Mnyika kaleta maendeleo Ubungo?

Mnyika kaleta maendeleo Ubungo?

Basi asingetoa ahadi au asigombea ubunge ili ampishe mgombea wa CCM akiongee KiCCM maji yapatikane.

Kwa akili za namna yako ipo siku utamtuma mkeo akalale na tajiri ili upate mali.

Ahadi alizotoa Mnyika zilimaanisha utekelezaji wa ilani ya CDM. Kama CDM inaingia madarakani (DOLA) basi hayo yalikuwa hukumu yake. Kwa sasa anachoweza kufanya ni kuweka msukumo
 
Umeweka mifano ya wabunge wenye wasi wasi na majimbo yao kiasi wako radhi kutumia fedha zao mifukoni kuwahonga watu waliokata tamaa ili wawape kura kwa kuwa waliwakopesha.

Labda nikuulize swali: Unadhani ni nani mwenye jukumu la kukopesha wajasiriamali? Mbunge au Financial Institutions?

Wewe niambie kwa akili yako unaonaje: Wabunge watoe 'hongo' za mikopo kwa wananchi au tukazania kwenye uboreshaji wa sera ili kila mwananchi akopesheke kwenye taasisi za fedha?

Kama ulivyosema, unaishi Dar. Sasa acha nikukumbushe kuwa UNAISHI DAR na SIO UBUNGO. Ubungo inakaliwa na watu wasomi wasiodanganyika na senti na mikopo isiyo na tija. Tangu waanze kukopeshwa hao wanaokopeshwa ni miaka, lkn maisha yao yako vile vile sbb ya sera mbovu za CCM. Sasa Mnyika anapoongea bungeni vilaza kama wewe unamuita 'muongeaji'.

Naomba unikumbushe tathmini ya 'the so called mabilioni ya Kikwete'. Kichefuchefu kitupu, na bado mpo mnaoamini kuwa mbunge akija kukukopesha sh 200,000 basi maisha yako yataboreka. Mkopo ukiupata huku sera za biashara na uchumi ni mbovu hamna kitu mdogo wangu.

Kwa faida yako na wenzio, mbunge ni mwakilishi wetu na sio mhamasisha michango. Mbunge anatusaidie mikwamo inayohusisha propaganda za kisiasa na sio fedha za mfukoni mwake. Akili zako zimekaa ki -CUF CUF nikimaanisha za KIKABWELA

nifanye kazi ya kutafuta mchungaji akuombee. unahitaji sala maalumu
 
Ukiandika kipuuzi namna hii (bila kituo wala herufi kubwa) sentensi haieleweki. Kwa hiyo ndio unasemaje sijakuelewa
1. Mnyika katoa fedha za barabara kubwa? au
2. Mnyika hajatoa fedha za barabara kubwa?

Inaonekana umebadilishana ubongo na chizi na huyo chizi alipata wokovu wake siku alipokukabidhi hii dhahma iliyoko kichwani. Unaongea upuuzi tu hapa badala ya kujibu hoja zangu:

1. Barabara za Manispaa zinajengwa kwa bajeti za manispaa ambazo zinasimamiwa na baraza la madiwani au mbunge?

2. Unajua maana ya MANISPAA?

je unajua kuwa mbunge anaingia ktk baraza la madiwani. namashaka hata uwezo wako wa kusoma biblia ni mdogo kama tafsiri ndogo tu inakushinda, niliamini ktk avator yako kuwa unaupeo kumbe kitimoto kabisa(nguruwe)
 
akili ndogo kama sisimizi kwa kuwa ni mbunge wa CDM hata akikuambia ukamsafishie nyumba yake utakwenda

Naenda kwa nini nisiende mkuu wakati ni kiongozi wangu na ninae mwamini kuwa anapigania HAKI zangu zilizo bakwa na mkoloni mweusi maccm
 
mbona kila siku ni MNYIKA MNYIKA TU!anawanyima usingizi sio nyie wanyonya damu..mafisadi papa..makupe!..mbona hatusikii hata siku moja mkiuliza makongoro kawafanyia nini segerea au zungu ilala...ila ni myika tuuu..mimi nina wasiwasi masaburi yako ndo yamekushauri uandike na siyo akili yako
 
ilo jimbo la ubungo mtakuwa mnalisikilizia tuuu kama la mzee ndesa
 
Hhehhehehe mi still sijswaelewa nimeuliza kuhusu maendeleo ya mnyika bt hakuna nalojibiwa zaid ya porojo tu.
Nais hawa watu wanafata mkumbo
 
Naomba kuuliza kwa watu wenye mapenzi mema na CHADEMA hivi Mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaidi ya kelele anazopiga bungeni?

Pia ushauri mdogo tu kwa CHADEMA muishio Ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguzi ujao,kama hampendi CCM mpeni CHADEMA mwingine.

Zungu ameleta maendeleo gan jimboni kwake?
 
Ulitakiwa kwanza useme kazi za mbunge ni zipi, kisheria/kiutawala, ndipo uulize utekelezaji wa mbunge huyo (Mnyika) ukoje, kulingana na job discripition inayosema.

Umenena mkuu maana Watz wengi tumedanganywa kuhusu kazi za mbunge na ndio maana ukienda sehemu yoyote nchini wananchi wameaminishwa kwamba chochote kinachotendeka katika eneo lake ni kazi ya mbunge kumbe kuna ambayo yanafanyika indirectly wtu hawayaoni.

