Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

..........Rais dhaifu sawa, muongozo wa spika sawa, EPA sawa, Taarifa SPIKA sawa,sifuti kauli sawa......lakini Ubungo hakuna maji........... 2015 ATAJINYA....
 
..........Rais dhaifu sawa, muongozo wa spika sawa, EPA sawa, Taarifa SPIKA sawa,sifuti kauli sawa......lakini Ubungo hakuna maji........... 2015 ATAJINYA....
kwani nani alikuambia kuwa Mnyika anataka Ubunge Ubungo 2015. Wapiilitamkwa kuwa kazi ya Mbunge bi kuleta maji? Kama Mbunge ataleta maji ya nini kuwa na Wizara ya maji? Ndio maana Mnyika anachapa kazi za kibunge kwa mujibu wa ibara 63 "Kuishauri na kuisimamia Serikali"
 
kwani nani alikuambia kuwa mnyika anataka ubunge ubungo 2015. Wapiilitamkwa kuwa kazi ya mbunge bi kuleta maji? Kama mbunge ataleta maji ya nini kuwa na wizara ya maji? Ndio maana mnyika anachapa kazi za kibunge kwa mujibu wa ibara 63 "kuishauri na kuisimamia serikali"

.......hata kama anataka uraisi lakini ubungo hakuna maji..................narudia tena atajinya...2015
 
Kwa upande wa Barabara CCM wamejipiga kitanzi kazi ya Mnyika ni kukivuta tu ili watekeleze ama wajinyonge. Ukisoma Ilani ya CCM ya mwaka 2010 utaona ahadi zifuatazo:

  • Kupanua mtandao wa Barabara za jiji kwa kujenga na kukarabati barabara zifuatazo:
    • Mbezi (Morogoro Road) - Malambamawili - Kinyerezi
    • Tegeta kibaoni - Wazo - Goba - Mbezi mwisho
    • Kimara Baruti - Msewe - Changanyikeni
    • Kimara Kilungule - External - Mandela Road
    • Tabata Dampo - Kigogo
Mkuu Kimbunga unaonaje ukimkumbusha raisi wa serikali ya JMT ambaye pia ni mwenyekiti wa magamba atekeleze ahadi za barabara jimboni kwenu kama alivyoahidi katika ilani yao ya uchaguzi? Yani unatambua kwamba ccm waliahidi kujenga hizo barabara lakini ghafla unageuka na kumtaka Mnyika azijenge?

Mnyika anafanya kazi yake vizuri sana ya kuisimamia na kuishauri serikali na kuikumbusha kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni Ubungo na jiji la Dsm kwa ujumla. Alipozindua mradi wa maji hivi karibuni akiwa na waziri wa maji Prof. Maghembe sikukuona ukitoa comment yoyote kuhusu jitihada hizo isipokuwa unasubiri tu ianzishwe hoja ya kumpinga ndipo unaingia miguu miwili.

Kama kweli unashirikiana na diwani manota na una nia nzuri na Mnyika, mbona hata siku moja hutoi comments za kuelezea mazuri anayofanya? au wewe unayaona ya upande mmoja tu?
 
Last edited by a moderator:
..........Rais dhaifu
sawa, muongozo wa spika sawa, EPA sawa, Taarifa SPIKA sawa,sifuti kauli
sawa......lakini Ubungo hakuna maji........... 2015 ATAJINYA.....

Ndio sababu tunaiondoa CCM 2015 na kuipa CHADEMA ili ituletee maji.Ni suala la serikali si mbunge.Umefika form iv wewe?
 
