Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

Mnyika, watchout! Maji Ubungo yatakuondoa...

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,688
Reaction score
14,700
Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi.

Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo.

Waziri Kabaka , Waziri wa Kazi na Ajira, amemrushia madongo mazito Mbunge John Mnyika kwa kushindwa kwake "kuona ndani" katika kulitatua tatizo hilo. (ref Mwananchi 6/11/2012, pg 8)

Waziri Kabaka amedai kuwa Mnyika amekuwa akitumia muda mwingi katika siasa za Bunge kuliko kutatua matatizo ya wananchi wa Ubungo.

Katika kusaidia kutatua matatizo ya Ubungo Waziri Kabaka ameahidi kumwona waziri mwenziwe wa Maji na ili alitazame tatizo la maji Ubungo na kulitatua.

Anachosema Waziri Kabaka kina mantiki kubwa, Mnyika inabidi ajipange na kuwa na uhusiano mzuri na "magamba" wanaoendesha wizara zinazomgusa kiutendaji jimboni kwake.

Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya mwanasiasa na kiongozi jamaa anaweza siasa but hawezi kuongoza wenye akili watanielewa wasio na akili watanitukana
 
Mmeanza tena?

Napenda niwahakikishie kuwa, mbinu na chokochoko mnazozifanya dhidi ya Mh Mbunge wa Ubungo - John John Mnyika - hazitafua dafu.

Kila siku huwa mnakuja na mada za kumshambulia Mnyika; kulaumu kuhusu maji Ubungo. Niseme tu kuwa, tangu nianze kuishi Ubungo (Mwaka wa 9 naenda wa 10 sasa), sijawahi kumwona Mbunge effective na efficient kama Mnyika.

Huyu ni mwakilishi wa wana Ubungo si tu bungeni, bali katika ngazi ya Jimbo. Na niseme wazi, sikuwahi kuona maji ya bomba yakitoka hapa Ubungo, zaidi ya kutegemea maji ya visimani kule kwenye kanisa la KKKT au kisima cha Jumuiya Ubungo NHC ambacho hata hivyo hakikuwa na uwezo wa kukidhi matakwa na mahitaji ya maji Ubungo. Lakini sasa maji yanatoka. Sawa, si kila siku lakini kwa maeneo yetu sisi huwa yanatoka Jumanne, Alhamisi na Jumamosi. Fair enough. Na watu wa Msewe/Kibangu kama wako apa waseme..juzi Jumapili nilipita mitaa ya kwenu; mbona maji yalikuwa yanatoka?

Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.

Mtasubiri sana 2015 mkidhani kuwa mtakomboa Jimbo...Sahauni.

Kwa maelezo zaidi tembelea JOHN MNYIKA usuuzike na roho yako...
 
Acha kumtisha Mnyika wewe,kuna wabunge kibao ambao hata majimboni hawafiki sembuse kuleta maji!chato wanatumia maji machafu ya ziwa toka uhuru na stil wanamchagua mapadlock,acha fitna kama ni mbunge wako mtafute ukampe maoni yako na namna ya kulitatua!
 
Tofautisha Chato na Ubungo.
Ubungo iko bongo proper na mbunge wa hapa yuko juu kuliko wa kulee.... nanihiii!
Kwa hiyo kilio cha hapa mujini ni kikubwa na kusikika zaidi, siyo bure kwamba Mama Kabaka kaamua kudondosha madongo hapa mjini na si Moshi wala Singida.
 
Hata shida ya maji ubungo yawezekana ni mbinu ya CCM kumpotezea kura Mnyika. Kumbuka ni wajibu wa serikali kushughulikia kero hiyo
 
Mkuu wengine tumesema humu weeeee lakini tunaonekana hatumtakii mema Mnyika. Kila siku kauli yangu ni kwamba Mnyika ni mahiri katika kujenga hoja na ni msaada mkubwa sana kwa Taifa hili kwa jinsi anavyojenga hoja za kulitetea. Lakini aangalie tusije kumkosa Ubungo kwa kushindwa kutatua kero za maji na barabara. Hayo matatizo ni makubwa Ubungo na ndiyo yanawaangusha wabunge. Najua kuna mipango na michakato mingi ya kutatua hayo matatizo lakini tukumbuke njaa haina mchakato. Atafanya michakato hadi anaondoka mwenzake anakuja anamalizia mchakato anaibuka bingwa!
 
Hata shida ya maji ubungo yawezekana ni mbinu ya CCM kumpotezea kura Mnyika. Kumbuka ni wajibu wa serikali kushughulikia kero hiyo

Hiyo pia yaweza kuwa kweli. Apambane sasa
 
Chato ni mfano tu, majimbo mengi tz yanashabihiana matatizo yao whether yako huko bongo usemapo ama bush,na kama watz wangekuwa wanachagua wawakilish kwa kuangalia utendaji wao na uwezo wa kuwatatulia matatizo yanayowakabil basi ccm ingeshakuwa chama cha upinzani kitambo!
Tofautisha Chato na Ubungo.
Ubungo iko bongo proper na mbunge wa hapa yuko juu kuliko wa kulee.... nanihiii!
Kwa hiyo kilio cha hapa mujini ni kikubwa na kusikika zaidi, siyo bure kwamba Mama Kabaka kaamua kudondosha madongo hapa mjini na si Moshi wala Singida.
 
Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi.

Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo.

Waziri Kabaka , Waziri wa Kazi na Ajira, amemrushia madongo mazito Mbunge John Mnyika kwa kushindwa kwake "kuona ndani" katika kulitatua tatizo hilo.
(ref Mwananchi 6/11/2012, pg 8)

Waziri Kabaka amedai kuwa Mnyika amekuwa akitumia muda mwingi katika siasa za Bunge kuliko kutatua matatizo ya wananchi wa Ubungo.
Katika kusaidia kutatua matatizo ya Ubungo Waziri Kabaka ameahidi kumwona waziri mwenziwe wa Maji na ili alitazame tatizo la maji Ubungo na kulitatua.

Anachosema Waziri Kabaka kina mantiki kubwa, Mnyika inabidi ajipange na kuwa na uhusiano mzuri na "magamba" wanaoendesha wizara zinazomgusa kiutendaji jimboni kwake.

Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.

Inaonekana wew ni mpiga debe tu, hufuatilii kujua nini kinafanyika kuhusu tatizo hilo. Hata CCM wenyewe wanakiri kuwa kazi inayofanyika katika nyanja hii ni kubwa kulingana na ukubwa wa tatizo lenyewe. Inawezekana vipi Waziri wa Kazi na Ajiara anayeshindwa kupeleka Bungeni KWA KURIDHIWA MKATABA WA ILO KUHUSU AJIRA AWEZE KUFUNGUA MDOMO KUHUSU MASUALA YA MAJI?

Hivi kati ya ukosefu wa Maji na ukosefu Ajira ni lipi tatizo kubwa hap nchini? Yapo majimbo ambayo hayana tatizo la maji lakini wakazi wake hususan vijana hawana ajira kabisa ilihali Waziri kakaa wizarani anashindwa hata kupeleka mikataba ya Ajira bungeni kwa ajili ya kuridhiwa. Hadi sasa Tanzania imeridhia mikataba 35 ya kimataifa inayohusu masuala ya ajira na haki za wafanyakazi http://www.ilo.org/dyn/normlex/en/f?p=1000:11200:3070969978430691::::P11200_INSTRUMENT_SORT:3 na badi haijaridhia mikataba 57 inayohusu Ajiri na haki za wafanyakazi http://www.ilo.org/dyn/normlex/en/f?p=1000:11210:3070969978430691::::P11210_INSTRUMENT_SORT:4
 
kuna tofauti kubwa kati ya mwanasiasa na kiongozi jamaa anaweza siasa but hawezi kuongoza wenye akili watanielewa wasio na akili watanitukana

thank u
umeelewaka mkuu
nadhani kijana asubiri wakati ufike aende zake kuzimu
rais dhaifu sawa,ushupavu wake yeye uko wapi sasa??
Nashangaa sana povu jiiiingiii
kumbe blaah blaaah..
 
Tofautisha Chato na Ubungo.
Ubungo iko bongo proper na mbunge wa hapa yuko juu kuliko wa kulee.... nanihiii!
Kwa hiyo kilio cha hapa mujini ni kikubwa na kusikika zaidi, siyo bure kwamba Mama Kabaka kaamua kudondosha madongo hapa mjini na si Moshi wala Singida.
Mama Kibaka anatuongezea idadi ya vibaka watachomwa moto wote na M4C
 
inaonekana wew ni mpiga debe tu, hufuatilii kujua nini kinafanyika kuhusu tatizo hilo. Hata ccm wenyewe wanakiri kuwa kazi inayofanyika katika nyanja hii ni kubwa kulingana na ukubwa wa tatizo lenyewe. Inawezekana vipi waziri wa kazi na ajiara anayeshindwa kupeleka bungeni kwa kuridhiwa mkataba wa ilo kuhusu ajira aweze kufungua mdomo kuhusu masuala ya maji?

Hivi kati ya ukosefu wa maji na ukosefu ajira ni lipi tatizo kubwa hap nchini? Yapo majimbo ambayo hayana tatizo la maji lakini wakazi wake hususan vijana hawana ajira kabisa ilihali waziri kakaa wizarani anashindwa hata kupeleka mikataba ya ajira bungeni kwa ajili ya kuridhiwa. Hadi sasa tanzania imeridhia mikataba 35 ya kimataifa inayohusu masuala ya ajira na haki za wafanyakazi http://www.ilo.org/dyn/normlex/en/f?p=1000:11200:3070969978430691::::p11200_instrument_sort:3 na badi haijaridhia mikataba 57 inayohusu ajiri na haki za wafanyakazi http://www.ilo.org/dyn/normlex/en/f?p=1000:11210:3070969978430691::::p11210_instrument_sort:4

ona sasa
yani mtu mzima na ana ndevu za osama anakuja hapa kwa tambo kuuliza kati ya maji na ajira bora nini??
Amesahau kua maji ni uhai??what the hell is ajira kulinganisha na uhai??
Wangapi hawana ajira lakini wanaishi??
Unauliza kati ya maji na ajira bora nini au unataka kuuliza kati ya mvua na jua bora nini??
Lipi lilikua lengo lako mkuu
breakfast umeipata lakin??karibu kahawa ya pemba hapa uchangamshe akili kidogo...
 
