Mnakumbuka jeuri ya pesa ya Qatar kupandisha ndege ng'ombe wa maziwa 4000 sababu Saudia ilizuia kupitisha maziwa

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,611
8,746
Watu na pesa zao, yaani wana kitu kimoja kinacho wapa pesa lakini kimewapa zaidi ya vitu vingi duniani.

Miaka ya nyuma Saudi Arabia alimuwekea vikwazo Qatar ila mwisho wa siku kapandisha ndege ng'ombe!

Mwenye kisa hiki tuelezeni.

8201711022366452585091.jpg
 
Almarai ndio kampuni kubwa sana ya maziwa Saudia na ndio walikuwa wanapeleka maziwa, jubuni na kila dairy Qatar
Baada ya nchi zingine kama KSA, UAE na wengine kumtuhumu Qatar kuwa yupo upande wa magaidi basi wakavunja uhusiano nao
Ndipo Mqatari mwenye asili ya Syria akaendeleza kampuni yake alikuwa na kondoo za nyama hivyo akaamua kuanza biashara hiyo ya maziwa
Aliiomba pia serikali imsaidie azma yake ili ikamilike na serikali ikamkubalia na kutoa ndege za Qatar Airways kubeba ng'ombe wa maziwa kutoka USA, Turkey na baadhi Iran
Waliletwa ng'ombe 3,400 awamu ya kwanza
Changamoto ilikuwa ni joto la uarabuni kwani walipelekwa jangwani
Ila kwa kuwa pesa ndio kila kitu waliwekewa kila kitu mpaka ubaridi na mashine zinazowamwagia maji ya baridi na feni kubwa
Ila boss wao anaeendesha kiwanda kizima yaani CEO ni Irishman ambae alikuwa anafanya kazi mwanzoni kwenye kiwanda cha maziwa cha Saudia na jamaa wa qatar wakambeba
Na mwaka 2021 hawa wa Qatari waliamua kuwekeza Romania na kununua ardhi ya hectares 5000 kwa ajili ya kulima chakula cha mifugo yao

Fursa zinatupita kila leo au uelewa wetu ndio mdogo kuhusu masuala ya kiuchumi na kutafuta fursa?

Mabalozi wengine wanatafuta fursa kila kukicha sisi wa kwetu wanakula Bata tu
 
Back
Top Bottom