Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

Kinachotakiwa ni mikakati endelevu ya kuondoa tatizo la maji .
Kumlaumu Kabaka ni kama kuvunja redio inokutangazia habari za msiba!.....

Kwahiyo unataka kusema serikali ya CCM haina mikakati endelevu ya kuondoa tatizo la maji ubungo? Maana sera ya maji inayotekelezwa ni ya serikali ya CCM siyo ya CHADEMA! Unapoleta hoja uwe umefanya utafiti kwanza!
 
Kwahiyo unataka kusema serikali ya CCM haina mikakati endelevu ya kuondoa tatizo la maji ubungo? Maana sera ya maji inayotekelezwa ni ya serikali ya CCM siyo ya CHADEMA! Unapoleta hoja uwe umefanya utafiti kwanza!....

Mkuu mbona unakuwa small time thinker, kwa hiyo anawakilisha wananchi ili afanye nini kama si kusaidia kutatua kero zao.

Wenziwe wanalitamani jimbo hilo na kwa kauli hizi tunazozisikia matatizo anabwagiwa incumbent ili suala liwe liability kwake 2015.
 
Mnyika mzigo anapiga kwa uwezo wake ; Kumbuka ana miaka 2 tu tangu aanze. Huyo Kabaka ana lake tu.
JOHN MNYIKA
 
Nina mambo matatu:

Mosi, Mnyika ni mbunge makini na anayejitu. hao watu wa Serikali anawasumbua ndio maana wanamshambulia
Pili, Kero ya maji ni moja ya ahadi kubwa za Kikwete kwa watu wa Dar es Salaam katika uchaguzi mkuu hajatekeleza.
Tatu, Serikali (aliyomo kabaka) ndiyo inayokusanya kodi, haitaki kuzirudisha kwa wananchi kwa njia ya huduma kama za maji, mnataka Mnyika zaidi ya kuwabana kila kona ili watekeleze ahadi, afanyeje?
 
MSITUCHANGANYE WATU WA UBUNGO MNYIKA NI MSAADA KWA TAIFA ZIMA, MBONA MLIKUWA MKICHAGUA MAFISADI MDA WOTE NA YAKIISHIA KCHAPA USINGIZI AU NDO MMESHAANDAA FISADI MNATAKA KULIPA JIMBO ILI TUHUMIE WOTE? ACHENI UBINAFSi
 
Unategemea Mnyika na Mtemvu wakiwasilisha shida zao kwa Waziri wa Maji nani atasikilizwa haraka acha ulumbukeni gamba wewe

Magamba bwana, watu wote wenye akili zao wanajua ya kuwa ukiwa upinzani basi utapata vikwazo wee hata katika masuala ya maendeleo ya nchi ili tu uonekane mbovu, wazalendo katika nchi hii wamebaki wachache sana wengine wote ni mbwa wa kuchora - hawang'ati.
Mnika ni kijana shupavu na muelewa sana, anajitahidi kuleta mabadiliko lakini vikwazo kutoka kwa magamba ndio tatizo lakini tutafika kwani hakuna refu lisilo na mwisho.
"Aluta continua"
 
Huyu mwalimu kabaka ni kilaza wa kiwango cha juu,hakumbuki ni hivi juzi tu amefanya madudu kwnye fao la kujito hadi bosi wake alipoingilia kati kwa presha ya wafanyakazi wa migodini,anapata wapi moral authority ya kumnanga Mnyika?Kwanza anaijua ladha ya kuwa mbunge wa jimbo au anaitamani Ubungo 2015,Nakumbuka alipokuwa naibu waziri wa elimu,pale wanafunzi walipokuwa katika mgomo kwa sababu boom halitoshi,vongozi wa DARUSO akina Mtatiro walipomwendea kuomba aingilie kati yeye alisema ataomba wanafunzi wapewe mahindi ya msaada kuweza kukabiliana na njaa,huyu mama ana uwezo mdogo sana wa kufikri!
 
Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi.

Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo

Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.....

Wapiga kura wa Ubungo wanaelewa fika CDM na Mnyika hawakusanyi kodi lakini wanatumia hoja za msingi kupambana na tatizo hilo,ila tahadhari kwa serikali ya CCM kupitia rais wake,ni udhaifu kuinyima Ubungo maji ilihali pato kubwa linatokana na kodi za wakazi wa jimbo hilo.

Pia Watanzania waishio Ubungo lazima mkumbuke kuwa umahiri na umakini wa Mbunge wenu ndiyo chachu ya maendeleo ya jimbo hilo japokuwa mbinu inayotumiwa na serikali kutokutatua tatizo hilo la maji na barabara ni silaha dhaifu kwa wapinzani hasa ukizingatia wanao kusanya kodi ni serikali,hivyo serikali haina budi kufanya mrejesho wa kodi za wananchi kwa kuwapa maendeleo wananchi wake.

Pia ikumbukwe kuwa Mnyika si bora kiongozi ndo maana alikataa kuhongwa ukuu wa wilaya alipochakachuliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.

Lakini hakurudi nyuma kuwapigania wananchi wake mpaka pale alipopata nafasi tena ya kuchaguliwa,pia mbunge huyu ni mbunge wa Kitaifa haijalishi jimbo lake liko Ubunge.Alichofanya mama Kabaka ni kujibu hoja ya udhaifu wa serikali yake na bunge lao.

Waziri kumtuhumu mbunge kuwa hawasaidii wananchi ni kuwafanya Watanzania wanafikiri kwa kutumia makalio ilihali baraza la mawaziri chini ya mwenyekiti wao rais ndiyo wenye kuweka vipau mbele gani kwa taifa.

Mh. Kabaka tuna kuheshimu kutokana na taaluma yako ya ualimu lakini usipende kuwahada wananchi kwa kutumia taaluma yako ya ualimu ilihali unajua mbunge kama mbunge mwisho wake ni kuilalamikia serikali.


 
Waziri Kabaka kakaa Wizara ya Kazi na Ajira kama mzigo, kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu ya 2002, Wizara za kisekta hutakiwa kuratibu wa survey za kisekta kwa ajli ya nchi kupata takwimu sahihi katika nyanja mabali mbali

Kwa upande wa tatizo nyeti kama ukosefu wa ajira kwa watanzania, Kila baada ya miaka mitano Wizara ya Kazi na Ajira inayoongozwa na Waziri Kabaka hutakiwa kufanya Intergrated Labour Force Survey (ILFS), mfano wa sensa ya masuala ya ajira kwa lengo la kupata takwimu sahihi juu ya

1)Watanzania wangapi wana ajira rasmi 2) Watanzania wasio na ajira rasmi 3) Watanzania wenye ajira zisizokidhi matakwa 4) ukubwa sekta isiyo rasmi 5)Shughuli za kiuchumi zinazotekelezwa na watanzania 6) Ukubwa nguvu ya Tanzania 7) Iwapo vipato vinawiana na mahitaji 8) Watanzania hufanya kazi masaa mangapi na hupata kipato gani kwa masaa hayo 9) Idadi ya watoto wanaotumikishwa n.k


ILFS ya mwisho ilifanyika 2006 na nyingine kutakiwa kufanyika 2011 ili Serikali iweze kuwa takwimu sahihi kuhusu yalliyotajwa hapo juu ili iweze kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo waweze kupanga mipango mbali mbali ya kutengeneza ajira kwa watanznaia.

Cha kushangaza Waziri Kabaka kakaa Wizara ya Kazi na Ajira kama mzigo na ameshindwa kusimamia kufanyika kwa ILFS mwaka 2011, Na hadi sasa tunapokaribia kumaliza mwak 2012 Serikali, Sekta binafsi wabia wa maendeleo n.k wanalazimika kutumia takwimu za Ajira za mwaka 2006.