thank u
umeelewaka mkuu
nadhani kijana asubiri wakati ufike aende zake kuzimu
rais dhaifu sawa,ushupavu wake yeye uko wapi sasa??
Nashangaa sana povu jiiiingiii
kumbe blaah blaaah..
Rais Dhaifu anakusanya kodi. Mikoba yote anayo!!!!!! Lakini Mnyika hajawahi kukusanya hata cent ya mtu ondoa bla bla bla hapa jamvini
 
Yani kati ya wabunge/mawaziri bogus mama Kabaka ni namba mbili baada ya Sofia Simba.
Hana akili ya kumshauri John Mnyika na hana uwezo wa kumsaidia Mnyika katika kutafutia ufumbuzi kero za jimbo la Ubungo.

Kazi anazofanya Mnyika kwa wapiga kura wake hakuna mbunge anayeweza kumfikia kwa sasa. Ni juzi tu akiwa na waziri wa maji Prof. Maghembe wamezindua mradi mkubwa sana wa maji maeneo ya Ubungo Makuburi/external kwahiyo eneo hilo amemaliza kero ya maji na bado anaendelea na maeneo mengine.

Wafitini na wenye wivu ndio mnaopiga kelele hapa kila mara lakini ukweli ni kwamba Mnyika amefanikiwa kwa sehemu kubwa sana kupunguza tatizo la maji ubungo kuliko wabunge wote waliomtangulia. Na kwakuwa anafanya vizuri sana katika siasa za kitaifa pia, ndo maana wale wanaomuombea mabaya kama Kimbunga na masopakyindi wanakesha kumchawia hapa JF.
 
Last edited by a moderator:
Tofautisha Chato na Ubungo.
Ubungo iko bongo proper na mbunge wa hapa yuko juu kuliko wa kulee.... nanihiii!
Kwa hiyo kilio cha hapa mujini ni kikubwa na kusikika zaidi, siyo bure kwamba Mama Kabaka kaamua kudondosha madongo hapa mjini na si Moshi wala Singida.
Waeleze hao kwamba ubungo ndio Daresalam.
 
Yani kati ya wabunge/mawaziri bogus mama Kabaka ni namba mbili baada ya Sofia Simba.
Hana akili ya kumshauri @J J Mnyika na hana uwezo wa kumsaidia Mnyika katika kutafutia ufumbuzi kero za jimbo la Ubungo.

Kazi anazofanya Mnyika kwa wapiga kura wake hakuna mbunge anayeweza kumfikia kwa sasa. Ni juzi tu akiwa na waziri wa maji Prof. Maghembe wamezindua mradi mkubwa sana wa maji maeneo ya Ubungo Makuburi/external kwahiyo eneo hilo amemaliza kero ya maji na bado anaendelea na maeneo mengine.

Wafitini na wenye wivu ndio mnaopiga kelele hapa kila mara lakini ukweli ni kwamba Mnyika amefanikiwa kwa sehemu kubwa sana kupunguza tatizo la maji ubungo kuliko wabunge wote waliomtangulia. Na kwakuwa anafanya vizuri sana katika siasa za kitaifa pia, ndo maana wale wanaomuombea mabaya kama Kimbunga na masopakyindi wanakesha kumchawia hapa JF.
Umenisoma akili zangu, aiseeeee.
 
rais dhaifu anakusanya kodi. Mikoba yote anayo!!!!!! Lakini mnyika hajawahi kukusanya hata cent ya mtu ondoa bla bla bla hapa jamvini

mbona mtemvu anafanya kazi kubwa kule temeke??au sababu ni gamba?
Well,mbona slaa kafanya kazi kubwa karatu?mbona zito kafanya kazi kubwa kigoma?
Yeye mnyika vipi??au yeye anadhani maneno ndio uwakilishi??
Vioja sana...
 
Mnyika akishinda ubunge 2015 nakunya hapa
 
mbona mtemvu anafanya kazi kubwa kule temeke??au sababu ni gamba?
Well,mbona slaa kafanya kazi kubwa karatu?mbona zito kafanya kazi kubwa kigoma?
Yeye mnyika vipi??au yeye anadhani maneno ndio uwakilishi??
Vioja sana...
Unategemea Mnyika na Mtemvu wakiwasilisha shida zao kwa Waziri wa Maji nani atasikilizwa haraka acha ulumbukeni gamba wewe
 
Back
Top Bottom