Mnyika kama mnyika anajitahidi sana, ila magamba wanajaribu kumwaribia aonekane si kitu.binafsi amekuwa akipiga kelele sana juu ya maji Ubungo
 
bunge imekwepa kujadili hoja binafsi ya mbunge wa Ubungo John Mnyika aliwasilisha tarehe 25/10/2012 kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007 Kanuni 54 (1), (2) na (3) na badala yake, spika amempa nafasi ya kuwasilisha hoja ya serikali kuhusu maji dar es salaam.

hii ni kutokana na serikali kumuwekea vikwazo mnyika asionekane kuwa anafuatilia matatizo ya maji kwa karibu. na ndio maana leo ameomba muongozo wa spika kwanini hoja yake haija jadiliwa, na hata hiyo hoja ya serikali haijazungumzia kuhusu fedha zilizotumika kutandaza mabomba ya mchina jijijni dsm ambayo hayatoi maji, yaliyogharimu zaidi ya 268b.

wakati kwenye hoja yake binafsi suala la fedha zilizopotea za mabomba ya mchina ipo na mambo mengine kama kuhusu kauli za kupishana ya waziri wa maji na naibu wake. na pia amehoji kama hoja yake binafsi ya kuhusu maji jimbo la ubungo na dsm pia itajadiliwa au la? m/kiti wa bunge hakutoa jibu.
 
Wanatuchukulia poa. Nchi hii ni yetu wote. Mnyika waambie hao kwamba cheo ni dhamana.
 
Ukweli ni kwamba watendaji wengi wa serikali wamelala na pale wanapozinduka huamkia kwenye maslahi binafsi na siyo wajibu wao kwa taifa. Akina Mnyika msichoke mpaka kieleweke.
 
Huyu Jeniste Mhagama naye ni mburula kama Anne Senkyu vere mache!
 
Nitajie mmoja atakae ishi milele... Acha kufikiri kwa tumbo kaka

Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi.

Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo.

Waziri Kabaka , Waziri wa Kazi na Ajira, amemrushia madongo mazito Mbunge John Mnyika kwa kushindwa kwake "kuona ndani" katika kulitatua tatizo hilo. (ref Mwananchi 6/11/2012, pg 8)

Waziri Kabaka amedai kuwa Mnyika amekuwa akitumia muda mwingi katika siasa za Bunge kuliko kutatua matatizo ya wananchi wa Ubungo.

Katika kusaidia kutatua matatizo ya Ubungo Waziri Kabaka ameahidi kumwona waziri mwenziwe wa Maji na ili alitazame tatizo la maji Ubungo na kulitatua.

Anachosema Waziri Kabaka kina mantiki kubwa, Mnyika inabidi ajipange na kuwa na uhusiano mzuri na "magamba" wanaoendesha wizara zinazomgusa kiutendaji jimboni kwake.

Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.
 
Wafanye wafanyalo jimbo la Ubungo ni la Mnyika.(2015) Maji yawepo Maji yasiwepo.
 
Nitajie mmoja atakae ishi milele... Acha kufikiri kwa tumbo kaka

Changamsha ubongo wako mzee, na si kila kitu pana matatizo ya tumbo kama mawazo yako yalivyojikita.

Watu wanalikodolea macho jimbo hilo, matatizo yaliyotajwa ni mtaji tosha wa kisiasa.
 
kabla ya kuanza kuchangia hoja hii ni bora ukafahamu majukumu ya mbunge ambayo ni;
1-kwa taifa lake
2-kwa jimbo lake
3- kwake yeye mwenyewe
ukiangalia majukumu haya yote mnyika anayafanya, kumbuka si jukumu la mbunge kuleta maji, shule,umeme na huduma nyingine bungeni, hiyo ni kazi ya serikali. jukumu la mbunge ni kukusanya na kuziwasilisha kero za wananchi bungeni. swali la kujiuliza ni je? mnyika hajafanya hayo yote?
 
Kama CCM ambayo ipo madarakani kwa 50+wameshindwa kutatua tatizo la maji, mnyika mnamwonea tu.
 
