Mo Ndani Ya Fox News

Mo Ndani Ya Fox News

hii habari imetikisa kuanzi Latin America , Australia , Canada, hapo EU na mashariki ya kati
Kulikua na Mjadala Katika hizo Nchi, au maandishi yanapita tu.. Basi.. Au ilikua breaking news
 
Na mimi ndio habari niliyoisikia japo napo nikajiuliza hao walinzi wa gymkana hawakuiona hiyo gari mwanzo? Sijabahatika kufuatilia imeachwa eneo lipi ili kujua kama ni ndani ya eneo lao la kazi au ni barabarani tu huko nje.

Na kama haikua eneo lao la kazi walifika pale wakati gani tokea gari itelekezwe pale au kitu gani kiliwafanya kuifuata ile gari?
mkuu gymkahan kuna walinzi?

ebu pita wewe pale usiku, kesho uje utoe ushuhuda!!

mnaongea hamjui eneo la vibaka sugu na uporaji wote pale

eti liko karibu na ikulu!!! my foot
 
Kwahiyo wewe unajua zaidi kuliko aliyetekwa eeh! tuamini maneno yako wewe uliyepo huko Tandahimba au tuamini maneno ya Mo?
Tunajua MO anadanganya kwa kuwa ameachiwa kwa makubaliano flani,reading btn the lines. Hizo analysis unazoziona unatafutwa ukweli wa nini hasa kilitokea,jaribu kutumia common sense japo kidogo.
 
Uwezo wako wa kutafakari ni mdogo Sana Kama wa mende.

1. Bunduki walizinunua/waliziandaa ili kufanikisha zoezi la kupata pesa. Kumbuka walifyatua risasi wakati wa zoezi la kuteka so maganda ya risasi yalichukuliwa na polisi. Kupitia hayo maganda ya risasi wataalam wa polisi wangebaini ni bunduki hiyo/hizo ndizo zilizotumika. Kwa wenye uelewa ni lazima wazitelekeze kwa lengo la kupoteza ushahidi. Hivyo kushindwa kufanikiwa kwa zoezi lao ndiyo ilikuwa ukomo wa kuwa na hizo silaha

2. Watekaji siyo waliyompa MO cm ya kuongea na nduguze bali RAIA wema waliyomuokota

3. MO hakuwa na cash money na ili ipatikane cash money ilikuwa ni lazima afanye mawasiliano kupitia hayo mawasiliano watu wa cyber wangebaini location na ingekuwa ni rahisi kuwakamata

4. Mipaka ya nchi ilifungwa so wasingeweza kutoka nje ya nchi ambako wangekuwa na Uhuru wa kufanya communication

Kwa mazingira hayo Kama una akili ya kupambanua mambo ilitakiwa uwasifu hao watekaji ya kuwa wana uelewa mkubwa Sana wa maswala ya kiupelelezi. Kwa kurumia uelewa huo wamefanikiwa mukwepa mbinu zote za kukamatwa wao sambamba na kukamatwa na vielelezo
Rubbish, kwa nini wajitie kwenye hatari(risk) ya kuhangaika kuja kumtupa Gymkhana area kama walikwa makini kiasi hicho?
 
Hapo kwenye red hiyo habari umeipata wapi mkuu?! Mo hakupewa simu na hao watekaji bali alipewa simu na walinzi waliokua eneo lile na kwa vile alikua na namba ya baba yake kichwani ndio akampigia.
Mkuu hao walinzi feki ni wale wale watekaji.
Hao walinzi hawakuwa na wasiwasi na hilo gari aijipii alishalionyesha awali.

Hilo Gari la IGP ndo hilo hilo lililomteka Mo.

Tofauti ni hii..


Picha Ya IGP ni Maandalizi ya Kumteka MO

Na Sehemu ya Tukio ni Gari limekywa modified kwa utayari wa kazi.

Yaani hivi...

Watekaji walilipiga picha kwanza lile gari likiwa kwenye matengenezo. Wakatoa lile tairi la akiba na holder yake pamoja na kubadili plate number kisha gari likaingia mzigoni. Picha ya IGP ni Ushahidi kuwa tayari alikuwa na hiyo picha.

Ukilinganisha taarifa mbalimbali za tokea kutekwa MO huna mashaka kabisa kuwa DAB ni muhusika namba moja.

Kuna saa nahisi hata DAB ndo alikuwa anambembeleza MO ale chakula.

Sura ya MO mbele ya Mambosasa ni kama inajiuliza hivi kumbe kikulacho...
 
