Mohamed Mpakanjia is no more!

Mohamed Mpakanjia is no more!

RIP meddy
it s not wise to try hiding the true cause of his death tho'
most of us know he has died of HIV/AIDS so whats the big deal trying to keep the public from knowing the truth??
if we real mean TANZANIA BILA UKIMWI we should be open!
 
Ndo maana kocha wa zamani wa yanga na mhadhiri wa udsm yupo fiti mpaka kesho
yes nimekubalikweli humu JF kuna DATA BANKS sio za kawaida,humu jamvini tunalonga waziwazi,sasa huyo kocha na huyo mhadhiri ni nani,at least tunanaomba faculty yake
 
- Wakuu heshima mbele sana, sasa kama kweli huyu homeboy ametangulia na ngoma, sasa itakuwaje kwa mbunge maarufu maana sio siri kwamba siku Amina alipotangulia mbunge wetu aliposikia alianguka na kuzimia hapo hapo sasa alipona kweli na dude hili au?

- Anyways, RIP Med-Mpakanjia, a hero homeboy kutoka ghetto mpaka kufikia kuwa the man mjini, mfano wa kuigwa kwa all the ghettos, kwamba kuzaliwa huko sio a death sentence, ila tu the lesson hapa ni kwamba fame and richness comes with higher responsibilities!

- Lakini, it is about time sasa, wa-Tanzania tukashituka kwamba this thing ngoma is for real, ninakumbuka sana kwa mara ya kwanza hili dude then kwa jina la "Juliana" lilipoingia Dar in the 80s, lilimuanza one of my best friend William Pamba, may God bless his soul, wengi tulidhani it was a joke, lakini since then tumepoteza ma-hommies kibao, I mean where is it going to stop?

- Halafu kwa nini hatuwi wakweli inapotokea mtu maarufu amechukuliwa na hili dude? Tuache huu utamaduni wa hovyo sana usemwe ukweli ili wengine wajifunze, I mean tufike mahali tuache hizi tabia na utamaduni mbovu sana wa kuaminisha jamii kwamba wananchi maarufu au matajiri katika jamii yetu hawakumbwi na hili gonjwa ila masikini tu, hii ni dhana mbovu sana kwa the future jamii na hasa vijana wetu wadogo!

- Waandishi wetu mbona mengine ya kijinga sana mnajua kufuatilia lakini haya ambayo ni muhimu zaidi kwa kuelimisha taifa mnafumbia macho na kushiriki kulidanganya taifa eti amekufa na ugonjwa unaoletwa na baridi, wakati watu wote tulioamka tunajua kwamba Dar hakuna baridi ya kuua mtu, basi si mngetafuta girini zito zaidi ya kukomalia baridi ya mapafu kila wakati, tafuteni lingine basi maana hili girini ni too low!

RIP Hommie Med-Mpakanjia, may God bless your soul!

Respect.

Field Marshall Es!
 
Pneumocystis Carinii pneumonia PCP wanasababishwa na aina fulani ya fungus waitwao pneumocystis carinii,

Na dawa zake zinakuwaga Septrin
Trimethoprim na Sulfamethoxazole , Bactrim , Septra

Ila ndugu yangu Pneumonia hii kidogo ni ngumu katika kutibika ukilinganisha na Pneumonia inayosababishwa na Bacteria .
Muombe mungu akuepushie hii kwani ni ya haraka zaidi.

Ili kwenda na wakati - napenda kuwajuza kuwa huyo organism Pneumocystis carinii siku hizi anaitwa Pneumocystis jirovecii na ana tabia za fungus na protozoa!
Wasalaam,
 
FMES,umelonga sasa whats next kwa mbunge kijana-maana as from now onwards his movements will be under FBI like scrutiny-this peril it seems is likely to claim many a high profile victims
 
Mkuu kama unayosema ni kweli kabisa, yaani kama ndio sayansi yenyewe, umenimaliza nguvu kabisa! Hizi ARV mi nilidhani zimeshaleta matumaini makubwa sana, naona watu wakiendelea na maisha yao na kutunza familia zao vizuri tu huku wakiendelea na shughuli zao za kiuchumi vizuri. Lakini kama ndio 'silent killer' ya kihivyo, naona ni balaa kabisa! Au labda jamaa alikuwa hazingatii dawa bana, mbona jamaa wengine kibao wako fresh tu?

Wajua nilishaelewa kuwa mtu akiwa kwenye hizo ARV basi ni 'life as usual', mradi tu akumbuke dozi yake daily, mambo ya check ups kwa physician wake mara kwa mara, awe active, mambo ya sports nk, ndivyo ninavyoona wengine wakiishi.

Mtu B:

Naona hapa kuna miss-information. Hapa Marekani kuna watu walioanza kutumia ARV toka miaka ya katika ya 80 na mpaka sasa bado wanadunda.

Kama kweli ARV ni Silent killer, basi kutakuwa na matatizo katika matumizi yake nchini Tanzania.

