Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

Umenena Mkuu.

Barabara zinazokatisha maeneo ya Ubungo zamani zilikuwa zinapitishwa greda na kusawazishwa vizuri kabisa. Toka kijana aingine madarakani huduma hii haijafanyika. Mashimo na madimbwi ya maji yamekuwa kero sana kwa wakazi wa Ubungo. Maji ndio hivyo tena! Mwambieni Mbunge asitusahau kiasi hicho wapiga kura wake! sisi bado tuna mlavu tu!

Ha ha ha !
Wewe kweli m-coconut wa mbunge kijana.
Ni heri wale wamwambiao ukweli ili atatue au asaidie kutatua matatizo kuliko wale hypocrites wanaomwambia mambo yote ni mpango wa magamba kumbe wanamzubaisha tu.
 
Hapo chacha. Lazima ajue kupambanua. Hivi anadhani tutaendelea kuvumilia hivi hadi lini???? yeye aanze sisi tutamaliza; alitupenda akatuomba kura, tulimpenda tukamchagua, akitugeuzia kisogo tutamgeuzia kichwa!
 
Hivi Gaudensia Kabaka ni Mbunge wa Jimbo gani vile? Naomba kukumbushwa. Asije akawa ni Mbunge wa JIMBO LA UPENDELEO.

Inawezekana kabisa anataka kujipima nguvu na Mnyika Ubungo kama yule mwanamama mwenzake Hawa Ng'humbi.

Huyu Gaundesia Kabaka aliyeleta muswaada wa kuondoa FAO la kujitoa angekuwa mtu wa mwisho kabisa kumsema Mnyika.

Tunamsubiri Rorya 2015 tumnyoe baada ya yule STD VII Lameck Kairo kutangaza kutogombea.
 
Ni kweli sakata la maji kwa Jimbo la ubungo inatakiwa mnyika akae meza moja na watendaji wa serikali walitatue kwa kushirikiana
Mnyika inatakiwa auweke pembeni ubunge wake,azungumze na DAWASCO na wadau bila kutoa amri na kuwanyoshea vidole watendaji hao.'
Kimsingi yawezekana anaangushwa kwa maksudi na watendaji wa serikali ya CCM,kwa sababu tu amekuwa akiwa face baadhi viongozi na kuwachana ukweli wao live live.
Mfano.ile kauli ya kwamba rais ni mdhaifu aliyoitoa bungeni,reaction yake yaweza kuwa ni chini kwa chini kama hivi kukwamisha maendeleo yake bungeni ili kwenye uchaguzi ujao wapate pa kusemea.
Pia anachangamoto ya barabara (fedal roads) zinazokutanisha na barabara kuu za rami.Kunauwezekano akaweka nata rafu Rami kwa ajili ya kuondoa kero ya barabara.
Mfano barabara ya Makabe kwenye Wazo hill ni muhimu sana,Kimara kuna barabara nyingi hazieleweki kabias,
Ubungo naona ameanza kuzifanyia kazi.Mfano external road kukutanisha na Ubungo terminal imefumuliwa na inajengwa upya kwa kiwango cha juu.
Otherwise JJM kila raheli jimboni kwako.​
 
Acha kumtisha Mnyika wewe,kuna wabunge kibao ambao hata majimboni hawafiki sembuse kuleta maji!chato wanatumia maji machafu ya ziwa toka uhuru na stil wanamchagua mapadlock,acha fitna kama ni mbunge wako mtafute ukampe maoni yako na namna ya kulitatua!

mweleze bora hata huyu mnyika anaongea na kuinyanyua serikali bungeni..kuna wengine majimboni kwao hawafiki na bungeni bado watoro sa sijui hua wanakuaga wapi
 
Ugonjwa huu umesambaa haraka sana, nasikitika inaelekea 90% ya watanzania wanaugua ugonjwa huu, "Utegemezi". Imefikia mahali hata fikra tunategemea za wengine. Anayekusanya kodi CCM, anayepanga matumizi ya kodi zote ni CCM, anayechagua watendaji wa serikali kusimamia utoaji wa huduma mbalimbali ni CCM, anayetunga sera za kuongoza nchi ni CCM, lakini huyu mwenye akili nyingi anamshambulia mnyika in personal. Tena kwa kufuata kauli ya mtu aliyeamua kutowajibika na kucheza mchezo mchafu wa siasa waziri Kabaka!!!!!!! Huu uvivu wa kufikiri ndio uliotufikisha kwenye hii hali mbovu ya uchumi, tunakwepa kuwajibisha wazembe tunashambulia wachapakazi. Hizi ni sifa ya nchi ya majungu. Kabla hujashambulia kwanza jiridhishe na mada yako, kazi za mbunge ni zipi? Je, ni kuchimba visima, kuweka nguzo za umeme, kusambaza mabomba, kujenga viwanda, kutengeneza ajira, kutoa mikopo na mambo kama hayo? Tuache fikra mgando tujitambue. Tukiendelea na upuuzi huu itafika wakati tutataka mbunge aje kutufulia chupi.
 