Mwaka 2006 watoto waliokuwa na miaka 13 mwaka huu ni vijana waliokwisha ingia katika kundi la watu waziama miaka 18 hivyo kuhitaji kuwa na ajira ili waweze kujikimu kimaisha. Uzembe wa mama huyu kushindwa kusimamia kufanyika kwa ILFS mwaka 2001 kunachangia kwa kiwango kikubwa ukosefu wa ajira hapa nchini.



 
Amekuwa anapigana sana na sisi wote ni mashaidi sana na sio mbunge wa ubungo wa tu ila Tanzania tu hivyo mada ya haina mashiko
 
Nataka tu kujua kati ya ubungo ,kinondoni na ukonga ni jimbo lipi linaongoza kwa kero ya maji,maana naona hapa kila siku MNYIKA na MDEE Wanashushiwa sana lawama AS IF wameongoza hapo 20 yrs.
 
Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi. Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo. Waziri Kabaka , Waziri wa Kazi na Ajira, amemrushia madongo mazito Mbunge John Mnyika kwa kushindwa kwake "kuona ndani" katika kulitatua tatizo hilo. (ref Mwananchi 6/11/2012, pg 8) Waziri Kabaka amedai kuwa Mnyika amekuwa akitumia muda mwingi katika siasa za Bunge kuliko kutatua matatizo ya wananchi wa Ubungo. Katika kusaidia kutatua matatizo ya Ubungo Waziri Kabaka ameahidi kumwona waziri mwenziwe wa Maji na ili alitazame tatizo la maji Ubungo na kulitatua. Anachosema Waziri Kabaka kina mantiki kubwa, Mnyika inabidi ajipange na kuwa na uhusiano mzuri na "magamba" wanaoendesha wizara zinazomgusa kiutendaji jimboni kwake. Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.

Umenena Mkuu.

Barabara zinazokatisha maeneo ya Ubungo zamani zilikuwa zinapitishwa greda na kusawazishwa vizuri kabisa. Toka kijana aingine madarakani huduma hii haijafanyika. Mashimo na madimbwi ya maji yamekuwa kero sana kwa wakazi wa Ubungo. Maji ndio hivyo tena! Mwambieni Mbunge asitusahau kiasi hicho wapiga kura wake! sisi bado tuna mlavu tu!
 
Mh Mnyiaka siyo maji tu hata barabara zimekushinda mnapitisha greda bila kifusi wala haina mitaro.Mfano ya riverside mpaka jeshini.Kila mbuge akija anatuuzia maneno muda umeisha.
 
Mkuu wengine tumesema humu weeeee lakini tunaonekana hatumtakii mema Mnyika. Kila siku kauli yangu ni kwamba Mnyika ni mahiri katika kujenga hoja na ni msaada mkubwa sana kwa Taifa hili kwa jinsi anavyojenga hoja za kulitetea. Lakini aangalie tusije kumkosa Ubungo kwa kushindwa kutatua kero za maji na barabara. Hayo matatizo ni makubwa Ubungo na ndiyo yanawaangusha wabunge. Najua kuna mipango na michakato mingi ya kutatua hayo matatizo lakini tukumbuke njaa haina mchakato. Atafanya michakato hadi anaondoka mwenzake anakuja anamalizia mchakato anaibuka bingwa!

Kimbunga kati ya watu wanaokesha usiku na mchana hapa dhidi ya John na Ubungo. Na kwa mujibu wa maoni yako mengi hapa ni kwamba John anapaswa kumaliza matatizo yote ya maji na barabara kwa muda huu wa miaka hii miwili na nusu ambayo yamekuwepo miaka kadhaa, yakilimbikizwa na serikali ya CCM, tena miaka 10 or so ya Keenja. Hayo huwa husemi.