Nyani Ngabu hii habari imetikisa kuanzi Latin America , Australia , Canada, hapo EU na mashariki ya kati. Hii kitu ina impact sijui ni kwa namna gani lakini ni habari ya mijini huko duniani
Licha ya Afrika kusini kuwa kinara kwa mabilionaires wake kutekwa kusini mwa jangwa la sahara ila bado inachanua.
 
Hapo kwenye red hiyo habari umeipata wapi mkuu?! Mo hakupewa simu na hao watekaji bali alipewa simu na walinzi waliokua eneo lile na kwa vile alikua na namba ya baba yake kichwani ndio akampigia.
Na walinzi hawakuona jitu hata attempt ya kulixhoma moto gari?
 
mkuu gymkahan kuna walinzi?

ebu pita wewe pale usiku, kesho uje utoe ushuhuda!!

mnaongea hamjui eneo la vibaka sugu na uporaji wote pale

eti liko karibu na ikulu!!! my foot

Ulichokosea ni kutokufuatilia nilichoandika awali, mtekwaji na habari zilizotolewa na wazee wetu ndio wamesema walinzi ndio walimpatia jamaa simu akawasiliana na ndugu zake. Hoja yangu ya walizi ndio ilianzia hapo. Nafikiri umenielewa.

Inategemea unaongelea Gymkana ipi, kuna siku mida kama ya saa moja jioni nilikua pale ufukweni usawa wa Gymkana nipondani ya gari, nilishangaa gari lapolisi wale wenye silaha wanaofanya doria walinibudhi sana na kunigombeza sana, walikagua gari kutaka kujua kwanini nipopale mida ile huku wakisema mambo mengine kuwatafutia lawama tu kwa vile pale ni eneo hatari ningeweza hata kuwa nimeshakatwakatwa kama sio kuvamiwa.

Sijataja Ikulu kwa sababu nilikua narejea maelezo yaliyotolewa jana, ukiniongezea huo mzigo utakua unanionea.
 
Mo mwenyewe Amesema walikuwa na wasi wasi sana.

Tanzania sio nchi ya kuchezea. Kuna wajumbe wa nyumba kumi kumi. Hawa ni part ya wanachama wa CCM na wanalipwa kwa kazi yao. Hawafanyi bure. Katika security hapo utachoka mwenyewe. Mwalim Nyerere aliona mbali sana.

Nawashangaa vijana wa leo katika Press Conferences wanauliza maswali ya kinjinga kuhusu utendaji wa jeshi la usalama na ulinzi Tanzania. Hawajui jinsi hii nchi kiulinzi ikoje? Hiyo ndiyo msingi ya ulinzi wa nchi yetu. Vinginevyo moja wetu ungesha vunjika.

Hii system Mwalim Nyerere kaitoa kwa wachina. Unachosema na kufanya mitaani tayari kimesha reportiwa kwa wahusika na wanajua nini kinatendeka. Nyie kaeni tu na utaalam wenu fake na kuuliza maswali yenu ambayo ni irrelevant.
Mo mwenyewe kaambiw aseme....
 
Tunajua MO anadanganya kwa kuwa ameachiwa kwa makubaliano flani,reading btn the lines. Hizo analysis unazoziona unatafutwa ukweli wa nini hasa kilitokea,jaribu kutumia common sense japo kidogo.
Kwahiyo wewe hiyo ndiyo common sense yako eeh! haya hongera sana.
 
hapo kwenye simu ilitoka kwa walinzi wa eneo umeitoa wapi? walinzi wa eneo la tukio uliwasiliana nao wakathibitisha kumpa simu?, je walichukua hatua gani za kiulizi na kiusalama kuhakikisha watekaji hawatoki eneo lile?, je alitupwa eneo lile pasipo walinzi kuona?, yebooo!
Naona umejikoki kubishana,naomba nikuachie hapa.
 
Na walinzi hawakuona jitu hata attempt ya kulixhoma moto gari?
Mkuu habari za jana nikua Mo alisaidiwa na walinzi wa eneo lile,hayo maswali yako kama waliona gari likichomwa moto,mimi sifahamu.
 
Na mimi ndio habari niliyoisikia japo napo nikajiuliza hao walinzi wa gymkana hawakuiona hiyo gari mwanzo? Sijabahatika kufuatilia imeachwa eneo lipi ili kujua kama ni ndani ya eneo lao la kazi au ni barabarani tu huko nje.

Na kama haikua eneo lao la kazi walifika pale wakati gani tokea gari itelekezwe pale au kitu gani kiliwafanya kuifuata ile gari?
Ndio mkuu hata mimi ndio nilivyosikia hivyo kua alisaidiwa simu na walinzi,hayo mengine sifahamu.
 
Back
Top Bottom