akataka kujua ilikuwaje Abdul Sykes akawa General Secretary wa Dar es Salaam Dockworkers Union mwaka wa 1948.

Iliffe akapewa maelezo na nyaraka akaandika paper hii:‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’ TNR, Dar es Salaam, 71, 1970.

Iliffe kama mimi miaka mingi baadae akawa Sykes, Sykes na Sykes.

Sijui kwa nini Iliffe hakuandika historia ya TANU kwa ukamilifu wake wala hakuwa na shauku ya kukutana na Abdul Sykes, baba wa mwanafunzi wake hodari Aisha ''Daisy,' Sykes ambae kamsaidia sana kuijua historia ya African Association na TANU.

Mohamed Said na yeye kwa kumsoma Iliffe gonjwa la Sykes likamkumba.

Mimi nikaamua kufanya kile Iliffe hakufanya nacho ni kuandika maisha ya Abdul Sykes lakini nikaamua pia kuweka mguu wangu pale unyayo wa Iliffe ulipokanyaga.

Hapa ndipo ilipoaanza safari yangu iliyonifikisha hadi Imhambane kijiji kinachoitwa Kwa Likunyi alipotoka Sykes Mbuwane kuelekea Laurenco Marquis akiwa ameongozana na Chief Mohosh na Wazulu wengine kupanda manowari ya Wajerumani kuja Pangani kuanza vita na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa mwishoni mwa miaka ya 1880.

Huyu Chief Mohosh ndiye akaja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika akiwa mkuu wa Germany Constabulary.

Prof. Emmanuel Achiempong wa Harvard na yeye gonjwa la Sykes likamkumba akaniandikia mwaka wa 2008 kuniomba anijumuishe katika mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) anataka niandike mchango wa Kleist Sykes katika historia ya Afrika.

Mradi huu ulijumisha waandishi na watafiti takriban 500 kutoka kila pembe ya dunia.

Oxford University Press, New York wamechapa volumes sita ya kazi hii.

Bwana Ndjabu,
Yako mengi lakini kwa leo tuuishie hapa sitaki kuwachosha wasomaji.

NB:
Mwaka wa 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika serikali ikaamua kutunuku Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa Ally na Abdul Sykes kwa kutambua mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Katika kitabu hicho hapo chini sura moja, ''Kleist Sykes the Townsman,'' (1894 - 1949) imeandikwa na Daisy Sykes Buruku (Aisha Abdul Sykes) inaeleza maisha ya babu yake.

Hii ni rejea muhimu katika kuielewa historia ya Tanganyika.

1639537119321.png
 
Nadhani hujumuekewa vizuri aliongelea kuhusu wapigania uhuru wa mwanzoni wa Taifa hili kutoandikwa kwenye historia ya Nchi .Lakini pia huyu Mzee sometimes ni mbaguzi Sana wa kidini hafai kwenye jamii ya watu waloelimika na kustalabika .Anapenda Sana dini yake kuliko uhalisia ulivo

Sent using Jamii Forums mobile app
kwahyo wewe kwa akili yako wapigania uhuru walikuwa hawa akina Nyerere na wazee wa Dar tu? akina Kinjikitile Mkwawa au Mangi Sina walikuwa wanacheza mduara. ukijiita mwana historia unatakiwa uje na historia ya watu wa nchi hii na tawala zao tamaduni za kabla ya kuja mzungu mpaka anakuja na mpaka anaondoka. we unakuja na historia ya akina Nyerere nan kakwambia wao ndio walioanzisha mapambano ya uhuru? au jesh la mlugaluga kule Tabora lilikuwa la nini. bure kabira.
 
Rubbish!!!

