Mo Ndani Ya Fox News

Mo Ndani Ya Fox News

Hapo napo bado yanaibuka maswali mengine kwa hao walinzi, ni wakati gani wamegundua uwepo wa hiyo gari hilo eneo, inasemekana wao ndio waliomfungua kamba alizofungwa. Hawakuona chochote zaidi ya kuikuta tu hiyo gari ikiwa imeachwa?
Nani alikuja nayo, aliondokaje na vitu kama hivyo.
Na hao walinzi nn kiliwazuia kuwasiliana na polisi kiasi mambo leo na wengineo wakaenda kumuona mo nyumbani kwake?kwa nini haikuwa polisi then hospital kujiridhisha uzima wake?
 
Uwezo wako wa kutafakari ni mdogo Sana Kama wa mende.

1. Bunduki walizinunua/waliziandaa ili kufanikisha zoezi la kupata pesa. Kumbuka walifyatua risasi wakati wa zoezi la kuteka so maganda ya risasi yalichukuliwa na polisi. Kupitia hayo maganda ya risasi wataalam wa polisi wangebaini ni bunduki hiyo/hizo ndizo zilizotumika. Kwa wenye uelewa ni lazima wazitelekeze kwa lengo la kupoteza ushahidi. Hivyo kushindwa kufanikiwa kwa zoezi lao ndiyo ilikuwa ukomo wa kuwa na hizo silaha

2. Watekaji siyo waliyompa MO cm ya kuongea na nduguze bali RAIA wema waliyomuokota

3. MO hakuwa na cash money na ili ipatikane cash money ilikuwa ni lazima afanye mawasiliano kupitia hayo mawasiliano watu wa cyber wangebaini location na ingekuwa ni rahisi kuwakamata

4. Mipaka ya nchi ilifungwa so wasingeweza kutoka nje ya nchi ambako wangekuwa na Uhuru wa kufanya communication

Kwa mazingira hayo Kama una akili ya kupambanua mambo ilitakiwa uwasifu hao watekaji ya kuwa wana uelewa mkubwa Sana wa maswala ya kiupelelezi. Kwa kurumia uelewa huo wamefanikiwa mukwepa mbinu zote za kukamatwa wao sambamba na kukamatwa na vielelezo
Kwa hiyo sasa hv hawawezi tena kukamatwa?
 
Watu na akili zao hutoa habari zao toka kwa mamlaka husika..sio hapa kila mtu ni mtaalam wa intelijensia..

Sijui kwanini polisi hawamchukulii hatua Lema kwa kutoa kauli zenye kuingilia mchakato wa upelelezi.
 
Na hao walinzi nn kiliwazuia kuwasiliana na polisi kiasi mambo leo na wengineo wakaenda kumuona mo nyumbani kwake?kwa nini haikuwa polisi then hospital kujiridhisha uzima wake?

Hii habari kila unavyoendelea kuifuatilia inachefua, nafikiri huu sasa ndio wakati muafaka wangeendeleza lile katazo lao la kuijadili.
 
Tanzania, watekaji wanatoka nchi jirani wanataka hela hawasemi ni kiasi gani halafu wanakuachia wanakupa simu halafu wanaacha bunduki na kupotea
Wanafanya jaribio la kuichoma gari,"wanashindwa" inawezekana ile gari imetengenezwa kwa madini ya asbestos. Na eneo walipomwachia haiingii akilini kwani ni eneo lenye ulinzi mkali. Drama nyingine ni kuacha silaha ndani ya gari. Mi naamini " kuchamba sana utatoka na mavi"
 
Nyani Ngabu hii habari imetikisa kuanzi Latin America , Australia , Canada, hapo EU na mashariki ya kati. Hii kitu ina impact sijui ni kwa namna gani lakini ni habari ya mijini huko duniani

Pesa Nguruvi3!

Ndo kitu pekee ninachoweza kukifikiria.

Mo asingekuwa bilionea sidhani kama wangemzungumzia.

But I could be wrong...
 
Ulichokosea ni kutokufuatilia nilichoandika awali, mtekwaji na habari zilizotolewa na wazee wetu ndio wamesema walinzi ndio walimpatia jamaa simu akawasiliana na ndugu zake. Hoja yangu ya walizi ndio ilianzia hapo. Nafikiri umenielewa.

