Kiswahili sasa hivi ni kigumu, kila neno lazima ulitolee maana kabla ya kusema mengi.
Ulikuwa kwenye chuma mboga? Sitii neno.
Nyie kizazi hiki mwafaudu?!
Mambo waaa! Kuna nafasi ya ukatibu mukhtasi...tuma maombi...
Lizzy wa JF
S.L.P 31 PM
JF
Yah : maombi ya kazi
Ndugu rais wa wabeba mabox , naomba nafasi ya kazi ya katibu mukhtasi katika jumuiya yenu ya wabeba mabox. Naahidi kufanya kazi yangu kikamilifu na kwa uaminifu. Nitakua msikilizaji mzuri na kufuata maagizo ntakayopewa bila kusahau kufuata matakwa yako.
Naomba ufikirie maombi yangu tena na tena mpaka utakapokubali kunipa hiyo nafasi. Nakuahidi kwamba hutojuta kuniajiri.
Wako mtiifu,
Lizzy
Hujaweka sifa zako kama elimu, uzoefu wa kazi, n.k. Na pia tunataka majina matatu ya references.
Hata mimi nashangaa... watu hawalali? Au huko kwao ndio saa za kuamka?Wengine tulisinzia.
Hata mimi nashangaa... watu hawalali? Au huko kwao ndio saa za kuamka?
Wengi wanatumia PCs za maofisini. Wakirudi majumbani wenye visimu vyenye intaneti unaweza ukabahatisha kuwaona hapa na pale kama netiweki haisumbui. Kama neti inasumbua basi itabidi uwasubirie hadi kesho yake wakitinga tena ofisini.
Ila kwa akina kama sisi wabeba maboksi tuko online 24/7 365/366. Teh teh teh...ngoja ninyamaze nsije nikaambiwa najidai bure....ingawa nimesema ukweli lol
Kiswahili sasa hivi ni kigumu, kila neno lazima ulitolee maana kabla ya kusema mengi.
Ulikuwa kwenye chuma mboga? Sitii neno.
Nyie kizazi hiki mwafaudu?!
Hata mimi nashangaa... watu hawalali? Au huko kwao ndio saa za kuamka?
Haya kongosho..muda wa kazi umefika! Funga upesi hiyo page ya JFDuh! Kweli dunia ni ya mviringo, na ukilala wenzio wanaendelea na kutengeneza pesa.
Hamlali jamani?
wengine tunalala na mito na midoli, usiku usingizi ukikata unaamua uingie tu jf.