Lakini pia maoni yako huwa yanafanana sana na yale ya mwandishi mmoja wa Jambo Leo aliwahi kuandika tangu John aingie bungeni kama Mbunge wa Ubungo, hajawahi kabisa kuzungumzia suala la maji!!!!!!! Maoni yako juu ya maji na barabara Ubungo huwa yanafanana na mwandishi huyo.

Na mara nyingi kama si mara zote, huwa hugusii kbs nini hasa wajibu wa Mbunge katika kutimiza majukumu hayo unayotaka yamalizike na huwa hutaki kwa makusudi au bila kujua, kuonesha Kama John hatimizi majukumu hayo au la. Lakini kwa uhalisia ni kwamba John anapambana na ameshughulikia matatizo ya Ubungo kwa kuisimamia na kuiwajibisha serikali juu ya Ubungo kuliko wakati wowote wa wabunge wa CCM huko nyuma.

Kama kweli uko genuine, tembelea blog yake kisha umpinge hapa kwa facts ili wewe na wenzako wengi mtushawishi nasi pia.

Kuna principle moja mnaitumia sana akina Kimbunga, kila Mara John akiwa-hit kwenye masuala mengi makubwa ya kitaifa, masuala mazito kama la mafuta Jana Bungeni na masuala ya ufisadi mkubwa unaoathiri wananchi wote, wakiwemo wa Ubungo, mnaingia kwenye mitandao humu kusema maji maji maji na barabara, as if hamjui kuwa serikali inawajibika kufanya kazi hizo.
 
Mkuu mbona unakuwa small time thinker, kwa hiyo anawakilisha wananchi ili afanye nini kama si kusaidia kutatua kero zao.

Wenziwe wanalitamani jimbo hilo na kwa kauli hizi tunazozisikia matatizo anabwagiwa incumbent ili suala liwe liability kwake 2015.

Wewe uelewa wako ni mdogo sana kwenye swala zima linahusu dhana uwakilishi wa bungeni na majukumu ya bunge, rudi darasi civics ya form one, au uraia darasa la saba!
 
Wewe uelewa wako ni mdogo sana kwenye swala zima linahusu dhana uwakilishi wa bungeni na majukumu ya bunge, rudi darasi civics ya form one, au uraia darasa la saba!
Pamoja na madongo yote swala liko pale pale.
Madongo si mtaji wa maji wala uwajibikaji, ila nitachukua ushauri wako.
 
Mkuu wengine tumesema humu weeeee lakini tunaonekana hatumtakii mema Mnyika. Kila siku kauli yangu ni kwamba Mnyika ni mahiri katika kujenga hoja na ni msaada mkubwa sana kwa Taifa hili kwa jinsi anavyojenga hoja za kulitetea. Lakini aangalie tusije kumkosa Ubungo kwa kushindwa kutatua kero za maji na barabara. Hayo matatizo ni makubwa Ubungo na ndiyo yanawaangusha wabunge. Najua kuna mipango na michakato mingi ya kutatua hayo matatizo lakini tukumbuke njaa haina mchakato. Atafanya michakato hadi anaondoka mwenzake anakuja anamalizia mchakato anaibuka bingwa!

Mkuu Kimbunga, this is the same oldest story.
Ukimsikia Mnyika ametajwa kwa jambo negative unakuwa sensitive sana kuweka comments zako lakini kwa yale positive hutii maguu kabisa.
Kama unataka kugombea jimbo la Ubungo kuwa muwazi mkuu unaruhusiwa lakini usijaribu kutumia mgongo wa Mnyika kutafuta huruma ya wapiga kura tena kwa habari za kutunga na upotoshaji.

Na kwa hakika mambo aliyoyafanya John Mnyika kwa wananchi wa Ubungo kwa kipindi kifupi cha miaka miwili ni makubwa kuliko yaliyofanywa na wabunge wenu wote wa magamba tangu kuanzishwa kwa jimbo la ubungo.
 
Back
Top Bottom