Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mohamed Said ana siasa za kulialia

Suala sio ally na abdul ishu wewe kutengeneza hisia na chuki za kidini kwa maamuma.
Na ingekuwa hatuna misingi mizuri wewe mze ungekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani.

Sema kauli zako unazificha ficha sio kama yule mzee Ilunga yeye chuki zilikuwa za wazi akitangaza hadi wakristo wauwawe.
Na alikuwa rafiku yako
Inside,
Ilunga ni ndugu yangu si rafiki yangu.

Nimeanza kuandika nikiwa na umri mdogo sana labda miaka 25 hivi na sasa mii ni mzee nakimbilia miaka 70.

Kalamu yangu haijasabsbisha hayo unayosema na ingelikuwa hivyo publishers, yaani wachapa vitabu wangenikwepa.

Kinyume chake nimechapa vitabu vyangu na wachapaji wakubwa duniani kama Oxford Univeristy Press (OUP) na nimo katika orodha ya waandishi kutoka Afrika.

1639537835522.png
 
Alipaswa kuelewa tatizo la Nchi hii ni Mkoloni mweusi CCM.

Akishang'olewa huyu Mkoloni hapo sasa aje na hoja zake .
 
Mzee mdini huyo msimwendekeze kabisa.
Sisi Watanzania tunapendana bila kujali itikadi zetu.
Na kamwe hawezi kutufarakanisha na chichoko zake.
Aendea akaishi Afghanistani huko kwenye Sharia za Kiislamu zisizo nyanyasa Waislamu.
Ni wa kumpuuza tu.
Che...
Si rahisi mtu kunipuuza na sababu ni kile ninachoandika.
Umeshindwa kujibu hoja sasa unanishambulia mimi.

Ingekuwa kweli tunapendana yasingetokea yote ambayo yametokea toka uhuru upatikane.

Labda unasema hivyo kwa kutojua historia.

Ndiyo mwanzo kabisa nikasema ikiwa mtu anataka kujadili hili tatizo la ubaguzi kwanza asome kitabu cha Abdul Sykes ajue kimesema nini vinginevyo ndiyo hivi.

Mimi sijaandika kuhusu sharia.
Hoja yangu iko wazi na si ya leo.
 
Sawa mzee Mohamed Said sikutaka mjadala uwe mrefu wala mjadala uwe mpana Sana,nilitaka unijibu kwanza hoja zangu 6 ili nijue ww ni mtu wa aina gani,lakin kinacho nisikitisha zaid bado unakwepa hoja zangu kama uLivyo fanya DW.
Rhz...
Ungesoma kwanza kama nilivyokushauri hakuna haja ya kukimbilia kufanya mjadala ilhali hulijui somo lenyewe.

Huwezi kusoma basi sikulazimishi.
 
Kitali,
Soma kitabu changu, "Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama," uone vipi nimemueleza Mangi Sina.

View attachment 2044502
unachofanya sio kutuletea historia ya nchi hii. unatuletea historia ya uislam. mi nimekupa mfano wa Mangi Sina lakn historia ya Uchaggan haianz na Sina Mzee. unatakiwa uje na historia ya hii nchi kabla hajaja mzungu. kwa mfano utuambie wazaramo hapo kale walitokea wap wakafika hapo watawala wao nk. kuna washiraz walikuja hapa miaka karibu 800 iliyopita nk. kuna tawala mbali mbali za kichifu namna walivyotawala. kuingia wamisionari shughuli zao nk. kuingia kwa wakolon na mapambano yaliyotokea vita ya maji maji nk. mpaka akina Nyerere na kundi lake na mpaka leo. sasa wewe muda wote unatafuta jina la Kiislam unalifuatilia halafu unakuja na jibu kuwa huyu alikuwa mpigania uhuru. hzo hadith utawadanganya hao wanywa kahawa na kashata huko vibarazan.
 
Kwa nini umeghadhibika kiasi hiki na kutoa maneno ya kunikejeli.

Tuchukulie kuwa mimi nimekosea katika jibu langu la Mangi Sina.

