Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich awekewa vikwazo na Uingereza

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
69,364
94,545
1646913009075.png

Tajiri wa Urusi, Mmiliki wa Club ya Chelsea awekewa vikwazo, vikwazo hivyo vinahusu mali zote zilizo UK na Club ya Chelsea yahusika

Uuzwaji wa Chelsea umesitishwa kwa muda. Chelsea haitaruhusiwa kuuza, kununua wachezaji.

Chelsea haitaruhusiwa kuongeza mikataba ya wachezaji waliopo.

Chelsea haitaruhusiwa kuuza jezi.

Kwa mbali naona makampuni yakiiacha Chelsea.
===
Mmiliki wa Club ya Chelsea Roman Abramovich ameongezwa katika orodha ya waliowekewa vikwazo nchini Uingereza na sasa mali zake zote zilizopo Uingereza zinashikiliwa na Serikali.

Mchakato wa kuiuza Chelsea pia umezuiwa, vilevile Chelsea imezuiwa kuuza tiketi kwa Mashabiki hivyo watakaokuwa wanaingia uwanjani kwa sasa ni wale tu wenye tiketi za msimu.

Bilionea huyo wa kirusi ambaye amekua akiishi Uingereza kwa zaidi ya miaka 20 anakuwa miongoni mwa Mabilionea 7 wa Urusi ambao mali zao zimewekewa vikwazo na baadhi ya mataifa kutokana na Urusi kuvamia Ukraine.

Mbali na hayo pia Roman amepigwa marufuku kufanya miamala ya pesa na Watu binafsi na pia Wafanyabiashara wa Uingereza, pia amepigwa marufuku ya kusafiri na vikwazo vya usafiri.

Chanzo: Millad Ayo
 
Hii hali sasa imekuwa ngumu eeeeeeeh eeeeeh

Washabiki wa chelsea sasa tutakula ndumu eeeeeh eeeeh

Mpaka tutajifunza hali nguma eeeeh eeeeh

Nimekumbuka wimbo wa fundi

(Juma Nature: Hii hali sasa imekuwa ngumu)
 
UK wanaona Chelsea inavipandikizi vya Roman ndio maana wamepanga kuimaliza kabisa

Kinachoenda kutokea Chelsea wachezaji watahama na timu jina litakufa pia utakuwa Kama kilabu ya kichangani
 
1646908464969.png

Mmiliki wa Club ya Chelsea Roman Abramovich ameongezwa katika orodha ya waliowekewa vikwazo nchini Uingereza na sasa mali zake zote zilizopo Uingereza zinashikiliwa na Serikali.

Mchakato wa kuiuza Chelsea pia umezuiwa, vilevile Chelsea imezuiwa kuuza tiketi kwa Mashabiki hivyo watakaokuwa wanaingia uwanjani kwa sasa ni wale tu wenye tiketi za msimu.

Bilionea huyo wa kirusi ambaye amekua akiishi Uingereza kwa zaidi ya miaka 20 anakuwa miongoni mwa Mabilionea 7 wa Urusi ambao mali zao zimewekewa vikwazo na baadhi ya mataifa kutokana na Urusi kuvamia Ukraine.

Mbali na hayo pia Roman amepigwa marufuku kufanya miamala ya pesa na Watu binafsi na pia Wafanyabiashara wa Uingereza, pia amepigwa marufuku ya kusafiri na vikwazo vya usafiri.

Chanzo: Millad Ayo
 
Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amewekewa vikwazo na serikali ya Uingereza kama sehemu ya hatua dhidi ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Yeye ni mmoja wa matajiri saba kupigwa vikwazo vipya, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kwa mali na marufuku ya kusafiri.

Orodha hiyo pia inajumuisha mabilionea Igor Sechin na Oleg Deripaska, wote wanaoonekana kuwa washirika wa Vladimir Putin.

Waziri Mkuu Boris Johnson alisema "hakuwezi kuwa na kimbilio salama" kwa wale ambao wameunga mkono uvamizi huo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Hii ni hatua nzuri sana kwa Uingereza, kuna njia nyingi za kupigana vita, hii ni mojawapo.
 
Hapo kwenye miaka 20+, ni muda mrefu sasa tangu Roman apigwe marufuku kuingia Uingereza….. hana mahusiano mazuri na serikali kwa miaka mingi tu.
 
Mtaji wa Timu za England ni kama ifuatavyo:-
Historia,
Mashabiki (hawa hawaami hata iweje)
Suala la Pesa na Mwekezaji linakuja baadae, Hivi unajua aliyoiuza Chelsea kwa Abramavich aliinunua kwa Pound Moja ?

Ilikuwa na Madeni na ilibidi anunue na madeni hayo na pia kuwekeza..., kwa sasa Brand ya Chelsea ilivyo hawatakosa kupata mwekezaji..., Ingawa Football as its Run kwa sasa its not sustainable timu nyingi zinaendeshwa kwa Hasara (Arsene Wenger ndio alikuwa anajua kuendesha timu kama Taasisi) na sio kutumia pesa ambazo hazipo au kutegemea a Godfather...

Itafika wakati mambo yatajiseti tu na timu nyingi zitakwenda under administration...
 
Uingereza walikua wanasubiri siku hii ifike kwa hamu wamminye kende billionaire baada ya kuona visa ya kuingia uingereza haitoshi. Kifupi serikali hawamtaki mtu huyu uingereza
 
Kwaiyo mali za huyu Oligarch sasa rasmi zitagawiwa ngawira, ni kipindi cha Ngawira tu na ufaransa juzi juzi wamezikamata meli mbili za urusi moja ilikuwa ya kampuni ya russia imesheheni na moja ni ya tajiri wa russia zote watu wamegawana Ngawira
 
Back
Top Bottom