Basically this is desicated hot air that lacks objective substance.
Kama mawazo ya mtoa hoja ni haya basi sioni faida ya mbunge wa upinzani- waachieni CCM wafanye kazi.
 
Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi.

Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo.

Waziri Kabaka , Waziri wa Kazi na Ajira, amemrushia madongo mazito Mbunge John Mnyika kwa kushindwa kwake "kuona ndani" katika kulitatua tatizo hilo. (ref Mwananchi 6/11/2012, pg 8)

Waziri Kabaka amedai kuwa Mnyika amekuwa akitumia muda mwingi katika siasa za Bunge kuliko kutatua matatizo ya wananchi wa Ubungo.

Katika kusaidia kutatua matatizo ya Ubungo Waziri Kabaka ameahidi kumwona waziri mwenziwe wa Maji na ili alitazame tatizo la maji Ubungo na kulitatua.

Anachosema Waziri Kabaka kina mantiki kubwa, Mnyika inabidi ajipange na kuwa na uhusiano mzuri na "magamba" wanaoendesha wizara zinazomgusa kiutendaji jimboni kwake.

Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.

Hapo kwenye RED unamaanisha nini? hivi mbunge hadi umpigie magoti waziri ndo matatizo ya wananchi yatatuliwe? Hoja yako haina msingi na hii inaonyesha jinsi serikali hii ilivyo dhaifu kiutendaji. Kama mipango mizuri imepangwa juu ya utatuzi wa matatizo ya wananchi kwa nini isitekelezwe bila kufuatana fuatana? na kamwe Mnyika hawezi kuonekana kikwazo katika maendeleo ya wana Ubongo kwani mipango yake ya maendeleo ipo tatizo serikali ya CCM haitekelezi sababu tu Jimbo lina mbunge wa CDM.
 
Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi.

Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo.

Waziri Kabaka , Waziri wa Kazi na Ajira, amemrushia madongo mazito Mbunge John Mnyika kwa kushindwa kwake "kuona ndani" katika kulitatua tatizo hilo. (ref Mwananchi 6/11/2012, pg 8)

Waziri Kabaka amedai kuwa Mnyika amekuwa akitumia muda mwingi katika siasa za Bunge kuliko kutatua matatizo ya wananchi wa Ubungo.

Katika kusaidia kutatua matatizo ya Ubungo Waziri Kabaka ameahidi kumwona waziri mwenziwe wa Maji na ili alitazame tatizo la maji Ubungo na kulitatua.

Anachosema Waziri Kabaka kina mantiki kubwa, Mnyika inabidi ajipange na kuwa na uhusiano mzuri na "magamba" wanaoendesha wizara zinazomgusa kiutendaji jimboni kwake.

Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.
unaonesha ulivyo mvivu wa kufikiri...ulisha muona mnyika akipita mitaa ya ubungo akiomba kodi? mnyika amekuwa baressa wa kuamka asubuhi nakuwaletea maji? kazi ya mnyika ni kwenda bungeni kutoa malalamiko ya wana ubungo kisha kumsii waziri husika kutatua hilo tatizo...we unamlalamikia mnyika badala ya kujilalamikia wewe kwa kuchagua dhaifu kukalia kiti??? elimika kwanza ndo uje jF
 
wakati ambapo Gamba EL aliposema ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiri kulipuka,Kabaka kutoka Gamba Party aliita waandishi wa habari kupinga kauli hiyo japo Mkuu wa Magamba alikubaliana nayo.Mtu mzima ataona kuwa kama KWA MIAKA 50 hata majimya kunywa ni suala la kumtishia Mbunge JJ Mnyika kwa nini kwa mantiki hiyo isiwe agenda ya kuitoa CCM madarakani kwa kuthubutu kushindwa kuwapa wananchi maji kwa miaka hii yote,tukiwapa mingine 50 watawapa Watanzania MAJI SAFI NA SALAMA?je wewe mtoa mada una hakika wewe ni Mtanzania au m-Ubungo ambaye huoni tatizo ni la nchi nzima hii takribani mikoa yote wilaya zote hadithi ni hii hii?Kwa nini Dr JM Kikwete asiambiwe kuwa kama hayapatikani CCM haina kura ya Urais 2015?Huyo Keenja kakaa miaka 10 alitatua kero ipi hasa Ubungo?Hii ndugu mtoa mada uliyoileta siyo tathmini ni uchimvi!
 
