Mnyika kaleta maendeleo Ubungo?

Mnyika kaleta maendeleo Ubungo?

vivios

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
244
Reaction score
9
Naomba kuuliza kwa watu wenye mapenzi mema na CHADEMA hivi Mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaidi ya kelele anazopiga bungeni?

Pia ushauri mdogo tu kwa CHADEMA muishio Ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguzi ujao,kama hampendi CCM mpeni CHADEMA mwingine.
 
Jamani naomba kuuliza kwa watu wenye mapenz mema na chadema hivi mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaid ya kelele anazopiga bungeni?
Pia ushauri mdogo tu kwa chadema muishio ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguz ujao.kama hampend ccm mpeni chadema mwingine

Hayo Maendeleo huyaoni? Morogoro Road inajengwa, Kimara kunajengwa daraja kubwa kuliko la Manzese huoni tu?
 
kaoshe nanilii yako uje tena, ulitaka akuletee maembe hadi nyumbani kwenu ndo ujue kale maendeleo Ubungo?
ukitaka maendeleo ya kukuza Tumbo hamia tigo au CCM.
 
jamani naomba kuuliza kwa watu wenye mapenz mema na chadema hivi mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaid ya kelele anazopiga bungeni?
Pia ushauri mdogo tu kwa chadema muishio ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguz ujao.kama hampend ccm mpeni chadema mwingine

zungu yeye kaleta maendeleo gani ilala?

Jamani naomba kuuliza kwa watu wenye mapenz mema na chadema hivi mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaid ya kelele anazopiga bungeni?
Pia ushauri mdogo tu kwa chadema muishio ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguz ujao.kama hampend ccm mpeni chadema mwingine

[h=3]Ziara Jimboni: KATA YA MANZESE 08 Desemba, 2012[/h]
Ziara ndani ya Jimbo: muendelezo wa kutembelea maeneo mbalimbali ya jimboni. Jana, Desemba 08, 2012 ziara kubwa ilifanyika katika kata ya MANZESE.

Ziara ilimudu kutembelea ofisi ya kata (Kilimani), kufungua misingi katika mitaa ifuatayo; Kilimani, Chakula bora, Mvuleni, Midizini, Mwembeni, na Mnazi Mmoja.

Kisha mkutano wa hadhara na wananchi wa mtaa wa Mnazi Mmoja.
 
Jamani naomba kuuliza kwa watu wenye mapenz mema na chadema hivi mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaid ya kelele anazopiga bungeni?
Pia ushauri mdogo tu kwa chadema muishio ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguz ujao.kama hampend ccm mpeni chadema mwingine

[h=2]Sunday, December 30, 2012[/h] [h=3]Wakazi wa GOBA na KWEMBE: Msikose leo saa nane mikutano juu ya MAJI[/h]
Wakazi wa Kata ya GOBA:

Tume ya Haki za Binadamu imetangaza/imenukuliwa kwenye vyombo vya habari leo kuwa imeanza kuchunguza na kuchukua hatua juu ya mashtaka niliyowasilisha kuhusu mgogoro wa toka mwaka 2007 unaokwamisha huduma ya MAJI katika mtaa wa Goba. Kwa upande wa Mtaa wa Kulangwa-Kata ya Goba tenki limeshajengwa, ujenzi wa miundombinu mingine unakaribia kuanza ili wananchi wapate maji kupitia mradi wa Madale Kisauke. Ili kuwa na usimamizi bora kuanzia hatua za awali fikeni leo (Desemba 30, 2012) kuanzia saa nane mchana , Mahali: Shule ya Kulangwa kutoa maoni kuhusu Katiba ya Jumuiya ya watumiaji Maji.

Tume ya Haki za Binadamu a Utawala Bora nayo ikifika muipe ushirikiano tupate ufumbuzi wa kudumu. Pamoja na jumuiya za watumiaji wa maji na kamati za maji kama ufumbuzi wa mpito, suluhisho la kudumu ni Kata nzima ya GOBA kuhudumiwa moja kwa moja na DAWASA na DAWASCO kupata miundombinu inayoendana mijini kwa kuwa Goba si kijijini tena.

