Mo Dewji afunguka kutekwa kwake kipindi cha Hayati Magufuli

Madwari Madwari

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
1,109
1,931
Mtangazaji : Tumeongelea vitu vingi sana kuhusu wewe. Watazamaji wengi watakaoangalia hii video wanajua kuwa kutekwa kwako ndio stori wanaihitaji kuisikia . Kuhusu kutekwa nyara naomba utuelezee A-Z ilikuwaje ?

Mo Dewji: Kwa miaka mingi nimekuwa na ratiba ya kuamka na Kwenda Gym saa kumi na moja asubuhi. Na gym huwa inafunguliwa mida hipo. Muda wa kuswali unabadilika mara nyingi huwa 04:50 am mpaka 05:15 am. Nilipangia bora niswali ndo niende Gym maana nikenda nikirudi nakuta muda wa kuswali umeshapita. Siku hiyo muda wa kuswali ulikuwa 05.05am -05:10am. Niliamka nikaswali na nikawaamsha watoto.

Ni muda pekee ambao naendesha gari yangu peke yangu. Watanzania ni watu wakarimu sana huwa nasaliminia na watu midaa hii nikienda gym.Na gari yangu ina plate number ya“MO“. Ilikuwa rahisi sana kwa mtu kunifuatilia.Ni mwendo wa dakika 7 kwenda Gym kutoka nyumbani kwangu. Kuna parking ya mmiliki karibu na lango kuu. Mlinzi huwa ananiwekea hio nafasi nikifika ananiruhusu nipark.Mmiliki anachelewa kuingia . Nimemaliza kupark ikaja gari nyuma yangu. Nikajua ni kawaida maana ilikuwa 05:15 am na watu washaanza kufanya mazoezi.

Ile nimemaliza ku-park watu watatu wakanirukia wakapiga risasi juu hewani. Hiki kitu sijawahi kushuhudia Tanzania. Kitu cha kwanza nilichofanya nililala chini. Walinibeba na kunisokomeza ndani ya gari yao. Sasa sikujuwa wanataka nini ? Maana hawakutaka gari langu . Walianza kumuamrisha Mlinzi afungue geti. Mlinzi alifungua geti gari ikaondoka.

Ndani ya dakika ishirini hawa watu walinivua nguo zote huku wakininyooshea bunduki kichwani. Walijua nina kifaa cha kunitrack. Walikuwa wananiuliza kila saa kama nina tracker kwenye nguo zangu. NIliwajibu sina tracker yoyote. Nilikuwa na saa ya “fitbit” wakaichukua na kuitupa.

Tulifika kwenye nyumba nikiwa na foronya ya mto kichwani wangu. Sikuweza kuona vizuri lakini nilikuwana uwezo wa kujua kuwa sasa nimeshaingia kwenye nyumba. Nilishindwa kudadisi muda ulikuwa saa ngapi. Nilijua tumefika ndani ya nyumba ya watekaji kwa sababu foronya ilikuwa inaniruhusu kuona walitumia tape nyeusi kunifunga juu ya foronya ya mto machoni.

Wakanipa khanga nivae kwa sababu sikuwa na nguo. Wakaniamuru nikae chini kulikuwa na godoro chini. Wakanipa simu nikaongea na mtu kwenye simu akasema anahitaji pesa kutoka kwangu. Na ndio simu peke niliyopewa kuongea na mtu akiyekuwa anahitaji pesa kutoka kwangu. Kwa siku tisa walinifunga miguu na mikono kwa tape. Mikono yangu waliifunga kwa nyumba kwa hio sikuwéza kulala wala kukaa. Walikuwa wananipiga na nilishindwa kugungua muda, siku na saa. Nisali na kumuomba Mungu wangu nilijiandaa na kifo.

Siku moja kabla ya kutekwa nilifunga kula,kwa hio kwa hizo siku tisa sikwenda chooni. Kwa sababu sikuweza kula. Kwenda chooni ilikuwa kwa ajili ya haja ndogo,walinichukua na kunipeleka chooni huku nikiwa nimefungwa tape machoni kwa hio sikuweza kuona. Walinilazimisha kula ila nilishindwa kwa sababu ya mshtuko.

Ilipofika siku ya tano wakaniambia tutakuuwa. Nilikuwa nishakubali hali yangu nikawaambia waniue. Unajua ilikuwa siku tano sijaona kitu chochote. Hata wewe ukikaa sahemu ambaypo uko salama ila ukafungwa kwa muda saa limoja tu unaweza ukahcanganyikiwa. Sasa fikiria upo sehemu ambayo hauijui halafu umefungwa macho hauoni chochote. Na watu wanakutushia kukuuaa na kukupiga na bunduki. Ilikuwa kipindi kigumu sana cha siku tisa.