Ongeeeeni weeee Lakini mimi Mkazi wa Ubungo naona kuna Ubora wa Upatikanaji wa Maji Ubungo kuliko kipindi chochote kile. Pigeni Kelele, pigeni Porojo, Pigeni Propaganda Kadi yangu ya Kupiga Kura Nimemkabidhi Mnyika akitaka awapigie yeye Kura CCM

You know what I'm Say
 
unaonesha ulivyo mvivu wa kufikiri...ulisha muona mnyika akipita mitaa ya ubungo akiomba kodi? mnyika amekuwa baressa wa kuamka asubuhi nakuwaletea maji? kazi ya mnyika ni kwenda bungeni kutoa malalamiko ya wana ubungo kisha kumsii waziri husika kutatua hilo tatizo...we unamlalamikia mnyika badala ya kujilalamikia wewe kwa kuchagua dhaifu kukalia kiti??? elimika kwanza ndo uje jF

Mkuu inelekea "umeamka nao", umeshinda na hiyo hang over na pengine utalala nao, malamiko si yangu , ni ya Waziri niliyemnukuu katka gazeti tajwa.
Kama ulipita darasa la saba nitashangaa maana husomi mada na ukaielewa.
Nna kwa vyovyote nikupoteza muda kujaribu kukuelimisha.
 
Ongeeeeni weeee Lakini mimi Mkazi wa Ubungo naona kuna Ubora wa Upatikanaji wa Maji Ubungo kuliko kipindi chochote kile. Pigeni Kelele, pigeni Porojo, Pigeni Propaganda Kadi yangu ya Kupiga Kura Nimemkabidhi Mnyika akitaka awapigie yeye Kura CCM

You know what I'm Say
Hilo nalo neno!!
 
Kuna tofauti kubwa kati ya
mwanasiasa na kiongozi jamaa anaweza siasa but hawezi kuongoza wenye
akili watanielewa wasio na akili watanitukana

kaka njoo hapa kimara stendi ubwabwaje huu utumbo wako afu utajua prezidaa wa ubungo ni nani!
 
wakati ambapo Gamba EL
aliposema ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiri kulipuka,Kabaka kutoka
Gamba Party aliita waandishi wa habari kupinga kauli hiyo japo Mkuu wa
Magamba alikubaliana nayo.Mtu mzima ataona kuwa kama KWA MIAKA 50 hata
majimya kunywa ni suala la kumtishia Mbunge JJ Mnyika kwa nini kwa
mantiki hiyo isiwe agenda ya kuitoa CCM madarakani kwa kuthubutu
kushindwa kuwapa wananchi maji kwa miaka hii yote,tukiwapa mingine 50
watawapa Watanzania MAJI SAFI NA SALAMA?je wewe mtoa mada una hakika
wewe ni Mtanzania au m-Ubungo ambaye huoni tatizo ni la nchi nzima hii
takribani mikoa yote wilaya zote hadithi ni hii hii?Kwa nini Dr JM
Kikwete asiambiwe kuwa kama hayapatikani CCM haina kura ya Urais
2015?Huyo Keenja kakaa miaka 10 alitatua kero ipi hasa Ubungo?Hii ndugu
mtoa mada uliyoileta siyo tathmini ni uchimvi!

afu una akili wewe!bila shaka muubungo mwenzetu!
 
Hivi Gaudensia Kabaka ni
Mbunge wa Jimbo gani vile? Naomba kukumbushwa. Asije akawa ni Mbunge wa
JIMBO LA UPENDELEO.

Inawezekana kabisa anataka kujipima nguvu na Mnyika Ubungo kama yule
mwanamama mwenzake Hawa Ng'humbi.

Huyu Gaundesia Kabaka aliyeleta muswaada wa kuondoa FAO la kujitoa
angekuwa mtu wa mwisho kabisa kumsema Mnyika.

Tunamsubiri Rorya 2015 tumnyoe baada ya yule STD VII Lameck Kairo
kutangaza kutogombea.

umesema Gaudensia nani?!mh!ubungo kunaongezeka VIBAKA ngoja tumstue Mnyika wetu
 
Mkuu Mwita Maranya kama Kimbunga hampendi Mnyika kabisa, akiiona hii thread atakesha nayo hata wiki nzima.....