Wakazi wa Kata ya Kwembe:

Utekelezaji wa miradi maji kwa ufadhili wa BTC unasonga mbele. Wakati ujenzi wa miundombinu ukiendelea ipo haja ya kuandaa Katiba ya jumuiya ya watumiaji wa maji ili kuwa na usimamizi endelevu maji yatakapoanza kutoka. Kwa wakazi wa Kata ya Kwembe fikeni ofisi ya serikali ya mtaa leo kuanzia saa nane mchana mtoe maoni yenu.
Hakika Tutafika!

Maslahi ya Umma Kwanza,

John Mnyika,
Mbunge Jimbo la Ubungo
30/12/2012
 
Tunashukuru kwa ushauri wako ila kama mkiti mstaafu wa Chadema jimbo la Ubungo na kama mjumbe wa Baraza kuu ninapenda kukuhakikishia kuwa kati ya wabunge wa chadema watakaorudi Bungeni kwa kishindo John Mnyika ni mmojawapo. Jambo hili halihitaji utafiti tu. Kumbuka kauli mbiu ya AMUA kama wewe ni mkazi unaelewa ina maana gani.
Pili, kuhushu shughuliza maendeleo alizofanya Mnyika tembelea blog yake ya Mnyika.
Tatu, harakati zake za kuleta maji zilizokwamishwa Dodoma pia tutawaeleza wananchi wakati huo.

NB; Mbona hoja hizi zimeanza baada ya Juliana shonza kurudi ccm? Kuna uhusiano gani hapa?
 
Jamani naomba kuuliza kwa watu wenye mapenz mema na chadema hivi mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaid ya kelele anazopiga bungeni?
Pia ushauri mdogo tu kwa chadema muishio ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguz ujao.kama hampend ccm mpeni chadema mwingine

[h=2]Saturday, December 22, 2012[/h] [h=3]‘SUMATRA idhibiti nauli Kibamba'[/h]
na Betty Kangonga

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetakiwa kudhibiti nauli za daladala zinazofanya safari zake katika barabara ya Morogoro.

Inaelezwa kuwa daladala zinazokwenda Kata ya Kibamba zinatoza sh 650 na zile zinazokwenda Kiluvya zikitoza sh 900.

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), alisema jana kuwa katika kikao kilichoketi Oktoba 4, mwaka huu alimkumbusha mwakilishi wa Sumatra kushughulikia tatizo hilo, lakini hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.

Alisema pamoja na Sumatra kutangaza nauli ya daladala Machi mwaka jana na kutaja eneo lenye nauli zaidi ya moja, lakini hakuna uwiano unaostahili baina ya njia za Kibamba na za maeneo mengine yenye umbali mrefu.

"Sumatra inapaswa kutoa maelezo kwa umma kuhusu hatua iliyofikiwa katika kudhibiti nauli za njia zinazokwenda Kata ya Kibamba ambazo zina wastani wa sh 650, huku njia nyingine zenye urefu zaidi au unaokaribiana na wa njia za Kibamba wastani wake wa nauli ukiwa sh 500," alisema Mnyika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Alisema kwa nauli zilizotangazwa na mamlaka hiyo njia ya Kibamba hadi Kariakoo inapaswa kuwa sh 650, Kibamba hadi Muhimbili sh 650, Kibamba mpaka Magomeni sh 650 na Kibamba hadi Kivukoni sh 650.

Mnyika alisema njia nyingine ndefu zaidi au zenye umbali unaokaribiana na ule wa Kibamba zinatozwa kiwango kidogo akitolea mfano Gongo la Mboto hadi Mwenge sh 500, Kitunda hadi Ubungo sh 500, Mbagala Rangitatu hadi Ubungo sh 500.
 