Ustaarabu ungeandika kwa taratibu na kunieleza kuwa nimekosea badala ya kutoa maneno ya jeuri.

Mimi nakushauri soma hicho kitabu kwanza ndiyo uchangie.

Nakuwekea hapa kipande kidogo kutoka kitabu changu:

''Mabadiliko haya ya utawala, na Mangi Sina kutaka Shangali atawazwe kuwa Mangi kama alivyotaka mfadhili na mlezi wake, ndiyo yaliyosababisha Mangi Sina kushambulia Machame mara kwa mara baada ya kifo cha Mangi Ndeseruo.

Ipo tofauti kubwa sana baina ya kumuua adui kwenye uwanja wa mapambano katika medani ya vita na kumuua mtu pembeni kwa kumvizia ukampiga mkuki, mshale au mapanga.

Kuna maelezo kuwa Muro Mboyo alimfahamisha Ngamini njama hii ya kumtoa roho yake na akamshauri wakimbie wote wakajisalimishe kwa Mangi Rindi Mandara wa Old Moshi.

Lakini hawakuwahi kufanya hili kwani mwishoni mwa mwaka wa 1889, palizuka vita vya wenyewe kwa wenyewe na jina la Muro pamoja na Nasua, Karawa, Ngulelo ambaye baadaye alikuja kujulikana kama Mangi Selemani yametajwa kuhusika katika ugomvi ule.''

Kitabu hiki nimeandika kutokana na nyaraka ambazo zimehifadhiwa kwa miaka 100 na nimesikiliza historia iliyohifadhiwa na ukoo wa ukoo wa Chief Shangali na ukoo wa Nkya kwa miaka zaidi ya 200 kizazi kimoja kikirithisha historia hiyo kwa kingine hadi kunifikia mimi mwaka wa 2019.

Sikukatalii kuwa sisi ni wanywa kahawa na kashata.

Wala hatuoni aibu kwa hili kwani huu ndiyo utamaduni wetu.

Ila tambua kuwa kunywa kahawa na kashata hakutufanyi tukawa wajinga.

Malezi ya wazee wetu wanywa kahawa na kashata ndiyo yaliyotufanya kuwa hivi hatugusi ulevi wa aina yoyote ila kwa yule aliyepotoka.

Lakini halikadhaika hatukai tukawatukana wale ambao imani, mila na desturi zao zinawaruhusu mathalan kunywa mataputapu katika vilabu vya pombe.

Hii ndiyo adabu waliotufunza mama zetu.

Wewe mama yako kakufunza adabu gani?

Kuwatukania watu mila na itikadi zao?
 
Kitali,
Kwa nini umeghadhibika kiasi hiki na kutoa maneno ya kunikejeli.
Tuchukulie kuwa mimi nimekosea katika jibu langu la Mangi Sina.

Ustaarabu ungeandika kwa taratibu na kunieleza kuwa nimekosea badala ya kutoa maneno ya jeuri.

Mimi nakushauri soma hicho kitabu kwanza ndiyo uchangie.
Nakuwekea hapa kipande kidogo kutoka kitabu changu:

''Mabadiliko haya ya utawala, na Mangi Sina kutaka Shangali atawazwe kuwa Mangi kama alivyotaka mfadhili na mlezi wake, ndiyo yaliyosababisha Mangi Sina kushambulia Machame mara kwa mara baada ya kifo cha Mangi Ndeseruo.

Ipo tofauti kubwa sana baina ya kumuua adui kwenye uwanja wa mapambano katika medani ya vita na kumuua mtu pembeni kwa kumvizia ukampiga mkuki, mshale au mapanga.

Kuna maelezo kuwa Muro Mboyo alimfahamisha Ngamini njama hii ya kumtoa roho yake na akamshauri wakimbie wote wakajisalimishe kwa Mangi Rindi Mandara wa Old Moshi.