Mkuu Precise pangolin Mnyika ni Mbunge wangu na mimi ni mdau mkuu sana wa maendeleo huko Ubungo. Kama kuna tatizo ni lazima tulisema na hii ni kumsaidia Mnyika aweze kudumu Ubungo.

Ambao hammpendi ndio mnataka kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Wengine tunazijua fitina za kisiasa huko Ubungo na tunamshitua Mnyika apige kelele lakini ninyi mnaona kama hatumpendi.

Yuko vizuri sana katika masuala ya kitaifa ila pia atupe mamcho jimboni, kilio ni kikubwa!
 
Mkuu Kimbunga, this is the same oldest story.
Ukimsikia Mnyika ametajwa kwa jambo negative unakuwa sensitive sana kuweka comments zako lakini kwa yale positive hutii maguu kabisa.
Kama unataka kugombea jimbo la Ubungo kuwa muwazi mkuu unaruhusiwa lakini usijaribu kutumia mgongo wa Mnyika kutafuta huruma ya wapiga kura tena kwa habari za kutunga na upotoshaji.

Na kwa hakika mambo aliyoyafanya John Mnyika kwa wananchi wa Ubungo kwa kipindi kifupi cha miaka miwili ni makubwa kuliko yaliyofanywa na wabunge wenu wote wa magamba tangu kuanzishwa kwa jimbo la ubungo......

Mkuu Mwita Maranya mimi sijawahi kuanzisha thread juu ya Jimbo la Ubungo na Mnyika. Pia mkuu mimi sina nia wala ndoto ya kugombea ubunge ubungo! Mimi ni technocrat siasa za majukwaa siziwezi hata kidogo.

Ila ni wajibu wangu kumkumbusha Mnyika juu ya fitina za kisiasa Ubungo. Nipo Ubungo miaka mingi na nazijua siasa zake. Nakumbuka tulivyomtoa Ngula tukamuingiza Dr. Lamwai. Kumbuka kuwa Ubungo (achilia mbali Keenja na uchakachuaji) ni Kama Jimbo la huko kwenu Musoma Mjini (mtu mmoja kipindi kimoja).
 
Kuna principle moja mnaitumia sana akina Kimbunga, kila Mara John akiwa-hit kwenye masuala mengi makubwa ya kitaifa, masuala mazito kama la mafuta Jana Bungeni na masuala ya ufisadi mkubwa unaoathiri wananchi wote, wakiwemo wa Ubungo, mnaingia kwenye mitandao humu kusema maji maji maji na barabara, as if hamjui kuwa serikali inawajibika kufanya kazi hizo.......

Mkuu Tumaini Makene mimi si mwandishi na hata hilo gazeti huwa silisomi kabisaaaa. Mkuu naona unafuatilia post zangu hasa kuhusu Ubungo na Mnyika.

Naomba nikuambie kuwa mimi ni Mkazi wa jimbo la Ubungo na ni mshabiki wa Mnyika na pia nikuambie kwa uwazi kabisa kwamba nilimpigia kura yeye pamoja na Diwani Manota.

Nikuambie pia kwamba nafanya kazi kwa ukaribu sana na Diwani Manota katika kujiletea Maendeleo maeneo ya Kimara.

Sina kinyongo na John Mnyika ila tu mimi nataka kumkumbusha wajibu wake kwa wapiga kura wake. Anatekeleza vyema sana wajibu wake kwa Watanzania kwa ujumla wake lakini anasahau Nyumbani.

Kwa upande wa Barabara CCM wamejipiga kitanzi kazi ya Mnyika ni kukivuta tu ili watekeleze ama wajinyonge. Ukisoma Ilani ya CCM ya mwaka 2010 utaona ahadi zifuatazo:

  • Kupanua mtandao wa Barabara za jiji kwa kujenga na kukarabati barabara zifuatazo:
    • Mbezi (Morogoro Road) - Malambamawili - Kinyerezi
    • Tegeta kibaoni - Wazo - Goba - Mbezi mwisho
    • Kimara Baruti - Msewe - Changanyikeni
    • Kimara Kilungule - External - Mandela Road
    • Tabata Dampo - Kigogo

Hizo zote ziko Jimbo la Ubungo. Kwa hiyo Mnyika akisimamia hizi zikatekelezwa hatakuwa na sababu ya kupiga Kampeni 2015.

Mkiendelea kumpigia makofi na kusema tutembelee Blog yake bila barabara na maji Ubungo matokeo yake yataonekana 2015
.
 
Back
Top Bottom