Kila siku Tanzania huwa nanunua magazeti 15 (ya habari, michezo na udaku n.k). Kukitokea Habari kubwa siku ya kwanza inakuwa ukurasa wa mbele, siku ya pili inakuwa ukarasa wa pili baada ya siku chache hio Habari haiandikwi tena. Mke wangu aliyatunza haya magazeti kila siku yalipokuwa yanaletwa nyumbani. Na kila siku kwa siku tisa Habari yangu ilikuwa ukarasa wa mbele wa magazeti.

Na kitu pekee kilichougusa moyo wangu sana ni watanzania wanyonge ndio walikuwa wananiombea. Wakristu waislamu watu wote walikuwa wananiombea. Katika kipindi ambacho kilikuwa vigumu kuongea . Kwa sababu mazingira yalikuwa magumu tulikuwa na uongozi wa wa kibabe watu walikuwa wanaopa kuongea. Mwishowe baada ya siku chache , weekend ikija nasikitika maana weekend bank hazifanyi kazi. Na walioniteka wanataka hela nikajua kuwa mud awa kukaa nao unaongezeka.

Siku ya tisa wakaniambia wananirudisha, niliwauliza kivipi ? Ndio wakaniambia wananiachia sikuamini. Maana nilijua hakuna hela waliyopewa, maana familia yangu wasingetoa hela bila kusikia sauti yangu kuamini kuwa nipo hai. Na pia wangeniuliza ratiba zangu za safari na ningewajibu sahihi wangejua wanaongea na mimi na si mtu mwingine. Sasa nikabaki najiuliza naani atakuteka na akuachie bila hela ? Nilijua wanaenda kuniuwa. Baada ya kunitoa ndani wakanipeleka kwenye gari wanawaasha gari haliwaki. Aisee nilichanganyikiwa baadae wakanirudisha ndani. Wakanifungua mikono na miguu na tape ya kichwani. Baada ya kunivua foronya wakanifunga tape nyingine machoni.

Bada ya kurekebisha tatizo na gari kuwaka, wakanirudisha ndani ya gari tayari kwa kuondoka. Gari ilikuwa na gharufu kali ya petroli. Nikasikia mtu anawasha kiberiti nikawauliza mbona mnawasha kiberiti wakati gari ina harufu ya petroli ? mmoja wao akaniamuru nikae kimya. Tukaanza safari nikiwa bado sina uhakika na hatma ya Maisha yangu. Baada ya muda Gari ikasimama jamaa niliyekuwa nae pembeni akaniambia tumeshafika akanisukuma nje ya mlango nikaanguka nje ya gari.Ilikuwa usiku sana.

Baada yah apo nikaondoa tape nilifungwa machoni nilikuwa sitambui nipo wapi .Nikaanza kujua kuwa nipo katika viwanja vya Golf. Nikaona ubalozi wa Denmark nyuma yangu nikawaona walinzi. Nilivyo jiangalia nilikuwa kifua wazi nikajifikiria ngoja nitafute hoteli yeyote niende. Nikalifikia Jengo la ubalozi wa umoja wa ulaya. Nikiwa natembea walinzi wa jengo wakaniuliza unafanya nini ? nikawaambia mimi ni Mo. Wakanipa pole na wakanisindikiza mpaka Holiday Inn. Nilipofika pale ndio nikapewa simu nikampigia baba. Baba yangu akaja tukaenda nyumbani tulipofika nyumbani tukawataarifu polisi na wakaja.Wakanipima kila kitu na kujua nipo sawa.

Wangeniua toka nilipokuwa Gym. Kuna kitu siwezi kusema, walikuwa Mercenaries waliamrishwa kufanya hii kazi lakini. Kuna kitu kikubwa kuliko hichi kilichojificha lakini mwishowe nia yao haikuwezekana. Pia watu wengi walinisaidia nilisoma Georgetown University. Nusu ya Maafisa wa serikali ya marekani wamesoma Georgetown. Rais wa alumni ya chuo cha Georgetown aliwahimiza serikali ya Marekani. Pia mabalozi wengi ni marafiki zangu. Na baba yangu aliongea na Uongozi wa serikali ya Tanzania kama wamehusika waniachie yuko tayari kutoa chochote. Mpaka leo hakuna mtu aliyekamatwa ndio maana na kuambia kuna vitu ambavyo siwezi kuvisema. Inaitwa paradox tatizo limetokea na limeisha lakini hujui limeishaje Tuyaache kama yalivyo.

Full Interview

View: https://www.youtube.com/watch?v=NjPSQEsUudg
👆 👆 Ameongelea pia kuhamia U.A.E na mwendelezo wa biashara zake. Nimetafsiri kama alivyozungumza Mo kadri ya uwezo wangu sijaongeza wala kupunguza maneno
 
Back
Top Bottom