Mmeanza tena?
Napenda niwahakikishie kuwa, mbinu na chokochoko mnazozifanya dhidi ya Mh Mbunge wa Ubungo - John John Mnyika - hazitafua dafu.
Kila siku huwa mnakuja na mada za kumshambulia Mnyika; kulaumu kuhusu maji Ubungo. Niseme tu kuwa, tangu nianze kuishi Ubungo (Mwaka wa 9 naenda wa 10 sasa), sijawahi kumwona Mbunge effective na efficient kama Mnyika.
Huyu ni mwakilishi wa wana Ubungo si tu bungeni, bali katika ngazi ya Jimbo. Na niseme wazi, sikuwahi kuona maji ya bomba yakitoka hapa Ubungo, zaidi ya kutegemea maji ya visimani kule kwenye kanisa la KKKT au kisima cha Jumuiya Ubungo NHC ambacho hata hivyo hakikuwa na uwezo wa kukidhi matakwa na mahitaji ya maji Ubungo. Lakini sasa maji yanatoka. Sawa, si kila siku lakini kwa maeneo yetu sisi huwa yanatoka Jumanne, Alhamisi na Jumamosi. Fair enough. Na watu wa Msewe/Kibangu kama wako apa waseme..juzi Jumapili nilipita mitaa ya kwenu; mbona maji yalikuwa yanatoka?
Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
Mtasubiri sana 2015 mkidhani kuwa mtakomboa Jimbo...Sahauni.
Kwa maelezo zaidi tembelea
JOHN MNYIKA usuuzike na roho yako.....