Jamani naomba kuuliza kwa watu wenye mapenz mema na chadema hivi mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaid ya kelele anazopiga bungeni?
Pia ushauri mdogo tu kwa chadema muishio ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguz ujao.kama hampend ccm mpeni chadema mwingine
we unapima maendeleo kwa vigezo vipi? foleni za magari kama fast jet.? kwa taarifa yako anachokifanya Mnyika ni zaidi ya maendeleo? mampambano dhidi ya Ufisadi ndio ufunguo wa maendeleo. Kama CCM itaacha wizi wa Rasilimali za taifa hivyo hivyo tutakuwa na pesa za kujenga barabara, reli, Hosp zenye dawa na madaktari tena si kwa Ubungo bali tanzania . Anachokifanya Mnyika ni kutafuta Ubungo/Tanzania yenye neema period
 
Huwa najiuliza, hivi Temeke ni jimbo la upinzani? Manake linazidi kuachwa nyuma tu na linazidi kuchakaa sana.
 
Jamani naomba kuuliza kwa watu wenye mapenz mema na chadema hivi mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaid ya kelele anazopiga bungeni?
Pia ushauri mdogo tu kwa chadema muishio ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguz ujao.kama hampend ccm mpeni chadema mwingine

Ulitakiwa kwanza useme kazi za mbunge ni zipi, kisheria/kiutawala, ndipo uulize utekelezaji wa mbunge huyo (Mnyika) ukoje, kulingana na job discripition inayosema.
 
Shonza ndo umeanza harakati za kung'oa kwa style hii? Du basi kazana sana maana bado upo nyuma. Ila angalia maana kina nape wanapiga domo ili wapewe hilo Jimbo sasa na wewe ndio unaanza kiherehere... Angalia.
 
Hayo Maendeleo huyaoni? Morogoro Road inajengwa, Kimara kunajengwa daraja kubwa kuliko la Manzese huoni tu?

kwa upeo wako hayo kayafanya Mnyika au ni serikali? Mpango wa ujenzi ulianza lini ni swali unalopaswa kujiuliza
 
Maendeleo mengine jaman ajafanya kama ujenz wa barabara ni mipango endelevu ya serikari yetu bwana.
Ila nashukuru kwa maelezo yenu mana mi sijuagi analofanya ndo mana niliomba msaada wa kupata maendeleo alioyaleta ila still hakuna la maana
 
Vivios kauliza kwania njema ila alivyojibiwa sasa...eeh! Hii ndio JF

Toka kwa MrArsenal
 
Jamani naomba kuuliza kwa watu wenye mapenz mema na chadema hivi mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaid ya kelele anazopiga bungeni? Pia ushauri mdogo tu kwa chadema muishio ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguz ujao.kama hampend ccm mpeni chadema mwingine
hahaha!!!!! atudanganyika, kama unataka kujuwa mafanikioa aliyofanya Nyika nenda ktk Ofice za mbunge wa ubungo utakuta kila kitu na jinsi alivyoahidhi na kile alichofanikiwa na ambavyo bado, kwani nyika ni baadhi ya wabunge ambao wako smart kwa mambo wanayofanya na alishawai kutupia humu JF mambo aliyofanya sijui ulikuwa wapi. La pili, Ktk wabunge wanaogopwa na CCM mjowapo ni Kamanda Nyika.....kwanini awamtaji jimbo la maswa mashari kwa shibuda au wabunge wengine au wameleta maendeleao sana majimboni kwao....siku zote unayemuogopa ndiye unaye mpigia kilele. Angalia hata ktk upinzani wa Mpira angalia chama cha upinzani kinapokuwa na nguvu km kilivyo sasa hivi chadema kitaandamwa kwa kila baya watatupiwa wao
 
kwa upeo wako hayo kayafanya Mnyika au ni serikali? Mpango wa ujenzi ulianza lini ni swali unalopaswa kujiuliza

Wewe kwa upeo unajua Mnyika anatoa pesa mfukoni ili watu wachote maji, wanunue vitabu, wajenge madarasa ndo unajua wewe hivyo?
 
Back
Top Bottom