Lakini hawakuwahi kufanya hili kwani mwishoni mwa mwaka wa 1889, palizuka vita vya wenyewe kwa wenyewe na jina la Muro pamoja na Nasua, Karawa, Ngulelo ambaye baadaye alikuja kujulikana kama Mangi Selemani yametajwa kuhusika katika ugomvi ule.''
mzee nimekuambia tena historia ya uchaggan haianz na Sina au shangali . unapozungumzia historia anza na vizaz vilikotokea. ndio uje na tawala. Sina ni wajuz sana. unamjua Mangi Tatua wewe? na by the way wachagga walitawaliwa na Wamangi tofaut kila kanda ya eneo. so historia yako inatakiwa ituambie kwa mfano wamasai ni watu gan wametokea wap wakaanzaje maisha na mpaka leo. hivyo kila jamii nchi hii. sio kutafuta historia ya Kirima cjui akaenda kwa Mangi sina so what? by the way hata sabab za Sina kupigana na Wamachame sizo ulizoandika. na Sina ni wa zaman shangali ni wa juz sana. ukitaka kitabu cha historia za wachagga tawala jografia na uchumi kipo utpawe. lakn msing wa hoja yangu uwe unaandika historia ya nchi sio din. Kirama unamjua wewe na waislam wenzio pale bomang'ombe ila uchagan hajulikan kwa lolote.
 
Ni kweli WaIslam wanabaguliwa sana ndio maana.

Rais wa JMT ni mgalatia
Waziri Mkuu ni Mgalatia
Rais wa Zanzibar ni Mgalatia
Jaji Mkuu ni Mgalatia
Jaji Kiongozi Mgalatia
Haya malizia wabunge wangapi Wakristo ?Scholarship ngapi munawapa waislamu .?Na kwa upende wa elimu wanavunzi wangapi waislamu munawafelisha kuna makorokoro kibao Fumba domo lako anayo ndugu yetu Mohd Said yako sawa ndio maana yanawekera kwa sababu anajaribu kuwamsha waislamu wamelala sana .
 
Kitali,
Kwa nini umeghadhibika kiasi hiki na kutoa maneno ya kunikejeli.
Tuchukulie kuwa mimi nimekosea katika jibu langu la Mangi Sina.

Ustaarabu ungeandika kwa taratibu na kunieleza kuwa nimekosea badala ya kutoa maneno ya jeuri.

Mimi nakushauri soma hicho kitabu kwanza ndiyo uchangie.
Nakuwekea hapa kipande kidogo kutoka kitabu changu:

''Mabadiliko haya ya utawala, na Mangi Sina kutaka Shangali atawazwe kuwa Mangi kama alivyotaka mfadhili na mlezi wake, ndiyo yaliyosababisha Mangi Sina kushambulia Machame mara kwa mara baada ya kifo cha Mangi Ndeseruo.

Ipo tofauti kubwa sana baina ya kumuua adui kwenye uwanja wa mapambano katika medani ya vita na kumuua mtu pembeni kwa kumvizia ukampiga mkuki, mshale au mapanga.

Kuna maelezo kuwa Muro Mboyo alimfahamisha Ngamini njama hii ya kumtoa roho yake na akamshauri wakimbie wote wakajisalimishe kwa Mangi Rindi Mandara wa Old Moshi.

Lakini hawakuwahi kufanya hili kwani mwishoni mwa mwaka wa 1889, palizuka vita vya wenyewe kwa wenyewe na jina la Muro pamoja na Nasua, Karawa, Ngulelo ambaye baadaye alikuja kujulikana kama Mangi Selemani yametajwa kuhusika katika ugomvi ule.''

Kitabu hiki nimeandika kutokana na nyaraka ambazo zimehifadhiwa kwa miaka 100 na nimesikiliza historia iliyohifadhiwa na ukoo wa ukoo wa Chief Shangali na ukoo wa Nkya kwa miaka zaidi ya 200 kizazi kimoja kikirithisha historia hiyo kwa kingine hadi kunifikia mimi mwaka wa 2020.

Sikukatalii kuwa sisi ni wanywa kahawa na kashata.
Wala hatuoni aibu kwa hili kwani huu ndiyo utamaduni wetu.

Ila tambua kuwa kunywa kahawa na kashata hakutufanyi tukawa wajinga.

Malezi ya wazee wetu wanywa kahawa na kashata ndiyo yaliyotufanya kuwa hivi hatugusi ulevi wa aina yoyote ila kwa yule aliyepotoka.