Inategemea unaongelea Gymkana ipi, kuna siku mida kama ya saa moja jioni nilikua pale ufukweni usawa wa Gymkana nipondani ya gari, nilishangaa gari lapolisi wale wenye silaha wanaofanya doria walinibudhi sana na kunigombeza sana, walikagua gari kutaka kujua kwanini nipopale mida ile huku wakisema mambo mengine kuwatafutia lawama tu kwa vile pale ni eneo hatari ningeweza hata kuwa nimeshakatwakatwa kama sio kuvamiwa.

Sijataja Ikulu kwa sababu nilikua narejea maelezo yaliyotolewa jana, ukiniongezea huo mzigo utakua unanionea.

umejitetea kama vile mimi ndio mtekaji! hautekwi bana

nimekupata mkuu, thanks for your nice language and clarifications
 
Nyani Ngabu hii habari imetikisa kuanzi Latin America , Australia , Canada, hapo EU na mashariki ya kati. Hii kitu ina impact sijui ni kwa namna gani lakini ni habari ya mijini huko duniani

kaka upo! kimya sana

sioni wa kunipa changamoto umekuwa kimya sana,

haya ya wenzako kuhama yataisha tu!

mimi na wewe kesi yetu ambayo tume i carry over ni kuwa zito msaliti au sio msaliti??. Bado nabisha sio msaliti! sijui umebadili mawazo yako au una msimamo ule ule??
 
Kwa hiyo watekaji walimkabidhi kwa walinzi?
Hiyo hadithi ya simu ya walinzi imekuja baada ya watu kuhoji kuhusu simu

Pamoja na kuwa suspect mkubwa ni system

Bado kuna chances wazazi wa MO walipeleka mzigo, a.k.a ransom au hela!! they will never tell us anything

mzee alikuwa wa kwanza kupigiwa simu, kuliko hata mke wa jamaa!!
 
Mkuu ukichoma moto gari ina maana unazalisha moto mkubwa ukiambatana na moshi na hapo inakua ni rahisi kugundulika hata na mtu aliye mbali.

Kwani unapo litia Moto unabaki hapo ku 'Selfie' ?
 
Pamoja na kuwa suspect mkubwa ni system

Bado kuna chances wazazi wa MO walipeleka mzigo, a.k.a ransom au hela!! they will never tell us anything

mzee alikuwa wa kwanza kupigiwa simu, kuliko hata mke wa jamaa!!
Mkuu waweza kuwa sahihi kabisa, lakini kwa vyovyote vile wakora hao lazima wana mahusiano na system eitha officially or unofficially. Hakuna mkora anaweza kutumia maeneo yale kuhusisha ukora wake bila hofu.
Na kama ni wakora wenye mahusiano na system lakini unofficially basi lazima wana MTU ambaye ni untouchable na asiye muogopa yeyote maana anayeogopwa pekee yeye anammudu. JEE NI NANI HUYO?
 
Siku hizi hakuna kitu.

Waulize akina Jokakubwa ,Mag3 Fundi Mchundo zama hizo balozi wa nyumba kumi na majukumu na heshima yake

Kwa taarifa yako balozi wa nyumba kumi zama hizo alikuwa mjumbe bila kujali vyama
Bado kabisa na hujui nini ilikuwa Tanzania kiulinzi. Hakuna kitu siku hizi usijidanganye
Hivi unajua kuna watu hadi leo hawajawah kusoma na kuelewa mabalozi wa nyumba kumi hasa baada ya vyama vingi. Wengi Bado wanadhan hawa mabalozi ni wa Ccm tu
 
Mkuu waweza kuwa sahihi kabisa, lakini kwa vyovyote vile wakora hao lazima wana mahusiano na system eitha officially or unofficially. Hakuna mkora anaweza kutumia maeneo yale kuhusisha ukora wake bila hofu.
Na kama ni wakora wenye mahusiano na system lakini unofficially basi lazima wana MTU ambaye ni untouchable na asiye muogopa yeyote maana anayeogopwa pekee yeye anammudu. JEE NI NANI HUYO?

uko sahihi, mkuu naona unataka kunitega

sina mkojo mimi!!
 
Hivi unajua kuna watu hadi leo hawajawah kusoma na kuelewa mabalozi wa nyumba kumi hasa baada ya vyama vingi. Wengi Bado wanadhan hawa mabalozi ni wa Ccm tu

wengi ni CCM hata hivyo

upinzani ulitakiwa kupambana kuondoa hawa wawepo kama sehemu ya serikali na siyo ya chama chochote

kikubwa na tatizo ni walikuwepo siku zote before vyama vingi
 
Back
Top Bottom