Mkuu una uhakika gani kama Mo hajajiteka mwenyewe?? Mimi naona hii ni "movie" tu imechezwa kwa sababu fulani fulani ambazo hatuzijui. Kama kweli ametekwa Serious basi watekaji wangeshadai fidia muda mrefu sana. Ukiona mtu anatekwa pasipo watekaji kudai "fidia" basi fahamu huo utekaji unamashaka makubwa.
Kama lengo lao lilikuwa ni kumuua basi wangeweza kumchapa "risasi" pale pale nje ya Hoteli, na kama lengo lao ni kupata "information" basi mpaka sasa hivi wangekuwa wameshamwachilia, na pia kama lengo lao ni kupata pesa pia mpaka sasa wangekuwa wameshadai walipwe fidia (ransom).... Kwa kifupi mimi naamini Mo amejiteka mwenyewe.