angelita
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 3,017
- 2,445
Hainikeri na wala sina sababu ya kuweweseka sababu huyo si mume wangu na hawezi kuwa mume wangu....siwezi kuwa na mume irresponsible kama huyo...
Na comment humu kwa kuwa kuna wanaotamani maisha yako...na wanasoma huu uzi kimya kimya...nataka kuwaonyesha kuwa huu si ujanja...
Najua wewe sina uwezo wa kukubadili...sababu kwa majibu ya comments zako inaonyesha umeshafanya maamuzi na uwezi geuka nyuma...
Hahahahaaaaaa..... Wenzio walisema na bado wanasema na waume zao bado wapo na vimada kwenye viti virefu wakitoka hapo wanaenda kustareheka akichelewa kurudi kwake saa2 usiku mke anasikia raha dadeki.
Mama tulia ulee wanao ushauri peleka kwa ndugu zako watakushukuru sana. Hapa tuliza mshono wako usije kuachia.