Moja ya matatizo hayo ni matumizi mabaya ya madawa yenyewe. Matumizi mabaya yanafanya virus kuwa immune. Virus wakiwa immune, effectiveness ya madawa yenyewe inakuwa hakuna.

Vilevile katika tiba kuna madawa ya aina mbili. Kuna madawa ya kutibu magonjwa na maintanance drugs. Ukimwi, kisukari, BP ni magonjwa ambayo hayana dawa za kutibu lakini kuna maintanance drugs. Maintanance drugs zinaambatana na mabadiliko ya life-style.

Kwa bahati mbaya sana, watanzania wengi hatubadili life-style zetu tunapokuwa na magonjwa yanayohitaji maintanance drugs. Mtu mwenye kisukari anakunywa chai yenye sukari, atakunywa pombe na mambo mengi.

Kuwa mkweli vilevile kuna saidia sana kwenye tiba. Kama unaficha basi hata tiba yenyewe utaitafuta kwa kujificha na vilevile unakosa moral support kutoka kwa ndugu na jamaa.

Kutokana na matumizi ya madawa na virus kuwa immune, virus wa UKIMWI wana sub-type zake. Hivyo ARV moja inaweza kuwa effective kutibu sub-type moja na kushindwa kutibu sub-type nyingine. Hivyo basi waathirika wanatakiwa kuendelea kutumia kondomu. Kwa maana mgonjwa mmoja anaweza kuambukizwa na sub-type nyingine ambayo imekubuu madawa.
 
Ili kwenda na wakati - napenda kuwajuza kuwa huyo organism Pneumocystis carinii siku hizi anaitwa Pneumocystis jirovecii na ana tabia za fungus na protozoa!
Wasalaam,

nashukuru kwakufahamisha mkuu....
 
Last edited:
Nadhani nimetumia busara sana..!!! Huwa kikombe naita kikombe na sahani ni sahani mkuu..!!

Inshallah kama umetafsiri ndivyo sivyo..!!!
 
Siku za mwisho za Mpakanjia
Mwandishi Wetu
Kifo cha mfanyabiashara maarufu Mohamed Mpakanjia ambaye pia alikuwa mume wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Marehemu Amina Chifupa, kimeibua majonzi makubwa kwa wengi wanaomfahamu huku wengine wakijaribu kuelezea siku za mwisho za mpendwa wao huyo.

Kwa mujibu wa baadhi ya wale waliokuwa wakimfahamu vya kutosha marehemu Mpakanjia, ni kwamba mwishoni mwa siku za uhai wake, alijtahidi kuzidisha ibada, huku akiswali sana pale katika Msikiti wa Masjid Noor, uliopo Sinza Palestina Jijini.

Akizungumza na Alasiri, mmoja wa waumini wanaoswali mara kwa mara katika msikiti huo wa Masjid Noor, amesema Mpakanjia alionekana kuzidisha ibada na kufanya mambo mengi mema.

Amesema muumini huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mohamed kuwa hata Ijumaa iliyopita, Mpakanjia aliswali naye kwenye safu moja pale Masjid Noor na kwamba alimshangaza zaidi kwani aliomba sana dua na kulala kwenye zulia.

"Kwakweli kati ya walioguswa sana na kifo chake, mimi ni mmojawapo kwa sababu nilikuwa naye kwenye safu moja wakati wa swala ya Ijumaa iliyopita," akasema muumini huyo.

Akieleza zaidi, akasema kuwa wakati mtoa mawaidha wa siku hiyo ya Ijumaa msikitini hapo ambaye ni Sheikh Hashim Rusaganya, Mpakanjia alionekana akisikiliza kwa umakini, kabla hajamaliza kuswali swala nyingi za sunna na hatimaye kuanza kujinyenyekeza mbele za Muumba, kisha akaomba sana dua.

"Nilimshuhudia mwenyewe jinsi alivyokuwa akiomba dua kwa Allah (Mwenyezi Mungu)... alinyoosha mikono yake, akawa kama anayefumba macho na kuomba sana," akasema.

"Baada ya hapo, alilala chali msikitini humo na kuendelea kuomba huku Sheikh Rusaganya akiendelea kutoa mawaidha... aliendelea kulala huku mikono ikiwa kifuani mwake hadi wakati wa swala ya Ijumaa ndipo akasimama na kuswali kama waumini wengine ," akaongeza.

Akasema baada ya swala, yeye alitoka msikitini hapo na kumuacha Mpakanjia akiendelea na maombi yake msikitini.

"Kwakweli nilishangaa jana kusikia kuwa amefariki... inasikitisha sana," akasema.

Aidha, taarifa nyingine zinaeleza kuwa siku chache kabla ya umauti, Mpakanjia alishirikiana na familia yake katika kutoa mchango mkubwa wa kufanikisha mashindano ya usomaji Qur-an yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Starlight Jijini ambapo washindi walitunukiwa vitita vikubwa vya pesa.

