Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mohamed Said ana siasa za kulialia

"TANESCO huwa ni chaka la kupiga pesa wakubwa"

Hii ni hoja ya msingi sana ya kuijadili kupita hiyo mada ya Mzee saidi,
Nadhani nia ya huyo mzee ni kuuza vitabu vyake tu. Na hasa apate soko toka kwa Waislam.
Che...
Ni vigumu sana kufanya mjadala na mimi.
Wengi hushindwa haraka.
 
Umefika wakati Mwamedi abadilike. Utu, utaifa ni muhimu zaidi kuliko tofauti za dini zetu
Sarri,
Tuwe waungwana lau kidogo ili tufanye mjadala wenye tija.

Acha maskhara.

Unapokwenda nje ya mjadala na kunipa majina unaondoa umakini wako katika mjadala wewe unageuka kuwa kichekesho.

"Mwamedi."

Unakusudia kumfanya nani kuwa kichekesho?
 
Mkristu pekee huyu mzee anaemkubali sharti asiwe mtanzania labda wa Mzungu au wa mataifa ya kiafrika .

Watu kama hawa ni sumu kwa Taifa .

Mimi Rafiki zangu wengi sana waislamu na nashirikiana nao safi kabisa katika maisha .

Lakini watu wa dizaini hii hatari mzee anaweza kukuchoma hivi hivi kisa wewe ni dini tofauti na yeye!!?

Dini zenyewe tumeletewa lakini twajifaya tunazijua zaidi ya hao waliotuletea ,ya shangaza sana na kuogopesha!!![emoji15]
The imp,
Naona mjadala umemalizika mapema.

Nimeandika mambo muhimu lakini hayajadiliwi.

Mimi sijaleta hapa dini.
Nimeleta suala la ubaguzi.
 
Wamanyema kujifanya waarabu
Hah hah ni kweli mkuu Wamanyema hupenda sana uarabu, miaka ya nyuma nilikuwa nakaa karibu na bibi mtu mzima Mmanyema,huyu bibi aliolewa na Muarabu na pia mwishoni akaja olewa na Mzaramo kwa hiyo kwenye familia yake alikuwa na watoto wenye damu ya Kiarabu na wengine weusi tii bahati mbaya au nzuri wale wenye asili ya Uarabu maisha yao yalikuwa mazuri sana na hawa weusi tu wakawa kama wasindikazji tu basi bibi anapoongea utamsikii akisema sisi Waarabu, nikawa nabaki nashangaa, huyo bibi yeye alikuwa Mmanyema na mume wake Muarabu alikuwa keshafariki na ndio akaolewa na Mzaramo, kwanini akawa anajiita sisi Waarabu, kila akiongea utasikia sisi Waarabu hadi ikawa inakuwa kero.
 
Mfia...
Mjadala haupo tena tunazungumza mengine.

Metal mada hii hakujua kuwa kichwa alichoweka akidhani kitanimaliza ndicho kilichoita wasomaji.

Nilipoingia tu wasomaji wamefika 2000 hiyo ni kati ya Maghrib na Isha.

Hivi sasa wasomaji wamefika 3345 and counting...

Neno "kulialia," na kuwa Mohamed, "anadhalilisha Uislam," ndiyo mtego uliomnasa yeye mwenyewe.

Kuna watu hapa hawachangii chochote lakini huja kunisoma tu.

Hawa wanapenda yale niandikayo.

Laiti mleta hii mada angefahamu angekaa kimya.

Nilijua hana uwezo wa kufanya mjadala na mimi toka asubuhi.

Natoa mtihani kidogo.

Pitieni ninayoandika mimi na yaandikwayo na wengine na fanyeni tathmini ya mantiki ya hoja hata na uandishi jibu utalipata.
 
Mkuu Mohamed Said.

Nafikiri mtoa mada anazungumzia "kulia lia" kutokana na kusoma baadhi ya mabandiko yako huku jukwaani na kupitia mahojiano yako kadhaa hasa hiyo idhaa ya DW!

Je ni kweli kwamba mtizamo wako bado ni huo kwamba waislam wanabaguliwa?
 