Unategemea Mnyika na Mtemvu wakiwasilisha shida zao kwa Waziri wa Maji nani atasikilizwa haraka acha ulumbukeni gamba wewe
Huyu waziri akili yake ni ndogo sana,myika siyo chama tawala na myika hana mafungu, kwakuwa yeye ni waziri na yuko kwenye serikali angechukua hatua ya kuiambia serikali yake ilete pesa na kuleta maji. anajua kuwa kila kitu cha seriali kinaenda kwa badgeti je kuna pesa iliyotengwa kwaajiri hiyo au ameamua kuongea akidhamni kwamba chama cha ssm ni chamapinani.
 
[/LIST]
Mkuu Kimbunga unaonaje ukimkumbusha raisi wa serikali ya JMT ambaye pia ni mwenyekiti wa magamba atekeleze ahadi za barabara jimboni kwenu kama alivyoahidi katika ilani yao ya uchaguzi? Yani unatambua kwamba ccm waliahidi kujenga hizo barabara lakini ghafla unageuka na kumtaka Mnyika azijenge?

Mnyika anafanya kazi yake vizuri sana ya kuisimamia na kuishauri serikali na kuikumbusha kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni Ubungo na jiji la Dsm kwa ujumla. Alipozindua mradi wa maji hivi karibuni akiwa na waziri wa maji Prof. Maghembe sikukuona ukitoa comment yoyote kuhusu jitihada hizo isipokuwa unasubiri tu ianzishwe hoja ya kumpinga ndipo unaingia miguu miwili.

Kama kweli unashirikiana na diwani manota na una nia nzuri na Mnyika, mbona hata siku moja hutoi comments za kuelezea mazuri anayofanya? au wewe unayaona ya upande mmoja tu?

Mkuu Mwita Maranya wapi nimesema Mnyika ajenge mimi nasema aisimamie serikali ya CCM izijenge. Kama anavyosimamia inajenga daraja la External. Mimi niseme Mnyika ajenge barabara pesa hata za kujenga Km 1 hawezi kuwa nazo!
 
Last edited by a moderator:
Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi.

Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo.

Waziri Kabaka , Waziri wa Kazi na Ajira, amemrushia madongo mazito Mbunge John Mnyika kwa kushindwa kwake "kuona ndani" katika kulitatua tatizo hilo. (ref Mwananchi 6/11/2012, pg 8)

Waziri Kabaka amedai kuwa Mnyika amekuwa akitumia muda mwingi katika siasa za Bunge kuliko kutatua matatizo ya wananchi wa Ubungo.

Katika kusaidia kutatua matatizo ya Ubungo Waziri Kabaka ameahidi kumwona waziri mwenziwe wa Maji na ili alitazame tatizo la maji Ubungo na kulitatua.

Anachosema Waziri Kabaka kina mantiki kubwa, Mnyika inabidi ajipange na kuwa na uhusiano mzuri na "magamba" wanaoendesha wizara zinazomgusa kiutendaji jimboni kwake.

Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.
Naishi ubungo kibangu miaka miwili sasa na sijawahi kununua maji,maji yanatoka mara 2 hadi 3 kwa wiki na yanatosheleza kabisa kwani tunayahifadhi.
Maeneo ambayo wakazi wengi hawapati maji ni maeneo ambayo hata miundo mbinu haijawahi kuwepo tangu uhuru na tangu mudawote tulipokuwa tunaongozwa na CCM,maeneo hayo baadhi ni makoka,makabe,msakuzi n.k ambayo siyakumbuki.
John Mnyika amefanya jitihada kubwa sana kwenye suala la maji kwa maeneo ambayo miundo mbinu ilikuwepo na hadi sasa harakati zake nazikubali.
Mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni.

TAARIFA TU:
ijumaa nimepata maji,jumane na leo jumatano ya trh 7/11/2012
 
kabla ya kuanza kuchangia hoja hii ni bora ukafahamu majukumu ya mbunge ambayo ni;
1-kwa taifa lake
2-kwa jimbo lake
3- kwake yeye mwenyewe
ukiangalia majukumu haya yote mnyika anayafanya, kumbuka si jukumu la mbunge kuleta maji, shule,umeme na huduma nyingine bungeni, hiyo ni kazi ya serikali. jukumu la mbunge ni kukusanya na kuziwasilisha kero za wananchi bungeni. swali la kujiuliza ni je? mnyika hajafanya hayo yote?
unajitia uchiz au unajifanya haujui ili kukwepa kujibu hoja?
wakati anatoa ahadi hakujua hilo?
 
