Mnyika apewa Uchifu Mwanza na kupewa jina la Chief Malonja, ataka marekebisho ya Katiba

Pole sana maana mimi nipo na bado sana sana nitaendelea kuwepo maana ndiyo chama kinachopendwa na mamilioni ya watanzania
Toka siku ile nilipokudharau na kukuona kuwa huna faida yoyote kwa CHADEMA, pamoja na wewe kuendelea kujitangaza kuwa upo huko.
Kati ya wanachama wasiokuwa na manufaa ndani ya chama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana MWANZA wamempokea Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa shangwe na kuweka historia kwenye mkoa huo kwa kuamua kukabidhi hadhi ya Chifu wa Wasukuma.

Hakika huu ni msimamo wa kujivunia sana kwa wana MWANZA na inaonyesha kuwa sasa wameanza kujua mchele ni upi na chuya ni zipi kati ya CCM na CHADEMA.


MNYIKA APEWA UCHIFU WA WASUKUMA
View attachment 1306538View attachment 1306539
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amewasili mkoani Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine amesimikwa kuwa Chifu wa Wasukuma na kupewa jina la Chifu Malonja lenye maana ya Mrekebishaji.

Sent using Jamii Forums mobile app

=====

Chadema chataka marekebisho ya mpito ndani ya Katiba ya sasa

Sunday December 29 2019


BY Jesse Mikofu, Mwananchi jmikofu@mwananchi.co.tz

IN SUMMARY

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania, John Mnyika amesema ili kuwa na tume huru ya uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, yafanyike marekebisho ya mpito kwenye katiba iliyopo sasa.

Mwanza. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania, John Mnyika amesema ili kuwa na Tume huru ya uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, yafanyike marekebisho ya mpito kwenye katiba iliyopo sasa.

Amesema kwa muda uliobaki kabla ya uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba, 2020 haiwezekani kukamilika kwa mchakato mzima wa katiba mpya, lakini inawezekana kufanyika kwa marekebisho ya muda ili kukidhi matakwa ya Watanzania.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Desemba 29, 2020 katika ofisi za Chadema Kanda ya Victoria, baada ya kusimikwa kuwa chifu na wazee wakisukuma na kupewa jina la kichifu la Malonga likiwa na maana ya kutengeneza mambo yawe mazuri.

Mnyika amewaambia viongozi wa kanda hiyo kuwa hakuna budi vyama vya upinzani kuungana pamoja na kupeleka muswada bungeni kwa ajili ya mchakato huo.

“Yapo madai kwamba katiba mpya ni gharama kubwa, lakini Rais John Magufuli akikubali tupeleka muswada wa dharura bungeni tunaweza kufanya marekebisho ya mpito kwenye katiba tuliyonayo bila kusubiria mchakato mzima wa Katiba mpya,” amesema Mnyika.

Amesema Katiba ya sasa inaweza kuongezwa vipengele vitatu ambavyo ni; kuongeza Tume huru ya uchaguzi, ibara inayotaka matokeo ya uchaguzi wa Rais yapingwe mahakamani .

Pia kunaweza kuongezwa kifungu kinachosema ili mtu atangazwe kuwa mshindi wa urais, lazima awe amezidi asilimia 50 ya kura zote.

Amesema wakati wa uchaguzi mkuu kilikuwapo kipengele cha kupiga kura ya maoni kuhusu aina gani ya katiba inayotakiwa ili wananchi waipigie kura wakati wakichagua wabunge, madiwani na Rais.
Nikiangalia nyomi la diamond kigoma naona hawa jamaa hawako serious.
 
Mwambieni asije akajitamburisha hivyo akija mwanza atapondwa mawe. Wasukuma hatuna huo ujinga harafu hatupendi furugu huo uchifu akapewe kwao upateni. Ipo cku mtamsikia .
 
Nimpe siri akienda mwanza awe naulinzi mkari sana vijana wa kisukuma wanajipanga kumfanyia kitu mbayaaa sana ambayo itamwachia arama ktk maisha yake yte. Higo nidharau kw koo zte za kisukuma.
 
Pole sana maana mimi nipo na bado sana sana nitaendelea kuwepo maana ndiyo chama kinachopendwa na mamilioni ya watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Endelea kuwepo huko, lakini tambua kuwepo kwako huko na kujifanya mjuaji na kujitambulisha na mambo ya chama hicho ni hasara kwa chama chenyewe.

Kama ni kweli upo huko, inafaa wakufunge gavana. Unawatia hasara.
 
Endelea kuwepo huko, lakini tambua kuwepo kwako huko na kujifanya mjuaji na kujitambulisha na mambo ya chama hicho ni hasara kwa chama chenyewe.

Kama ni kweli upo huko, inafaa wakufunge gavana. Unawatia hasara.
Upo wapi.
 
Kama wewe unavyo kitia hasara chama chako cha kijani
Endelea kuwepo huko, lakini tambua kuwepo kwako huko na kujifanya mjuaji na kujitambulisha na mambo ya chama hicho ni hasara kwa chama chenyewe.

Kama ni kweli upo huko, inafaa wakufunge gavana. Unawatia hasara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom