Mnyeti ni mfano hai wa Wabunge mizigo na anayehatarisha diplomasia ya nchi

Mnyeti amefanyiwa Vetting huyu akawa
mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa
Mkoa akaibukia kwenve ubunge. Kabla
va hapo alikuwa mkuu wa Shule pale
Igokelo Sekondari kuanzia 2013 hadi
2016. Ukiniuliza ni maajabu gani alifanya
pale hadi akachaguliwa kuwa mkuu wa
wilaya au mkuu wa mkoa hakuna
mwenye jibu labda tuhisi ilikuwa ni
connection kazi
 
Huyu mtu anaitwa MNYETI ni hatari...

Naandika kwa kifupi...
Akiwa mkuu wa Mkoa nafikiri Manyara alileta hatari nyingi sana...

I) Alikuwa na mahusiano ya ndani sana na kiongozi mkuu

II)Aliwaweka matajiri wa Tanzaniate mfukoni.. Alihakikisha anayo gawio kubwa

III) Alichukua maslai yote ya vitalu vya uwindandi

IV) Alikuwa anachukua asilimia kubwa ya mavuno ya Tanzanite... Yaani jiwe likitoka anayo asilimia yake... Kiongozi mkuu alijua sana hii mission

V) Alianzisha Club ya Mpira... Nafikiri Lake Victoria Zone.. Na kujenga uwanja... Kwa PESA yake mfukoni

VI) Wafanyabiashara... Wa Arusha / Manyara wanamjua.... Jamaa aliwanyoosha sana... Kwa ufupi waende kwenye kampuni ya mabasi Mtei.... Nimeeleza kwa kifupi sana

Sishangai kwa maneno yake bungeni.... Huyu ALIPITA BILA KUPINGWA 2020.... Mgombea wa Upinzani nusura afe....
 
Tunapowatukana Wasukuma siyo kwamba tuanawadharau au hatuwapendi la hasha bali ni matendo yao,asilimia kubwa wanapopata madaraka makubwa wanayatumia vibaya.Mfano upo wazi kabisa kwa Magufuri,Makonda,Gwajma,Mnyeti,Pascal Mayala na wengine wengi ni tatizo kwa kweli.
Pascal Mayala alipata madaraka gani?!
 
🐒🐒🐒

 
"ALEXANDER MNYETI" sio jina geni katika siasa ya Tanzania. Wengi wanakumbuka ugomvi wake mkubwa na waandishi wa habari mkoa wa Arusha wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambapo chanzo kinaelezwa kuwa ni Mnyeti kumuweka ndani mwandishi wa ITV (Arusha) Halfan Liundi kwa kile kilichoelezwa kuwa Mwandishi huyo aliripoti habari ya maji ambayo yeye (Mnyeti) HAKUIPENDA. baadaye Jeshi la polisi lilimwachia huru mwandishi huyo bila kuweka bayana makosa yake.
Waandishi wa habari walipomtafuta ili kutaka ufafanuzi aliwaambia
“KAMA KUNA MWANAUME ANAYEJIAMINI ANIFUATE KUNIHOJI,”

Sasa haya ni ya zamani, lakini Mnyeti alikwenda kwenye kura za maoni akambwaga Charles Kitwanga na hatimaye akawa mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoa wa Mwanza.

Bungeni nako ameendeleza matendo yake ya ajabu na yasiyotabirika lakini kubwa na la hivi karibuni ni kauli aliyoitoa Alhamisi, 23-06-2022 katika Mkutano wa saba wa Bunge la 12 kikao cha 50 wakati akichangia hoja ya bajeti kuu ya Serikali.

