Kongosho
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 35,987
- 24,234
He he he, umenikumbusha msemo wa 'mbwa wako asipobweka, bweka mwenyewe"
Show ilikua nzuri sana, maswali yalikua yenye mwelekeo wa kujenga vilevile kudadisi.
Kama ni upele ulipata mkunanji, The Boss kayajibu maswali kwa ufasaha kulingana na hulka ya sisi wanaume. Nimeweza kugundua huyu jamaa ni mmoja kati ya wanaume smart hapa MMU na JF kwa ujumla. Hakika tupo wachache ukiacha ile mizaha midogo midogo tuitumiayo kuchangamsha wanajamvi nyakati tofauti tofauti.
Ombi langu kwa watu wote, tuweni wavumilivu nyakati za interviews. Ni vyema kwa waendesha show na mgeni wakamaliza maswali na majibu ndipo nasi tujimwage jamvini.
Kuna wakati nahisi akili zetu za Chit chat(wengi wa wanaCC ni wanaMMU pia) huwa zinatufanya kuleta masikhara hata kwenye majukwaa nyeti.