Kuna ugumu gani kuwakamata waliomteka Mo Dewji na kumpiga risasi Tundu Lissu?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Watanzania mwenzangu nawasalimu.

Kwanza nilipongeze Jeshi letu la Polisi kwa baadhi ya kazi zake nzuri na pia nitoe masikitiko yangu juu ya baadhi ya matukio ya muda mrefu ambayo pamoja na intelejinsia yake limeshindwa kutupa majibu Watanzania.

Mambo ambayo Jeshi letu yanaonekana limeshindwa kabisa ni pamoja na:

1. Kukamata waliomteka Mo Dewji

2. Kukamata waliompiga risasi Tundu Lissu

3. Alipo Ben Saanane

4. Kukamata aliyempiga risasi binti Akwilina

Mambo haya yanafikirisha sana, kwani ndugu na jamaa wanatamani kuwajua na kukamatwa kwa waliofanya huu uhalifu kwa ndugu zao ili haki ya wapendwa wao iweze kupatikana.

Niliamini kama Jeshi letu limeshindwa kuwapata na kuwakamata wahusika, kwanini lisiombe usaidizi wa kitalaamu kutoka nje ili kuwabaini wahusika?

Naamini Jeshi letu lina mahusiano mazuri na Mashirika ya Kijasusi juu ya kuwabaini wahalifu.

20210829_095038.jpg
20230517_231405.jpg
1649840785448.jpg
20220125_194452.jpg
 
Kijana wa mwenyekiti wa kijiji kaua kondoo wa jirani unadhani mwenyekiti atasema kuna uhalifu umefanyika? Na sheria za kijiji zifuatwe ikiwa mwenyekiti mwenyewe alikuwa na wivu kuona kundoo wa jirani wanavutia?

Itafanyikq endapo jirani akipewa wenyekiti wa kijiji pia akizishinda hila za ukoo wa mwenyekiti wa kijiji wa leo.
 
1. Kuna mambo ambayo, kwa sababu zake yenyewe, serikali huona kuwa kuyaweka wazi kutaleta athari kubwa zaidi kuliko kama yangebakia tu sirini kama yalivyo. Na wakati mwingine yaweza kuwa hata haihusiki nayo.

2. Mo anaweza kuwa anawafahamu waliomteka lakini hawezi kuwataja pamoja na utajiri wake wote. Jiulize ni kwa nini 😳

3. Serikali nyingi hapa duniani zina tabia ya kuumiza raia wake ikiwemo kuua - kwa uwazi na kwa siri.

4. Na kila serikali ina mifumo yake ya kujilinda na kulindana. Vinginevyo isingeweza kutawala!

5. Ukweli na haki hata hivyo vina tabia ya kucheleweshwa tu lakini daima siku moja huchomoza.

6. Hata katika haya matukio siku moja ukweli utajulikana tu baada ya wahusika kuondoka katika mfumo; au mfumo wenyewe kubadilika.

7. Haki iliyocheleweshwa ni haki iliyopotea! 🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
 
Watanzania mwenzangu,

Nawasalimu.

Kwanza nilipongeze JESHI letu la POLISI kwa baadhi ya kazi zake nzuri na pia nitoe masikitiko yangu juu ya baadhi ya Matukio ya muda mrefu ambayo pamoja na INTELEJINSIA yake LIMESHINDWA kutupa MAJIBU WATANZANIA.

Mambo ambayo JESHI letu yanaonekana LIMESHINDWA kabisa ni pamoja na:

1. WALIOMTEKA MO DEWJI
2. WALIOMPIGA RISASI TUNDU LUSSU
3. ALIPO BEN SAANANE
4. LIYEMPIGA RISASI BINTI AKWILINA

Mambo haya yanafikirisha sana kwani ndugu na Jamaa wanatamani kuwajua na kukamatwa kwa Waliofanya huu UHALIFU kwa NDUGU zao ili HAKI ya WAPENDWA wao iweze kupatikana.