Lakini halikadhaika hatukai tukawatukana wale ambao imani, mila na desturi zao zinawaruhusu mathalan kunywa mataputapu katika vilabu vya pombe.

Hii ndiyo adabu waliotufunza mama zetu.
Hii thread ni ya kimkakati zaidi kuliko uhalisia wa kinachojadiliwa, naendelea kuamini katika Timing yake,
 
Nilikuwa nasikiliza kipindi cha maoni kinachorushwa na DW, ndipo nikamsikia huyu mtu anaitwa Mohamed Said akitoa maoni yake kuhusu miaka 60 ya uhuru, ingawa kabla nimewahi kusoma makala zake kadhaa, sikufikiri kwamba kwa ukubwa wa changamoto tulizonazo leo pamoja na mabadiliko makubwa ya kielimu na kimfumo bado atakuwa na mawazo kwamba waisilam wanabaguliwa.

Ninapata shida kumwelewa kwa sababu kwa taifa letu lilipofikia ningeweza kusema kama ni ubaguzi unaopaswa kupambana nao ni ule unaopendelea chama tawala.

Ubaguzi anaosema waisilam wanabaguliwa ni wa kufikirika sana. Sijui kama huyu ndugu amefanya utafiti kujua wakristo na waisilam wanaosota na kubaguliwa kwa sababu wao sio CCM!!.

Akiwa anasema hayo wapo viongozi wa kiisilam wengi tu wanaoshiriki uharamia wa kuwabagua ndugu zao ilimradi tu sio CCM.

Nashauri aache mambo ya kukaririshwa kwamba waisilam wanaonewa hizo hoja zilishapitwa na wakati. Isitosha zinafanya waisilam waonekane wanyonge na watu wa kuhurumiwahurumiwa tu.
Akili kubwa sana hii Mkuu
 
Wewe hujui historia ya Tanzania wakati hawa wazee wanapambana ulikuwa maporini huko lazima utasema hivyo.
 
Mzee Mohamed Said, ulishawahi walau kuhoji mbali na Kudai haki za watu wa Imani za zilizokuwepo kabla ya Uislamu na Ukristo?

Kama ni kuchimbua mizizi ya Dhuluma, kwanini tusianzie huko?

Je, umejaribu kutafakari hata kidogo, ni maumivu na mateso na hata damu kiasi gani ilimwagwa na Wahenga wako, ili kufanya wewe uzaliwe katika Uislamu na mwingine Ukristo? Haki za Asili yako hudaiwa na nani kama unatetea udhalimu juu yao?

Unataja Taasisi za Kimataifa kama Oxford nk kushibisha uhalali wa hoja zako, Je, hujui ni kwa namba gani hizo Taasisi nyingi ni Manipulative na agents wa Utumwa wa Fikra Ulimwenguni?

Ulishawahi kuhoji zinawasemeaje Waislamu wa Afghanistan au Iraq? Aje wale Wasomalia? Au ndio umeamua kula nguruwe aliyenona?
 
Ukweli ni Maji na Uongo ni Povu la Omo .Hawataki Ukweli kwa sababu wanaujua au hawataki ukweli kwa sababu ni wajinga na wapumbavu .Je munafanana watu wanaojua na watu wasiojua lakini UKWELI UTABAKIA MILELE.
 
Mzee Mohamed Said, ulishawahi walau kuhoji mbali na Kudai haki za watu wa Imani za zilizokuwepo kabla ya Uislamu na Ukristo?

Kama ni kuchimbua mizizi ya Dhuluma, kwanini tusianzie huko?

Je, umejaribu kutafakari hata kidogo, ni maumivu na mateso na hata damu kiasi gani ilimwagwa na Wahenga wako, ili kufanya wewe uzaliwe katika Uislamu na mwingine Ukristo? Haki za Asili yako hudaiwa na nani kama unatetea udhalimu juu yao?

Unataja Taasisi za Kimataifa kama Oxford nk kushibisha uhalali wa hoja zako, Je, hujui ni kwa namba gani hizo Taasisi nyingi ni Manipulative na agents wa Utumwa wa Fikra Ulimwenguni?