Rhz...
Ungesoma kwanza kama nilivyokushauri hakuna haja ya kukimbilia kufanya mjadala ilhali hulijui somo lenyewe.

Huwezi kusoma basi sikulazimishi.
Mzeee Mohamed Said Nimeshalisema huko juu makala zako nyingi kuhuru historia ya uhuru wa tanganyika nimezisoma sana.

Naomba kama kuna majibu ya maswali yangu 6 kweny hivyo vitabu vyako uweke hapa kwa faida ya wengine wasiopenda kusoma vitabu.
Halafu kwann unanilazimisha kusoma vitabu vyako? Na dhamira kubwa kweny vitabu vyako inajulijana wazi ni kusahaulika kwa waislam wapigania uhuru.

Pia unaposema Nisome vitabu vyako huoni hiyo ni njia ya kukwepa maswali yangu,kwasababu hapa hatujadili vitabu vyako! Hapa tunajadili kile ulichokuwa unakisema DW.
 
a4a...
Hayo uliyoleta hapa si hoja iliyoletwa hapa dhidi yangu nami nikaja kuijibu.
Ndani ya hoja huzaliwa hoja Mkuu, Si jambo baya. Umesema ni lazima tujue mizizi ya matatizo, tuijue historia sahihi.

Sasa ili tusiwe Bias na tujenge integrity ya madai yetu, Unaonaje tukaanza mbali zaidi kujuta Hata hao Waislamu na wenzao walitokeaje Tanzania? Ni lazima tujue ili Tupate uhalali wam madai
 
Mkuu Mohamed Said.

Nafikiri mtoa mada anazungumzia "kulia lia" kutokana na kusoma baadhi ya mabandiko yako huku jukwaani na kupitia mahojiano yako kadhaa hasa hiyo idhaa ya DW!

Je ni kweli kwamba mtizamo wako bado ni huo kwamba waislam wanabaguliwa?
Tod...
Hilo neno kulialia ni kebehi.

Mtoa mada kuleta mada nzito lakini ananikebehi.

Laiti ungesoma post zangu za nyuma katika mjadala huu usingeniuliza swali hili.

Hatuko makini.
 
Mzeee Mohamed Said Nimeshalisema huko juu makala zako nyingi kuhuru historia ya uhuru wa tanganyika nimezisoma sana.

Naomba kama kuna majibu ya maswali yangu 6 kweny hivyo vitabu vyako uweke hapa kwa faida ya wengine wasiopenda kusoma vitabu.
Halafu kwann unanilazimisha kusoma vitabu vyako? Na dhamira kubwa kweny vitabu vyako inajulijana wazi ni kusahaulika kwa waislam wapigania uhuru.

Pia unaposema Nisome vitabu vyako huoni hiyo ni njia ya kukwepa maswali yangu,kwasababu hapa hatujadili vitabu vyako! Hapa tunajadili kile ulichokuwa unakisema DW.
Rhz...
Mimi nikwepe maswali yako wewe.
Sijakulazimisha kusoma wala si vitabu vyangu ila kitabu kimoja tu cha Abdul Sykes na nimeeleza kuna nini Part One hadi Part Three.

Huwezi kusoma basi hakuna tatizo.
Huu ni mjadala huwezi kusoma rejea za kukueleza yaliyomo ndani ya somo unaona kwako muhimu kuuliza maswali ujibiwe sawa.

Kama wapo hapa wanaokijua kitabu kinasema nini watakujuza.
 
Kilembwe,
Nakuwekea hapo chini link ya hotuba ya Kitwaba Selemani Kondo Bungeni Dodoma akieleza tatizo la ubaguzi katika elimu.

Ingia katika link hiyo hapo chini:
Kilembwe,
Nakuwekea hapo chini link ya hotuba ya Kitwaba Selemani Kondo Bungeni Dodoma akieleza tatizo la ubaguzi katika elimu.