Mkuu Tumaini Makene mimi si mwandishi na hata hilo gazeti huwa silisomi kabisaaaa. Mkuu naona unafuatilia post zangu hasa kuhusu Ubungo na Mnyika.

Naomba nikuambie kuwa mimi ni Mkazi wa jimbo la Ubungo na ni mshabiki wa Mnyika na pia nikuambie kwa uwazi kabisa kwamba nilimpigia kura yeye pamoja na Diwani Manota.

Nikuambie pia kwamba nafanya kazi kwa ukaribu sana na Diwani Manota katika kujiletea Maendeleo maeneo ya Kimara.

Sina kinyongo na John Mnyika ila tu mimi nataka kumkumbusha wajibu wake kwa wapiga kura wake. Anatekeleza vyema sana wajibu wake kwa Watanzania kwa ujumla wake lakini anasahau Nyumbani.

Kwa upande wa Barabara CCM wamejipiga kitanzi kazi ya Mnyika ni kukivuta tu ili watekeleze ama wajinyonge. Ukisoma Ilani ya CCM ya mwaka 2010 utaona ahadi zifuatazo:

  • Kupanua mtandao wa Barabara za jiji kwa kujenga na kukarabati barabara zifuatazo:
    • Mbezi (Morogoro Road) - Malambamawili - Kinyerezi
    • Tegeta kibaoni - Wazo - Goba - Mbezi mwisho
    • Kimara Baruti - Msewe - Changanyikeni
    • Kimara Kilungule - External - Mandela Road
    • Tabata Dampo - Kigogo

Hizo zote ziko Jimbo la Ubungo. Kwa hiyo Mnyika akisimamia hizi zikatekelezwa hatakuwa na sababu ya kupiga Kampeni 2015.

Mkiendelea kumpigia makofi na kusema tutembelee Blog yake bila barabara na maji Ubungo matokeo yake yataonekana 2015
.

Kimbunga ukiamua kutoelewa hautaelewa, ofcourse. Kama pamoja na uelewe wako huwezi kuona namna ambavyo John anapiga kelele Bungeni juu ya matatizo ya Ubungo, hasa maji na barabara na mambo mengine na namna ambavyo serikali inashindwa au haitaki kuwajibika kwa uplands wake, basi nafikiri tatizo lako ni kubwa zaidi.

Ndiyo maana nikakwambia, wewe si layman, mpinge kwa facts, pata taarifa za utendaji wake kisha umpinge kwa facts kuwa mrejesho wa kile alichofanya anatudanganya.

Nimekuuliza wajibu wa Mbunge ni upi na serikali ni upi, badala yake umeendeleza hoja ile ile ya mwandishi Yule. Na hii ni lugha ya CCM kwa Jimbo la Ubungo eti John ni Mbunge wa kitaifa, maana yake nini eti wanataka kuonesha kuwa hafanyi lolote jimboni kwake. Mbona kuna watu aw Ubungo hapa hapa wanaona ambacho wewe umeamua kutokiona kwa makusudi. Mara kwa mara sana huwa unaifahamu kwenye mgongo wa kuwa ulimpigia kura John na Manota. Kama hivyo mbona unawahukumu kwa maneno.

Leo tu, serikali wameamua ku-hijack hoja yake ya maji Mkoa wa Dar es Salaam, wakitaka asiwabane kesho, hivyo Waziri wa Maji akaamua kuwasilisha kauli ya serikali Leo Bungeni kuzungumzia yoooooooote ambayo alitaka kuyasema kupitia hoja yake kesho.
 
Back
Top Bottom