Ulishawahi kuhoji zinawasemeaje Waislamu wa Afghanistan au Iraq? Aje wale Wasomalia? Au ndio umeamua kula nguruwe aliyenona?
Kwa nini usihoji wewe kuna mtu kakukataza?
 
Kusema ukweli mimi namuogopaga sana Mohamed Said. Naonaga kama mkristu akikaa nae karibu ataweza kumpa hata sumu. Naonaga vidio zake yutube. Anaongea kwa chuki sana. I MIGHT BE WRONG. INAWEZEKANA SAID NI MTU POA TU
Mkristu pekee huyu mzee anaemkubali sharti asiwe mtanzania labda wa Mzungu au wa mataifa ya kiafrika .

Watu kama hawa ni sumu kwa Taifa .

Mimi Rafiki zangu wengi sana waislamu na nashirikiana nao safi kabisa katika maisha .

Lakini watu wa dizaini hii hatari mzee anaweza kukuchoma hivi hivi kisa wewe ni dini tofauti na yeye!!?

Dini zenyewe tumeletewa lakini twajifaya tunazijua zaidi ya hao waliotuletea ,ya shangaza sana na kuogopesha!!![emoji15]
 
Hakika ni mawazo ya kijihadist ambayo yamepitwa na wakati. Siku hizi tanzania ukiona waislamu wenye hii mambo ya kukandamizwa au kubaguliwa kwa uhakika wanatafuta upendeleo kuteuliwa.
Majuzijuzi tumeona watu wakimtolea mama orodha ya wakurugenzi mashirika ya umma kwenye mitandao kuonesha wakristo wangapi na waislamu wangapi. Namna yoyote ya kusawazisha bila kuona weledi na uadilifu na uzalendo ni jambo la kijinga.
Tumeshaona waziri mmoja mwenye rekodi nzuri sana wa nishati akiondolewa na kuwekwa mtu anayetiliwa mashaka utendaji wake na watu wengi. Hakuna sababu yoyote imetolewa hadi sasa kwa nini dr menard ameondolewa.
TANESCO huwa ni chaka la kupiga pesa kwa wakubwa. Maza kaamua kufuata ushauri wa 'wahuni' akamuweka waziri Ma'rope' ili afanikishe mishe zao za upigaji as ndo anawezaga hizo makitu. Si unasikia kaingia tu biashara ya majenereta na Sola imependeza? Pia kakodi softiwea kwa 68B?
 
"TANESCO huwa ni chaka la kupiga pesa wakubwa"

Hii ni hoja ya msingi sana ya kuijadili kupita hiyo mada ya Mzee saidi,
Nadhani nia ya huyo mzee ni kuuza vitabu vyake tu. Na hasa apate soko toka kwa Waislam.
 
Wacha roho mbaya yako kwani umelazimishwa wewe kununua kitabu
 
Mzee Mohamed Said, ulishawahi walau kuhoji mbali na Kudai haki za watu wa Imani za zilizokuwepo kabla ya Uislamu na Ukristo?

Kama ni kuchimbua mizizi ya Dhuluma, kwanini tusianzie huko?

Je, umejaribu kutafakari hata kidogo, ni maumivu na mateso na hata damu kiasi gani ilimwagwa na Wahenga wako, ili kufanya wewe uzaliwe katika Uislamu na mwingine Ukristo? Haki za Asili yako hudaiwa na nani kama unatetea udhalimu juu yao?

Unataja Taasisi za Kimataifa kama Oxford nk kushibisha uhalali wa hoja zako, Je, hujui ni kwa namba gani hizo Taasisi nyingi ni Manipulative na agents wa Utumwa wa Fikra Ulimwenguni?

Ulishawahi kuhoji zinawasemeaje Waislamu wa Afghanistan au Iraq? Aje wale Wasomalia? Au ndio umeamua kula nguruwe aliyenona?
a4a...
Hayo uliyoleta hapa si hoja iliyoletwa hapa dhidi yangu nami nikaja kuijibu.
 
Back
Top Bottom