Ingia katika link hiyo hapo chini:
Mzee wangu Mohamed nakusalimu na ninakushukuru kwa hotuba uliyonitumia ambayo na imani kuwa kuna wengine pia wamepata wasaa wa kuisoma hotuba ile iliyotolewa na al marhum Kitwana Kondo mwaka wa 1999; Mzee Mohamed ukisoma malalamiko ya Marehemu Mzee Kitwana Kondo mengi yameisha fanyiwa kazi...hili la kufeli watoto wa kiislam kama ulivyoliweka Marehemu Prof Kighoma Ali Malima alilipatia dawa likapona....hilo la waislam wengi kuwa gerezani kwanza halina ushahidi....pili huenda Kitwana Kondo aliangalia majina ya wafungwa na jina sio uthibitisho wa dini, lakini hata kama ni kweli kwa hivyo waachwe wavunje sheria za nchi kisa waislam!? Tufike mahali tujivunie mafanikio yetu kama waislam kama watanzania.....
 
Wacha roho mbaya yako kwani umelazimishwa wewe kununua kitabu
Roho mbaya gani sasa.
Mzee angeandika tu kuhusu historia ya nchi mimi ningefikiria kununua kitabu chake.
Huwa sijishughurishi na vitabu vyenye mtizamo wa kidini hasa vinavyo taka kuleta taharuki za kidini.
Lazima tuthamini umoja na msikamano wetu ambao uliasisiwa na wazee wetu.
 
Mimi nazungumzia tatizo lile la wanafunzi wale waliofanya mtihani ule.

Hayo mengine ya wafungwa sikuyagusa.
Unasema hilo tatizo limefanyiwa kazi.

Je, una ushahidi?

Hii mosi pili ningependa kujua kilitokea nini ikawa wachache waliofanya mtihani ule ndiyo wengi waliopasishwa na wale wengi hawakuendelea na masomo?
 
Mimi sina utaalamu wa dini.

Kitabu cha Abdul Sykes ni Political History ya Tanganyika.

Kimefanyiwa review tatu zote zimechapwa katika Cambridge Journal of African History.

Nadhani umeelewa.
Unazungumzia umoja.

Kitabu kinaeleza Julius Nyerere alivyopokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes 1952.

Vipi alitiwa katika uongozi wa TAA na TANU na vipi aliungwa mkono na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Kote huko Nyerere akipelekwa na Abdul Sykes.

Kitabu kinaeleza vipi Wamishionari walivyomtaka achague ualimu au siasa.

Hiki ndicho kitabu cha Abdul Sykes ambacho kishatoka matoleo manne hadi sasa.

Nyerere akaacha kazi akaja kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes na vipi kipindi hicho Abdul alivyokitumia kumjengea Nyerere urafiki na watu mashuhuri Dar-es-Salaam kama Mshume Kiyate, Shariff Abdallah Omar Attas na mkewe Bi. Chiku bint Said Kisusa nk. nk.

Hiki ndicho kipindi baba yangu ingawa hakuwa mwanasiasa alikuja kumjua Nyerere kupitia kwa Abdul Sykes pale nyumbani kwake Stanley Street, Kariakoo.

Huu ndiyo umoja na mshikamano uliotengenezwa na wazee wetu.

Baada ya uhuru kupatikana ndipo hali ikabadilika na historia ya TANU ilipoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni wazee wangu wote wakafutwa kwenye historia hiyo.

Hiyo picha imepigwa February 1955 uwanja wa ndege safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO.

Hao akina mama ndiyo wazee wangu mie wanamsindikiza Mwalimu na jana yake palifanyika dua kubwa kumuombea Mwalimu salama katika safari yake na ikafanyika dhifa katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika),

Kulia ndiye Bi. Chiku bint Said Kisusa mke wa Shariff Abdallah Omar Attas, Bi. Titi Mohamed kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee na Baba wa Taifa yuko katikati.

Screenshot_20211215-144040_Facebook.jpg
 
Che...
Ni vigumu sana kufanya mjadala na mimi.
Wengi hushindwa haraka.
Mijadala yenye mlengo wa kuleta taharuki za kidini huwa sioni umuhimu sana kuijadili.

Labda kama inatoa suluhusho kwa makosa yalifanyika huko nyuma na wazee wetu.