Niliamini kama JESHI letu limeshindwa kuwapata na kuwakamata WAHUSIKA kwanini LISIOMBE USAIDIZI wa Kitalaamu kutoka NJE ili kuwabaini WAHUSIKA?

Naamini JESHI letu lina MAHUSIANO Mazuri na MASHIRIKA ya KIJASUSI juu ya Kuwabaini WAHALIFU.

View attachment 2715944View attachment 2715946View attachment 2715949View attachment 2715950
Wahalifu hao wako madarakani, siku wakiondolewa ndipo itawezekana kuwafikisha katika vyombo huru vya sheria. Kwa sasa hakuna vyombo huru
 
Pascal Mayalla
Du!
P
Mkuu Mr Q , unashangaa nini?.
Tena pia niliuliza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?
P
 
Watanzania mwenzangu,

Nawasalimu.

Kwanza nilipongeze JESHI letu la POLISI kwa baadhi ya kazi zake nzuri na pia nitoe masikitiko yangu juu ya baadhi ya Matukio ya muda mrefu ambayo pamoja na INTELEJINSIA yake LIMESHINDWA kutupa MAJIBU WATANZANIA.
Sio kila kitu tunaweza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?,
Mambo ambayo JESHI letu yanaonekana LIMESHINDWA kabisa ni pamoja na:

1. WALIOMTEKA MO DEWJI
Hawa wanajulikana, Baba Mo, Gulam Dewji alilipa ransom under conditions polisi wasihusishwe, wakamrudisha Mo, na Mo baada ya kurejea hajaripoti chochote polisi na badala yake ni polisi ndio walikwenda kwa Baba Mo na wakakirimiwa...
2. WALIOMPIGA RISASI TUNDU LUSSU
Hawa ni hawajulikani, kwanza tuliwatambua Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana kisha tukajitolea kusaidia Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija
l
3. ALIPO BEN SAANANE
Hili naomba nisilizungumzie zaidi ya kumkumbuka tuu Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...
4. LIYEMPIGA RISASI BINTI AKWILINA
Hapa risasi ilipigwa juu, ikapinda kona na kumfuata Aqulina na kumuua! Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!
Niliamini kama JESHI letu limeshindwa kuwapata na kuwakamata WAHUSIKA kwanini LISIOMBE USAIDIZI wa Kitalaamu kutoka NJE ili kuwabaini WAHUSIKA?

Naamini JESHI letu lina MAHUSIANO Mazuri na MASHIRIKA ya KIJASUSI juu ya Kuwabaini WAHALIFU.
Sio lazima, watu wenye uwezo huo wapo, ni PT kujitokeza kuomba msaada wasaidiwe!.
P
 
Sio kila kitu tunaweza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?,

Hawa wanajulikana, Baba Mo, Gulam Dewji alilipa ransom under conditions polisi wasihusishwe, wakamrudisha Mo, na Mo baada ya kurejea hajaripoti chochote polisi na badala yake ni polisi ndio walikwenda kwa Baba Mo na wakakirimiwa...

Hawa ni hawajulikani, kwanza tuliwatambua Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana kisha tukajitolea kusaidia Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija
l

Hili naomba nisilizungumzie zaidi ya kumkumbuka tuu Waandishi wa Habari na Kupotea/Vifo vya Kutatanisha, Toka Katabalo, Saanane, Gwanda, Mwangosi, Isango. Ni Ama Tuombe Mungu Atunusuru ama...

Hapa risasi ilipigwa juu, ikapinda kona na kumfuata Aqulina na kumuua! Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Sio lazima, watu wenye uwezo huo wapo, ni PT kujitokeza kuomba msaada wasaidiwe!.
P
Kwa akwilina hapo panachekesha na kuhuzunisha mtu asie kuelewa anaweza dhani unaleta mashara 😁
 
Kwa sasa? Labda serikali mpya ndiyo itaweza kufunua siri hizi mbaya. Maana dunia haina siri za kudumu, itajulikana tu waliofanya matukio haya ni kina nani na walitumwa na nani na kwa lengo gani?
 
Back
Top Bottom