Mpakanjia alifariki jana saa 8:30 mchana katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo ambako alilazwa kuanzia saa 5:00 asubuhi, hiyo hiyo jana.

Inaelezwa kuwa awali, marehemu alikuwa akisumbuliwa na homa ya matumbo (typhoid).

Pia inadaiwa kuwa figo yake moja ilishindwa kufanya kazi na kusababisha umauti wake.

Aidha, kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Abdul, mazishi yake (Mpakanjia) yalitarajiwa kufanyika leo mchana, pale kwenye makaburi ya Kisutu ambapo mamia ya watu wanatarajia kuhudhuria, akiwemo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu na Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba.

ALASIRI
 
Amour Hassan
Hemed Mpakanjia, aliyekuwa mume wa Mbunge wa Vijana Viti Maalum (CCM), Amina Chifupa amefariki dunia ikiwa na siku moja tu baada ya kuoa mke mwingine aliyetajwa kwa jina la Zaituni.
Mpapanjia anadaiwa kuwa alifunga ndoa eneo la Magomeni juzi kabla ya jana na kukimbizwa hospitali ya Jeshi ya Lugalo jana saa 5.00 asubuhi, lakini alifarikia saa tatu na nusu baadaye, yaani saa 8.30 mchana.
Mpakanjia ambaye alikuwa mfanyabiashara na mpenzi mkubwa muziki, atazikwa leo saa 7:00 mchana kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa familia kaka wa marehemu, Abdul Mpakanjia, alisema Mpakanjia maarufu kama Meddy, alikimbizwa hospitali ya Lugalo baada ya kujisikia vibaya.
"Alikuwa mzima akifanya shughuli zake kama kawaida, lakini tulimpeleka hospitali baada ya kujisikia vibaya.
"Kama wiki mbili hivi nyuma alikuwa akijisikia tumbo linamsumbua.... alipoenda kucheki aligundulika kuwa ana typhoid. Sasa leo tulipompeleka hali yake ikawa mbaya na ikagundulika kuwa figo moja imefeli... hicho kimechangia kifo chake.
"Unajua alikuwa akifunga, sasa na kutokana na kuwa mgonjwa hali yake ikawa mbaya sana wakati tulipomfikisha hospitali. Madaktari waliwahi kumshughulikia, lakini ilipofika saa 8:30 akafariki," alisema Abdul.
Msemaji huyo aliongeza kuwa msiba upo nyumbani kwake Sinza alikokuwa akiishi na mama yao mzazi na wafanyakazi tangu alipofariki mkewe Amina.
Jana nyumbani hapo walionekana ndugu na jamaa wakimiminika kwa wingi huku wasanii nyota wa fani mbalimbali walionekana wakiwa wamejawa na huzuni. Miongoni mwao alikuwepo rafiki yake mkubwa Mbunge wa Mbinga-Magharibi Kapteni John Komba, mmiliki wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka, waigizaji wa luninga, Richie Richie, Dude, Cloud na JB, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa marehemu.
Wanamuziki wa TOT kama Juma Jerry, rapa Jua Kali, na muandaaji wa matamasha wa miaka mingi nchini Juma Mbizo, ambaye pia ni rafiki wa karibu wa marehemu pia walikuwepo.
Kapt Komba alisema kuwa msiba huo umemhuzunisha sana kwanza kama rafiki wa karibu na pili kama mdau wa burudani ambaye alikuwa akimpa ushauri katika mambo mengi yakiwemo ya kimaisha na hata kuimarisha kundi lake la TOT.
"Ni pigo kubwa sana," alisema Komba. Tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi, "alisema Komba kwa huzuni.
Mpakanjia anafari dunia miaka miwili miezi miwili na siku 14 baada ya kifo cha mkwe, mbunge kijana machachari, Amina, aliyechanua kama ua na kunyauka ghafla Juni 26, 2007.
Amina kwa kipindi kifupi alichokuwa mbunge tangu Desemba 2005 hadi Juni 2007 alijitwali umaarufu mkubwa hasa baada ya kutangaza wazi kwamba atapambana na wauzaji wa dawa za kulevya bungeni. Kifo cha Amina mbali ya kuacha simanzi kubwa, pia kiliacha maswali jinsi maisha yake yalivyofikia ukomo kwa kasi kubwa.
NIPASHE
 
Huyo shuhuda wa sala yeye alikuwa haswali? mbona kama alikuwa anamwangalia tu Marehemu anavyoswali? ( Ah nimesahau kumbe huwa hawafumbagi macho!)
 
Huyo shuhuda wa sala yeye alikuwa haswali? mbona kama alikuwa anamwangalia tu Marehemu anavyoswali? ( Ah nimesahau kumbe huwa hawafumbagi macho!)

Hilarious comment! Dada unaakili sana ...Jamaa alikuwa anapiga chabo (Kozimeni) mwenzake akiswali....nadhani ni upambe tu anatengeneza story!
 
Kule kwa michuzi kuna jamaa amesema Meddy alikuwa na majipu kweli
RIP
 
Back
Top Bottom