Yaani ilenge kujadili ni namna gani jamii yetu ya sasa iende bila kuegemea upendeleo kwenye masuala ya Ustawi wa jamii nzima

Kwakuwa mimi kama mimi sikuhusika kwa namna yoyote ile kuhusu kuikandamiza jamii flani na sio kipaumbele changu.

(Je na tufanye nini sasa kurekebisha palipo haribika ?)

Hapo nitaweza kutoa maoni yangu.
 
Kilembwe,
Mimi nazungumzia tatizo lile la wanafunzi wale waliofanya mtihani ule.

Hayo mengine ya wafungwa sikuyagusa.
Unasema hilo tatizo limefanyiwa kazi.

Je, una ushahidi?

Hii mosi pili ningependa kujua kilitokea nini ikawa wachache waliofanya mtihani ule ndiyo wengi waliopasishwa na wale wengi hawakuendelea na masomo?
Mzee wangu Mohamed Said nakumbuka hili la wanafunzi wa kiislam kufeli Hayati Prof Kighoma alibadili mfumo kutoka ule wa kuandika majina kwenye karatasi za mtihani wa mwisho wa darasa la saba na kuleta mfumo wa kuandika namba napengine mfumo huu ulikuwa kabla hata ya 1999...kwa ukweli sina ushahidi wowote ninachoamini kuwa lilifanyiwa kazi ni kuona matokeo ya ufaulau kwa miaka hii ya sasa... nini kilitokea kwa kweli sijui...
 
Rhz...
Mimi nikwepe maswali yako wewe.
Sijakulazimisha kusoma wala si vitabu vyangu ila kitabu kimoja tu cha Abdul Sykes na nimeeleza kuna nini Part One hadi Part Three.

Huwezi kusoma basi hakuna tatizo.
Huu ni mjadala huwezi kusoma rejea za kukueleza yaliyomo ndani ya somo unaona kwako muhimu kuuliza maswali ujibiwe sawa.

Kama wapo hapa wanaokijua kitabu kinasema nini watakujuza.
Mzee Mohamed Said kwaheshima yako naomba tuishie hapa.
Lkn tambua mimi sipingi dhulma kwa waislam wa tanganyika,hilo lipo wazi waislam wanavyo baguliwa na viongozi wa kiserikali tangu uhuru wenu.
Hata rafiki yako marehem ilunga hassan alilizungumza sana enzi za uhai wake
 
Mzee wangu Mohamed Said nakumbuka hili la wanafunzi wa kiislam kufeli Hayati Prof Kighoma alibadili mfumo kutoka ule wa kuandika majina kwenye karatasi za mtihani wa mwisho wa darasa la saba na kuleta mfumo wa kuandika namba napengine mfumo huu ulikuwa kabla hata ya 1999...kwa ukweli sina ushahidi wowote ninachoamini kuwa lilifanyiwa kazi ni kuona matokeo ya ufaulau kwa miaka hii ya sasa... nini kilitokea kwa kweli sijui...
Kilembwe,
Ukiwa huna ujuzi na kitu unawauliza wenye kujua.

Hukimbilii kujibu.

Hayo ya Prof. Malima ni mwaka wa 1987 haya ya Kitwana Kondo ni 1999.
 
Kilembwe,
Ukiwa huna ujuzi na kitu unawauliza wenye kujua.

Hukimbilii kujibu.

Hayo ya Prof. Malima ni mwaka wa 1987 haya ya Kitwana Kondo ni 1999.
Nitachukua ushauri wako Mzee wangu Mohamed..pia nashukuru kwa kuweka sawa rekodi juu ya maamuzi ya Prof Kighoma, lakini bado nasisitiza kuwa kama bado kuna dhulma sio wakati sasa wa kulalamika ni wakati wa kufanyia kazi mapungufu yetu kama waislam na kujiondoa kwenye huu "unyonge" wa "kudhulumiwa" kama kweli bado upo! Unafikiri wakristo hawatendewi haya...wanapambana na masahibu haya haya ila nadhani wao wamejifunza kupambana nao kimya kimya....adui yetu sote twamjua..
 
Back
Top Bottom