Then mkishakuwa mpo wengi kuna siku wingi wenu utakuletea kula mezani kwako eti?au kukusomeshea watoto wako wapate nao elimu nzuri kama watoto wa watawala wanaokutawala?sijui kama unajitambua.
Aah aahh aaaahhh,
Nilikua namjibu alieanza mkuu,
Sijui nae umemkemea au unanionea mimi tu
Jaribu kupitia kwanza
Kuna aliyeanza hayo madai
 
Nilikuwa nasikiliza kipindi cha maoni kinachorushwa na DW, ndipo nikamsikia huyu mtu anaitwa Mohamed Said akitoa maoni yake kuhusu miaka 60 ya uhuru, ingawa kabla nimewahi kusoma makala zake kadhaa, sikufikiri kwamba kwa ukubwa wa changamoto tulizonazo leo pamoja na mabadiliko makubwa ya kielimu na kimfumo bado atakuwa na mawazo kwamba waisilam wanabaguliwa.

Ninapata shida kumwelewa kwa sababu kwa taifa letu lilipofikia ningeweza kusema kama ni ubaguzi unaopaswa kupambana nao ni ule unaopendelea chama tawala.

Ubaguzi anaosema waisilam wanabaguliwa ni wa kufikirika sana. Sijui kama huyu ndugu amefanya utafiti kujua wakristo na waisilam wanaosota na kubaguliwa kwa sababu wao sio CCM!!.

Akiwa anasema hayo wapo viongozi wa kiisilam wengi tu wanaoshiriki uharamia wa kuwabagua ndugu zao ilimradi tu sio CCM.

Nashauri aache mambo ya kukaririshwa kwamba waisilam wanaonewa hizo hoja zilishapitwa na wakati. Isitosha zinafanya waisilam waonekane wanyonge na watu wa kuhurumiwahurumiwa tu.
Hakika ni mawazo ya kijihadist ambayo yamepitwa na wakati. Siku hizi tanzania ukiona waislamu wenye hii mambo ya kukandamizwa au kubaguliwa kwa uhakika wanatafuta upendeleo kuteuliwa.
Majuzijuzi tumeona watu wakimtolea mama orodha ya wakurugenzi mashirika ya umma kwenye mitandao kuonesha wakristo wangapi na waislamu wangapi. Namna yoyote ya kusawazisha bila kuona weledi na uadilifu na uzalendo ni jambo la kijinga.
Tumeshaona waziri mmoja mwenye rekodi nzuri sana wa nishati akiondolewa na kuwekwa mtu anayetiliwa mashaka utendaji wake na watu wengi. Hakuna sababu yoyote imetolewa hadi sasa kwa nini dr menard kalemani ameondolewa.
 
Dira...
Hakuna mtafiti anaeweza kuandika historia ya TANU kuanzia African Association, TAA, TANU na uhuru wa Tanganyika au historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere asitaje ukoo wa Sykes.

Chuo Cha CCM Kivukoni walidhani kama wanaweza kuandika historia ya TANU kwa kumkwepa Abdul Sykes.

Balaa lake likaja kuwa kubwa sana.
Ndiyo tuko hapa leo tunaisoma historia ya TANU upya.

Nakuwekea link hapo chini ya makala niliyoandika miaka mingi iliyopita baada ya mtu kughadhibishwa na mimi kila ninapoandika historia ya AA, TAA, TANU, uhuru wa Tanganyika na Mwalimu Nyerere lazima ukoo wa Sykes niutaje.

Ikutoshe tu kuwa Kleist Sykes yuko katika Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press, 2011.

Nilialikwa Northwestern University, Chicago kumzungumza Abdul Sykes.
Hiki chuo ndicho kinaongoza ulimwenguni katika African History.

Kitabu cha Abdul Sykes kimebadili historia nzima ya Tanganyika.
Mzee usipate taabu kunielewesha kwasababu mimi nimeamua kupuuza fikra zako za udini.
 
Rhz,
Katika post yangu # 63 nimesema atakae kujua tatizo kama nilivyolieleza kwa ushahidi asome Part Three ya kitabu cha Abdul Sykes.

Hili jambo si la kulifanyia haraka.

Muhimu usome kwanza historia ya Tanganyika kuanzia harakati za uhuru hadi uhuru ulipopatikana na baadae.

Ukija na maswali ilhai hulijui tatizo hatuwezi kujadili.
Sasa Mzee@Mohamed said nani asiye jua historia ya nchi yenu ilipotoshwa maksudi kbs na kikudi cha watu wachache
Mara kadhaaa hata wanasiasa wanalisema hilo,mfano mwaka 2014 tundu lissu akiwa visiwan pemba kwny mkutano na wana cuf alieleza ni kwajinsi gani historia ya uhuru wa tanganyika ilivyo jaa uongo.

Lakn turudi kwny hoja
Nataka unijibu hoja zangu 6. Hapo juu Kwanza,kuhusu kusoma vitabu vyako hilo tuliweke pembeni kwanza kwasababu Nilisha soma sana machapisho yako kweny blog yako,pia hapa Jf.na kwakutoa tu sammary ya machapisho Mengi unaongelea dhulma kwa waislam waliopigiania uhuru na waislam wasasa wanavyo teswa na mfumo huu.

Sasa bs jibu hoja zangu 6 halafu tuendelee vizuri.
Mzee Mohamed Said karib.
 
Rhz...
Huwezi kujadili kitu usichokijua.
Lijue somo lenyewe kisha ndiyo ufanye mjadala.
 
kwahyo wewe kwa akili yako wapigania uhuru walikuwa hawa akina Nyerere na wazee wa Dar tu? akina Kinjikitile Mkwawa au Mangi Sina walikuwa wanacheza mduara. ukijiita mwana historia unatakiwa uje na historia ya watu wa nchi hii na tawala zao tamaduni za kabla ya kuja mzungu mpaka anakuja na mpaka anaondoka. we unakuja na historia ya akina Nyerere nan kakwambia wao ndio walioanzisha mapambano ya uhuru? au jesh la mlugaluga kule Tabora lilikuwa la nini. bure kabira.
Kitali,
Soma kitabu changu, "Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama," uone vipi nimemueleza Mangi Sina.

Screenshot_20211215-010335_Photos.jpg
 
Hakika kisa cha akina Sykes ni kisa mimi kimenikamata sana.

Achilia ule udugu lakini siku niliposoma kitabu, ''Modern Tanzanians,'' kitabu alichohariri John Iliffe na kusoma, ''The Townsman: The Life of Kleist Sykes,'' sura iliyoandikwa na mjukuu wa Kleist Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes Buruku historia hii ilikamata fikra zangu (Modern Tanzanians, (ed), East African Publishing House, Nairobi, 1973).

Nakumbuka kama vile jana nilikuwa katika Maktaba ya Taifa, Arusha ndipo nilipokikuta kitabu hiki.

Utafiti wangu wa kutaka kujua mengi ulianza siku ile.
Nikawauliza hawa ndugu zangu juu ya kitabu cha Iliffe.

Wakanifahamisha kuwa babu yao, Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 alikuwa ameandika ''kitabu,'' ambacho alimwachia mwanae Abdul Sykes.

Kwa hakika hakikuwa kitabu bali mswada wa kitabu.

Mwanae Abdu Sykes, Daisy alipoingia Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki mwaka wa 1967 kusoma Elimu na Historia ndipo alipokutana na John Iliffe na huyu mwalimu wake baada ya kufahamu historia ya akina Sykes na yeye kama mimi akakumbwa na hii ''obsession,'' akataka kujua mengi vipi walifika Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini.

Hapo ndipo Daisy akawa anachukua nyaraka zilizokuwa katika familia na kumuonyesha Iliffe pamoja na mswada wa kitabu alichoandika babu yake.

Kutokana na nyaraka hizi Iliffe akaandika paper hii: '‘The Role of the African Association in the formation and Realisation of Territorial Conciousness in
Tanzania.’ Mimeo, Universityof East Africa Social Sciences Conference,'' 1968.
'
Iliffe kapatwa na homa ya ''obsession,'' ya akina Sykes anataka kujua mengi zaidi Daisy akipewa ''assignment,'' anakwenda kwa baba yake anauliza anapewa maelezo na ushahidi wa nyaraka.

Iliffe kila akielezwa hili ndani linazuka jingine akataka kujua ilikuwaje Abdul Sykes akawa General Secretary wa Dar es Salaam Dockworkers Union mwaka wa 1948.

Iliffe akapewa maelezo na nyaraka akaandika paper hii:‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’ TNR, Dar es Salaam, 71, 1970.

Iliffe kama mimi miaka mingi baadae akawa Sykes, Sykes na Sykes.

Sijui kwa nini Iliffe hakuandika historia ya TANU kwa ukamilifu wake wala hakuwa na shauku ya kukutana na Abdul Sykes, baba wa mwanafunzi wake hodari Aisha ''Daisy,' Sykes ambae kamsaidia sana kuijua historia ya African Association na TANU.

Mohamed Said na yeye kwa kumsoma Iliffe gonjwa la Sykes likamkumba.

Mimi nikaamua kufanya kile Iliffe hakufanya nacho ni kuandika maisha ya Abdul Sykes lakini nikaamua pia kuweka mguu wangu pale unyayo wa Iliffe ulipokanyaga.

Hapa ndipo ilipoaanza safari yangu iliyonifikisha hadi Imhambane kijiji kinachoitwa Kwa Likunyi alipotoka Sykes Mbuwane kuelekea Laurenco Marquis akiwa ameongozana na Chief Mohosh na Wazulu wengine kupanda manowari ya Wajerumani kuja Pangani kuanza vita na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa mwishoni mwa miaka ya 1880.

Huyu Chief Mohosh ndiye akaja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika akiwa mkuu wa Germany Constabulary.

Prof. Emmanuel Achiempong wa Harvard na yeye gonjwa la Sykes likamkumba akaniandikia mwaka wa 2008 kuniomba anijumuishe katika mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) anataka niandike mchango wa Kleist Sykes katika historia ya Afrika.

Mradi huu ulijumisha waandishi na watafiti takriban 500 kutoka kila pembe ya dunia.

Oxford University Press, New York wamechapa volumes sita ya kazi hii.

Bwana Ndjabu,
Yako mengi lakini kwa leo tuuishie hapa sitaki kuwachosha wasomaji.

NB:
Mwaka wa 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika serikali ikaamua kutunuku Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa Ally na Abdul Sykes kwa kutambua mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Suala sio ally na abdul ishu wewe kutengeneza hisia na chuki za kidini kwa maamuma.
Na ingekuwa hatuna misingi mizuri wewe mze ungekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

Sema kauli zako unazificha ficha sio kama yule mzee Ilunga yeye chuki zilikuwa za wazi akitangaza hadi wakristo wauwawe.
Na alikuwa rafiku yako
 
Rhz...
Huwezi kujadili kitu usichokijua.

Lijue somo lenyewe kisha ndiyo ufanye mjadala.
Sawa mzee Mohamed Said sikutaka mjadala uwe mrefu wala mjadala uwe mpana Sana,nilitaka unijibu kwanza hoja zangu 6 ili nijue ww ni mtu wa aina gani,lakin kinacho nisikitisha zaid bado unakwepa hoja zangu kama uLivyo fanya DW.
 
Ni kweli WaIslam wanabaguliwa sana ndio maana.

Rais wa JMT ni mgalatia
Waziri Mkuu ni Mgalatia
Rais wa Zanzibar ni Mgalatia
Jaji Mkuu ni Mgalatia
Jaji Kiongozi Mgalatia
Umemsahau ustaadh sheikh ubwabwa wa Dar anayeamini Magufuli Ni zaidi ya mtume (maneno yake mwenyewe)
 
Back
Top Bottom