Akichangia hoja Mnyeti alisema "Jirani akiwa na matatizo tumsaidie haina mbaya, lakini jirani tunayemsaidia awe ni jirani anayejitambua, wako majirani HAWAJITAMBUI, inauma sana tunapopeleka askari wetu wanakwenda kupigana vita zao wanarudi wamekufa,...alafu wale wa nchi husika TUNAOWASAIDIA HATA HAWAJALI NCHI YAO, WAKO TANZANIA WANATETEMA KIFUA, WANATETEMA MIKONO ETI WAMEFUNGA MAGOLI. Hizo nguvu wanazotumia kutetemeka kifua na mikono kwanini wasibebe mtutu wa bunduki wasaidie mataifa yao ili dhahabu yao ibaki kwenye nchi yao,...hili sio sawa , Waziri wa Ulinzi lazima mlione hili, haya mambo ya mtu anakuja kutetemeka Tanzania alafu ameacha nchi yake inaibiwa dhahabu huko, hiyo halikubaliki"

Maneno kama haya kuzungumzwa na MBUNGE, ndani ya BUNGE ni hatari sana kwani yanaweza kuleta mgogoro wa kidipolomasia na majirani zetu (Kama alivyowaita Mnyeti). Tunaofuatilia michezo tunafahamu anayetetema ni MAYELE na anatoka nchini CONGO na tunaofuatilia Siasa tunafahamu mgogoro mkubwa unaoendelea baina ya Rwanda na Congo kwa kinachodaiwa kuwa wizi wa MADINI (Dhahabu kama alivyosema Mnyeti), tunafahamu kuwa Askari wetu kadhaa wamepoteza maisha katika maeneo ya nchi hizi LAKINI yeye Mnyeti anapata wapi uhakika kuwa kuna nchi inaibia dhahabu nchi nyingine hadi asimame ndani ya BUNGE kuwataka raia wa nchi hiyo waache kufunga magoli waende KUSHIKA MITUTU YA BUNDUKI kuzuia wizi wa dhahabu.

Mnyeti ni mfano hai wa wabunge na viongozi mizigo tulionao ndani ya Bunge na ndani ya Serikali wasiofahamu nini kisemwe wapi, madhara ya maneno yao na maafa wanayoweza kusababisha. Rais Samia Suluhu anafanya kazi kubwa kurudisha mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi nyingine ambayo yaliyumba sana, lakini watu kama kina Mnyeti ni dhahiri wako katika mwelekeo tofauti kabisa.

Lakini kama huyu Mnyeti alishindwa kusimamia Wilaya kwa haki na usawa, kama aliweza kufikishwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge wakati akiwa DC ni kwanini tutegemee mambo tofauti na anayoyafanya sasa anapozungumza kwa ukubwa wa mijadala ya Nchi, kwa urefu wa maarifa yake ni dhahiri anayoyafanya na mengine ya hovyo anayoweza kuyafanya ndio uwezo wake wa kiuongozi ulipofikia, hii ni mizigo ya kufagia 2025.

Pongezi kwa Waziri wa Ulinzi, Dk. Stergomena Tax, ambaye ameliomba Bunge kuondoa kwenye Kumbukumbu Rasmi za Majadiliano katika mijadala na hoja kati ya Wabunge na Serikali (Hansard) maneno ya Mbunge Alexander Mnyeti AMBAYO AMESEMA NI HATARI NA YANAYOINGILIA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA.

View attachment 2270538
Hata ile taasisi ya usalama aliyokuwa akitumikia alikuwa akitumikia hivi?
Ni aibu tu
 
Mnyeti amefanyiwa Vetting huyu akawa
mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa
Mkoa akaibukia kwenve ubunge. Kabla
va hapo alikuwa mkuu wa Shule pale
Igokelo Sekondari kuanzia 2013 hadi
2016. Ukiniuliza ni maajabu gani alifanya
pale hadi akachaguliwa kuwa mkuu wa
wilaya au mkuu wa mkoa hakuna
mwenye jibu labda tuhisi ilikuwa ni
connection kazi
Sidhani kama wkt huo kulikuwa na vetting. Ilimradi unaendana na mkuu basi teuzi ilikuwa lazima
 
Back
Top Bottom