Kuchitimbo
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 364
- 279
Naomba kuuliza,hii taarifa jana ilirushwa na tv yoyote au waliogopa kufungiwa?
Toka siku ile nilipokudharau na kukuona kuwa huna faida yoyote kwa CHADEMA, pamoja na wewe kuendelea kujitangaza kuwa upo huko.
Kati ya wanachama wasiokuwa na manufaa ndani ya chama!
Bangi inakuharibu akili. Achana nayo.
Tumekwishaje sasa? Kwamba Mnyika aiongoze Chadema kuishinda CCM kwenye Uchaguzi wa 2020? You must be out of your mind!!!
Usiyependezwa na mambo ya serikali jichanganye ccm ukapinge huko chadema utazeeka na kufa bila kubadirishana lolote.Waramba miguu nawaona mlivyo fura kwa hasira na taharuki maana mbuzi tayari kala mkeka
Sent using Jamii Forums mobile app
Nikiangalia nyomi la diamond kigoma naona hawa jamaa hawako serious.Wana MWANZA wamempokea Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa shangwe na kuweka historia kwenye mkoa huo kwa kuamua kukabidhi hadhi ya Chifu wa Wasukuma.
Hakika huu ni msimamo wa kujivunia sana kwa wana MWANZA na inaonyesha kuwa sasa wameanza kujua mchele ni upi na chuya ni zipi kati ya CCM na CHADEMA.
MNYIKA APEWA UCHIFU WA WASUKUMA
View attachment 1306538View attachment 1306539
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amewasili mkoani Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine amesimikwa kuwa Chifu wa Wasukuma na kupewa jina la Chifu Malonja lenye maana ya Mrekebishaji.
Sent using Jamii Forums mobile app
=====
Chadema chataka marekebisho ya mpito ndani ya Katiba ya sasa
Sunday December 29 2019
BY Jesse Mikofu, Mwananchi jmikofu@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania, John Mnyika amesema ili kuwa na tume huru ya uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, yafanyike marekebisho ya mpito kwenye katiba iliyopo sasa.
Mwanza. Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania, John Mnyika amesema ili kuwa na Tume huru ya uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, yafanyike marekebisho ya mpito kwenye katiba iliyopo sasa.
Amesema kwa muda uliobaki kabla ya uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba, 2020 haiwezekani kukamilika kwa mchakato mzima wa katiba mpya, lakini inawezekana kufanyika kwa marekebisho ya muda ili kukidhi matakwa ya Watanzania.
Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Desemba 29, 2020 katika ofisi za Chadema Kanda ya Victoria, baada ya kusimikwa kuwa chifu na wazee wakisukuma na kupewa jina la kichifu la Malonga likiwa na maana ya kutengeneza mambo yawe mazuri.
Mnyika amewaambia viongozi wa kanda hiyo kuwa hakuna budi vyama vya upinzani kuungana pamoja na kupeleka muswada bungeni kwa ajili ya mchakato huo.
“Yapo madai kwamba katiba mpya ni gharama kubwa, lakini Rais John Magufuli akikubali tupeleka muswada wa dharura bungeni tunaweza kufanya marekebisho ya mpito kwenye katiba tuliyonayo bila kusubiria mchakato mzima wa Katiba mpya,” amesema Mnyika.
Amesema Katiba ya sasa inaweza kuongezwa vipengele vitatu ambavyo ni; kuongeza Tume huru ya uchaguzi, ibara inayotaka matokeo ya uchaguzi wa Rais yapingwe mahakamani .
Pia kunaweza kuongezwa kifungu kinachosema ili mtu atangazwe kuwa mshindi wa urais, lazima awe amezidi asilimia 50 ya kura zote.
Amesema wakati wa uchaguzi mkuu kilikuwapo kipengele cha kupiga kura ya maoni kuhusu aina gani ya katiba inayotakiwa ili wananchi waipigie kura wakati wakichagua wabunge, madiwani na Rais.
Endelea kuwepo huko, lakini tambua kuwepo kwako huko na kujifanya mjuaji na kujitambulisha na mambo ya chama hicho ni hasara kwa chama chenyewe.Pole sana maana mimi nipo na bado sana sana nitaendelea kuwepo maana ndiyo chama kinachopendwa na mamilioni ya watanzania
Sent using Jamii Forums mobile app
Ungekuwa na kitu kichwani usingekomalia upuuzi huu.Nakupa ushauri wa bure wacha kutafuna majani tena ukiwa nyumbani kwa shemaji yako
Sent using Jamii Forums mobile app
Upo wapi.Endelea kuwepo huko, lakini tambua kuwepo kwako huko na kujifanya mjuaji na kujitambulisha na mambo ya chama hicho ni hasara kwa chama chenyewe.
Kama ni kweli upo huko, inafaa wakufunge gavana. Unawatia hasara.
Inakuhusu nini wewe!Upo wapi.
Wewe mwenyewe ni mpuuziUngekuwa na kitu kichwani usingekomalia upuuzi huu.
Tunamjua yy ni mpare akapewe kwao.
Endelea kuwepo huko, lakini tambua kuwepo kwako huko na kujifanya mjuaji na kujitambulisha na mambo ya chama hicho ni hasara kwa chama chenyewe.
Kama ni kweli upo huko, inafaa wakufunge gavana. Unawatia hasara.
ndioInamaana Mh Magufuli (Msukuma) anatakiwa amheshimu Mnyika kama "CHIFU" wake.