Kuna haja mamlaka zinazohusika zikaainisha kazi za mbunge vinginevyo wananchi wengi watakuwa wanachagua watu kwa kumwangalia kitambi na uwezo wa kifedha wakati mbunge ni kiungo tu kati ya serikali kuu na serikali ya mtaa yaani mbunge anapokuwa katika halmashauri yake anashirikiana bega kwa bega na baraza la madiwani ambalo ndio waamuzi wa mwisho katika halmashauri husika na yale ambayo yapo nje ya uwezo wao ndio mbunge anayabeba na kuyapeleka bungeni ili serikali kuu iangalie namna ya kusaidia.

Mie nilidhani angeanza kuhoji mwenyekiti wake wa mtaa na diwani wake maana jinsi navyoona jamaa amelewa sumu iliyopandikizwa muda mrefu kwamba mbunge ndio kila kitu kumbe kuna mambo mengine yapo chini ya mwananchi, mwenyekiti wa mtaa, diwani na mengine mbunge.
 
Umeweka mifano ya wabunge wenye wasi wasi na majimbo yao kiasi wako radhi kutumia fedha zao mifukoni kuwahonga watu waliokata tamaa ili wawape kura kwa kuwa waliwakopesha.

Labda nikuulize swali: Unadhani ni nani mwenye jukumu la kukopesha wajasiriamali? Mbunge au Financial Institutions?

Wewe niambie kwa akili yako unaonaje: Wabunge watoe 'hongo' za mikopo kwa wananchi au tukazania kwenye uboreshaji wa sera ili kila mwananchi akopesheke kwenye taasisi za fedha?

Kama ulivyosema, unaishi Dar. Sasa acha nikukumbushe kuwa UNAISHI DAR na SIO UBUNGO. Ubungo inakaliwa na watu wasomi wasiodanganyika na senti na mikopo isiyo na tija. Tangu waanze kukopeshwa hao wanaokopeshwa ni miaka, lkn maisha yao yako vile vile sbb ya sera mbovu za CCM. Sasa Mnyika anapoongea bungeni vilaza kama wewe unamuita 'muongeaji'.

Naomba unikumbushe tathmini ya 'the so called mabilioni ya Kikwete'. Kichefuchefu kitupu, na bado mpo mnaoamini kuwa mbunge akija kukukopesha sh 200,000 basi maisha yako yataboreka. Mkopo ukiupata huku sera za biashara na uchumi ni mbovu hamna kitu mdogo wangu.

Kwa faida yako na wenzio, mbunge ni mwakilishi wetu na sio mhamasisha michango. Mbunge anatusaidie mikwamo inayohusisha propaganda za kisiasa na sio fedha za mfukoni mwake. Akili zako zimekaa ki -CUF CUF nikimaanisha za KIKABWELA

Hapo nilipo-bold umesema kitu chenye mantinki maana wabunge siku hizi wamekuwa watu wa kutoa ela badala ya kuhamasisha wananchi wao wachangie shughuli za maendeleo na mwisho wa siku wananchi wanabaki kuchagua watu kwa kumwangalia uwezo wake kifedha badala ya kuangalia uwezo wake wa kuongoza na kushirikiana na wananchi. Mbunge anatakiwa akienda sehemu kama kuna shida si kukimbilia kutoa mabati na cement bali aangalie na wananchi wake wamejipanga vipi kuondoa hilo tatizo ndipo na yeye aongezee lakini siku hizi ni kawaida kusikia mbunge anakwambia nimejitolea sehemu yangu ya mshahara nimenunua madawati 50 na ninataka kuongeza mengine 100 (sasa hapa ni kuwafanya wananchi wawe tegemezi wakati kilichotakiwa ni kuhoji halmashauri husika na ikiwezekana akae na wananchi wake kuangalia namna ya kutatua tatizo kwa pampja)
 
Mbunge kama mbunge hawezi kuleta maendeleao kwenye jimbo kwani hana chanzo cha mapato,bali serikali ndiyo yenye dhamana ya kuleta maendeleo na siyo ubungo tu bali Tanzania yote.Anachofanya mbunge kwa nafasi yake ni kuhakikisha maendeleo yanaletwa kwenye jimbo husika kwa kufuatilia watendaji ambao ni waajiriwa wa serikali na kuwasemea wanachi wajimbo lake bungeni.Anachfanya Myika John kingefanywa na wabunge wote yaani hata wa Chama Tawala leo Tanzania yetu ingekuwa Dubai ya pili.
Kama nimekosea naomba kurekebishwa.
Safi
 
Naomba kuuliza kwa watu wenye mapenzi mema na CHADEMA hivi Mnyika toka kawa mbunge ameleta maendeleo gan jimboni kwake zaidi ya kelele anazopiga bungeni?

Pia ushauri mdogo tu kwa CHADEMA muishio Ubungo jimbo litabaki nyuma kama hamtombadilisha uchaguzi ujao,kama hampendi CCM mpeni CHADEMA mwingine.
Wewe umeleta Maendeleo gani?
 
CCM imeleta maendeleo gani katika umri wa uzee wa mtu mzima? Hill ndilo lingeanza kabla ya Mnyika kwani yeye amekulia ndani ya nchi isiyo na maendeleo.
 
CCM imeleta maendeleo gani katika umri wa uzee wa mtu mzima? Hill ndilo lingeanza kabla ya Mnyika kwani yeye amekulia ndani ya nchi isiyo na maendeleo.
 
Back
Top Bottom