Hii taarifa inanipa mashaka.
But anyway, Mnyika kama kweli ametoa hiyo taarifa, basi anatakiwa ajue kuna wakati interest za makundi mawili zinaweza kufanana.
Mfano, kama wanaharakati wakipigania haki za binadamu na utawala bora, hapo lazima wanaharakati watatolea mfano wa Lissu aliyepo gerezani.
Kama wakitolea mfano wa Lissu, basi automatically itakuwa imetajwa Chadema, kwasababu Lissu ni kiongozi wa chama hicho.
Hivyo basi, naona Mnyika anatakiwa awe brave enough kutambua ni mazingira yapi yanayowafanya wanaharakati kuitaja Chadema, pasi ktengeneza sintofahamu kati yao.
Kama wanamtaja Lissu wakishinikiza aendelee kukaa gerezani, sio kwa nia mbaya, bali wanamtaja Lissu abaki gerezani ili apelekwe mahakamani.
Kwasababu hata mimi ninaamini Lissu hana kosa lolote, na kuliko kumuachia kwa masharti, ni bora aendelee kukaa gerezani mpaka watawala watakaposhindwa kesi mahakamani, ili Lissu awe huru pasipo masharti yoyote juu yake.
Naandika hivi kwasababu naamini jambo moja, kama Lissu akikubali kutoka gerezani kwa masharti, basi watawala wataonekana walikuwa sahihi walivyomshikilia kwa zaidi ya mwaka mmoja, jambo ambalo kwangu naamini sio sawa.
On the other hand, hii kauli ya Mnyika pia inanifanya nianze kuona kuna dalili za mazungumzo kati ya Chadema na serikali ya CCM.
Hii kauli ya kuitenganisha Chadema na wanaharakati, imekuja purposely ili kuondoa misuguano inayoweza kujitokeza pale ambapo mazungunzo yataanza.
Ili isionekane kauli za wanaharakati zina uhusiano wowoe na Chadema hasa zikiwa negative zenye muelekeo wa kuvuruga mazungumzo.