Mkuu
The Boss napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza kwa kujibu maswali kwa ufasaha, yaani bila kuacha maswali, maana si mimi tu bali hadhira yote iliyokuwa inafuatilia hii show imejikuta haina cha kuuliza bali wanapongeza na kushukuru.
Nimejifunza mengi kupitia majibu yako na nimenufaika pia na busara zako.
Nilikuwa na tu viswali twangu tuwili, lakini hawa Wadada weshaniwahi na hivyo nimejikuta sina cha kuuliza.
Shukran kwa Ma-Host wa show hii
lara 1 na
Zinduna, ambao kwa kweli wameonyesha ukomavu wa hali ya juu katika haya mambo.
Maswali yalipangwa vizuri na yalizingatia Tafsida maana kila nilipokuwa naliona swali nilikuwa nashika mdomo, nikajua hii kitu inaweza kutupiwa kule kwenye jukwaa la chini kama alivyosema
platozoom, lakini busara na hekima vilitawala..
Dada zangu
lara 1 na
Zinduna, combination yenu ni nzuri na ninaamini show hii itakukuwa ikitupa raha kila Ijumaa.
Nawaombea kila la kheri kwa kila mtendalo